Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Hilo sio zuio, ni ukweli.
Petrol ni maafa, isioo hifadhiwa vizuri.
Tangu enzi za mkapa walikuwa wanstumia mbinu Gani kupata hayo mafuta
Huu ni mradi wa kijinga mnataka kubuni au kuanzisha.
Ewura wanafanya kazi nzuri ni kibano kibakie hapo hapo
Wao ndo wanatusababishia kununua generators halafu acha ushamba, hata mashine za kukata majani zinatumia mafuta kujiendesha. Au tuzikojolee?
 
Kokota mashine yako ya majani hadi petrol station🤣🤣🤣🤣🤣.
Mnanichekesha nyie watu
 
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi), alizeti, n.k. Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Soma pia:

Thread 'Kukataa Wazo la REA Kujiusisha Kwenye Sekta ya Mafuta' https://www.jamiiforums.com/threads/kukataa-wazo-la-rea-kujiusisha-kwenye-sekta-ya-mafuta.2262255/
Uko Sahihi
 
Kuna dharura mtu umeishiwa mafuta maporini huko utasukuma gari mpaka mjini?? Na sio kila mji stesheni inakuwa karibu.
Watakuambia ujaze full tank.
Hawajui unaweza kupata tatizo tank likatoboka au 'pipe' ikakatika au kupasuka, Kuna kuibiwa mafuta (wapiga nyoka kwenye tank).
Kuna maji kuingia kwenye tank baada ya ajali n.k.
 
Kwani full tank haiishi kwani?
 
Tangu enzi za mkapa walikuwa wanstumia mbinu Gani kupata hayo mafuta
Huu ni mradi wa kijinga mnataka kubuni au kuanzisha.
Sijakuelewa hapo.
Fafanua vizuri unamaanisha nini?
Mradi gani?
Wakati wa Mkapa tulinunua mafuta kwenye madumu.
Wakati wa Mwinyi na Nyerere tulinunua kwenye magaloni maalum ya chuma ambayo sasa hayapatikani madukani labda yanayokuja kwenye baadhi ya magari hasa kampuni ya Land Rover au Jeep.
 
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi), alizeti, n.k. Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Soma pia:

Thread 'Kukataa Wazo la REA Kujiusisha Kwenye Sekta ya Mafuta' https://www.jamiiforums.com/threads/kukataa-wazo-la-rea-kujiusisha-kwenye-sekta-ya-mafuta.2262255/
Mungu akubariki na taarifa hizi ziakuwa zimemfkia Mh Waziri
Viongozi wetu wanayo mengi mno ya kufanya kwa wananchi wao na hivyo, wakati mwingine wanapitiwa; tuwe tunawakumusha pia; watafurahi kuwa wanasikia kutoka kwetu
 
Amen.
Na Sasa msimu wa kulima na tractor unakuja.
Likiishiwa mafuta haliwezi kutembea kilomita nyingi kwenda kujazia mafuta na kurudi tena shambani kuendelea na kazi.
Sababu ya kwanza muda, pili gharama za kuendesha tractor kufuata mafuta mara kwa mara, na tatu usumbufu.
 
Hukatazwi kununua mafuta kwenye kidumu bali kuna kidumu maalum kwa ajili ya petrol na diesel. Hili sio jipya. Huwezi kwenda kununua mafuta na dumu la maji ya uhai.
Na hii ndio sheria ninayoijua ila kusema eti ni marufuku hii hoja haina mashiko
Sheria ipo na tangu enzi watu wananua kwenye Jerry cans
Mtu anaenda na kibuyu
 
Kwa sasa hali ipo tofauti.
Nikuulize wewe, ndugu zako na rafiki wangapi wenye vifaa vya kutumia mafuta wanamiliki hizi special Jerry canes?

Hazipatikani madukani huko mikoani hata Dar yenyewe utazipata kwa shida.

Huku wilayani mkoani achana na kuzuiwa kununua na dumu bali ukikutwa umebeba mafuta kwenye dumu unakamatwa na tishio faini laki nane wasemavyo.
Huoni wametengeneza Chaka la rushwa ukikamatwa nayo?

Huoni wamiliki magari wataibiwa Sana mafuta na dereva wao kisha kuuza kwa magendo?
 
Nakumbuka miaka ya 60 mzee wangu alikuwa nayo kwenye Land Rover yake ila kwa sasa kila kitu hakuna na sheria hazifuatwi
Hata wenye viwanda wanaweza kutengeneza hizo ila serikali haijali mambo mengi sana
Ila kama kuna maslahi ya mkubwa utaona inavyochangamkiwa kama Helmets wakati ule

Sio wengi wanazo hizo cans na kama unavyosema hata madukani hakuna sasa hapo nani wa kumlaumu?
Ila kuuza kwenye chupa ya Lita moja ya Dasani ni sawa boss? Kwanza sio salama kabisa hata kwa watoto huko inakoenda
Mengi tunashindwa wenyewe na kusema zaidi umasikini
 
Hii hapana kabisa.
Hatari kubwa.
 
Kuna ile marufuku piki piki kubeba mkaa nayo inatakiwa kurekebishwa
 
Naomba kusaidiwa taarifa - kwa hapa Dar wapi hizo Jerry can za chuma zinauzwa?
 
Back
Top Bottom