Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Waziri wa Sheria, Damas Ndumbaro akiwa kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya WILDAF yaliyohudhuriwa na Rais Samia amewataka wanaume wanaotaka kuwania Urais wakapumzike kwani aliyepo shughuli anaiweza barabara.
Ndumbaro ametaka wanawake waongoze nchi hata miaka 20 na kama wanaume wanataka kwenda kombe la dunia lazima Rais awe mwanamke kama wanawake walivyoweza kufika robo fainali.
=======
Damas Ndumbaro: Tumepata Rais wa kwanza mwanamke, sidhani kama kuna mafanikio makubwa kama hayo, rai yangu kwa nyinyi wanawake wapigania haki za wanawake, hapa tuliposhika tusiache.
Sisi kule Songea, wangoni tunaimba kwamba ninapotaka mimi ni hapa tu, sisi tunasema tunapotaka sisi ni hapo tu, tumefika.
Kwahiyo sisi wanaume ambao tulikuwa tunavizia vizia hii nafasi ya Urais hebu twende likizo kwanza. Hii shughuli sio yetu, siku hizi ina wenyewe hii, ndio ukweli na mbaya zaidi huyo mwanamke ambae ndio Rais kazi anayofanya hakuna wanaume ambao wanaweza kuifanya.