Katika nafasi ya uwaziri naungana nanyi kwamba amepanic na anajikuta hajui msaidizi yupi anaweza kumfaa na yupi ampatie majukumu gani, pia ana tatizo la kuamini vile anavyojua yeye ndio sahihi.
Kuhusu kuleta mabadiliko, aliweza alipokua TAMISEMI kwasababu baadhi ya mbinu zake zilihusisha kuimarisha mfumo mzima wa utendaji kazi vituoni, tofauti na sasa ambapo anatoa matamko yasiyokua na mbinu mbadala za utatuaji.
Kikubwa kinachomtesa ni ahadi ya chama chake kuhusu Bima ya Afya kwa wote iliyotolewa kwenye ilani, ukizingatia Bima hiyo anaifahamu vizuri utekelezaji wake katika kundi kubwa ni mgumu, maana ni yeye alieianzisha akiwa Iramba, ikaja kumsumbua akiwa RMO Singida baada ya kuhamisha makusanyo kutoka wilayani kuja mkoani. Kwahiyo anajaribu kuhamasisha wananchi wajiunge lakini anajua kabisa ile bima ni tatizo.
Kuhusu watu anaowatuhumu kuwa wezi na waongo (amemuambikiza na naibu wake), ni ngumu sana kuwa sahihi kwenye utunzaji wa rekodi za matumizi ya dawa, hasa kutokana na changamoto ya upungufu wa watumishi iliyopo nchini. Bahati mbaya sana Mama haamini kwenye uhaba wa watumishi, yeye anadai watumishi wapo wa kutosha lakini hawawajibiki.
Kujiita Field Marshal nadhani yupo sahihi kwenye sekta yake (tuzingatie kwamba hajasema yeye ni Field Marshal wa sekta ya afya, amesema yeye ni Field Marshal kwenye masuala ya uongozi wa sekta ya Afya).
Ni sahihi kabisa kwasababu ni mtu alietoka chini kabisa, japo kwenye CV yake haijaonesha lakini inasemekana alianza kuhudumu kama RMA ndipo akapanda hadi kufikia MO, kaongoza kuanzia Zahanati, Wodi, Kituo cha Afya, Kitengo cha hospitali, hospitali, Idara ya afya wilaya, Idara ya Afya mkoa, kurugenzi ya huduma za afya katika wizara ya afya, bodi mbalimbali za hospitali na huduma za afya, Ofisi ya raisi - Afya na sasa Waziri wa Afya. Hauwezi kukuta yeyote mwenye experience zinazokaribiana nae.