Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Hajawekwa bure huko kwenye afya ni uozo mtupu. Mafarmasia na boharia kazi kubwa kuuza dawa za serikali haziwafikii wagonjwa. Kwani hamsikii kila mahali wamama wazee vijana wakidai kazi ya pharmacia imekua kuelekeza wapi wagonjwa wakanunue dawa wakati hospitali zinapatiwa dawa? Kama duka lako la dawa unauziwa dawa za serikali ndio utamuona huyo mama ni wazimu. Huko kwa kina mama bado wanaambiwa waje na vifaa kujifungua au wanauziwa na manesi. Mtu unayeona hiyo hali mbaya ni sawa ndio utamchukia huyo mama.
Mapambano na fisadi na wazembe bado yanaendelea hadi wote tuona ufisadi na uzembe sio kitu cha kukubaliwa kama ndio kawaida.
Viva mama gwajima tunakutakia ushindi kusafisha wizara ya afya.
Hamna chochote anachofanya huyo mama zaidi ya utopolo tu
 
Acha maza aendelee kutuburudisha kwa vichambo.

Nampenda huyu mama kwa staili yake ya kuongea...
Pole sana mkuu,unashangilia madaktari wetu kunyooshwa badala ya kutiwa moyo?

Madaktari wetu wanahitaji kufanya kazi katika mazingira tulivu bila kuingiliwa na wanasiasa

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kitu ambacho atujaonyeshwa kwenye hizi clips hadi yeye kujitapa; ni auditing skills alizotumia hadi kubaini uongo waliotaka kumletea.

Ndio maana huwa anasema angekuwa mtu mwingine si wangemribuni kirahisi ila sio yeye wakajipange.
 
Wakuu habari za mchana....
Wewe na wenzako acheni wizi wa madawa.mama yuko sawa acheni majungu. Mnataka waziri aje mumfungulie milango ya gari kisha mumdanganye aondoke?

Wizara ya afya ni moja ya wizara nyeti sana nchini ikihusu uhai wa WATANZANIA.

Pia wizara hii imejaa ufisadi wa kutisha kwa muda mrefu sana.

Mfano ni hivi majuzi pale MOI muhimbli na hapo UKEREWE.

Acheni mama asafishe uozo.
Mngekuwa wastaarabu msngeiba madawa na kuacha ndugu zetu wakifa mahospitalini

SHAME ON ALL OF YOU THIEFS
 
Kuna priority Mkuu, una Paracetamol chache mtu anakuja na mild pain ukimwangalia unamuona kbs akipumzika maumivu yanaweza isha sasa kwanini usizitunze ili akija mwenye maumivu makali ndo umpe
Sasa kwanini daktari amwandikie mgonjwa paracetamol kwenye prescription note. Si angemwambia akapumzike hayo maumivu yake sio makubwa yatapoa.

Kama ni uhaba pia kuna swala la uzembe ambalo alishalizungumzia kwenye ziara yake nyingine wanatakiwa kuelewa maswala ya inventory control sio unakaa mpaka dawa zinaisha kabisa ndio maana anataka appraisal system sasa ya wafanyakazi kwenye hivi vituo vya afya inaonekana kuna watu wana nafasi huko mahospitalini wakati hawana qualification nor training za health management.

Kilichotokea hapo japo akijaonyeshwa walitaka kumuongopea dawa hakuna yeye akatumia auditing skills zake ikabidi waseme ukweli ndio maana akawaambia angekuwa mwanasheria si wangemuongopea because you don’t think they would do know how to go about to uncover the truth.

Hiyo wizara imepata kiboko yake, sema anaonekana mama ana akili na watu wenye akili wanatabia ya dharau wanapoongea hiyo kidogo ndio inaweza onekana kama weakness yake kwa watu wengine, but me like it.
 
Back
Top Bottom