Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Mkuu pesa za Majini zipo.Yule mganga njaa kama mimi tu ila mie dalali ye mwenzangu tapeli kwa kivuli cha uislam,,, hana tofauti na manyaunyau, kamchape, lambalamba etc. Ikiwa huyu Veronica kakili utapeli wake basi ni zamu ya yule anaejiita dokta sule nae atuthibitishie hayo majini yanaletaje ela,, mpumbavu tu yule njaa zake zinafanya auchafue uislam..
Kwa hiyo wamemlazimishaBINTI ALIYEDAI ANAISHI NA NYOKA AJISALIMISHA KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA
Aomba radhi, adai hajawahi kufanya hivyo alidanganya.
DAR ES SALAAM.
Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni kupitia televisheni ya MBENGO TV ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.
Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima , alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.
Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.
Leo 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.
Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.
Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.
MWISHO
NB; nawasihi wanajamii wote kuheshimu Sheria kwa maendeleo na ustawi wa jamii na kutunza maadili.
Pia soma: Epuka kusambaza maudhui yasiyo na maadili. Anayedai kumiliki nyoka na kushiriki naye tendo, ajisalimishe
View attachment 2995537
View attachment 2995538
Mh!Wazirii Gwajima, kuna jambo nataka likufikie, haijalishi utalikubali au utalikataa, ila lazima nikufikishie.
Binti anaitwa Veronica Bernard Anton lakini amevaa kama bint wa kiislam yote hiyo kuchafua waislam waonekane wanapenda kujishirikisha na ushirikina😂 ila hii nchi inavichaa sanaa
Ndiyo zipo ambazo ni za utapeli kama huu.M
Mkuu pesa za Majini zipo.
Zipo kabisa.
Na watu wanazipata na kuzitumia kama kawaida.
Dr. Sule haongopi, ni swala la kumwita tu aeleze zinapatikanaje ili zituletee maendeleo kwa jamii.
Zipo Mzazi
Naomba tushirikiane nipeni links hizo, mimi kazi yangu kutafuta sheria zetu zinasemaje Ili wakazijibu. Imetosha sasa. Watanzania tunapenda kuomba sheria iandaliwe lakini ikiandaliwa utekelezaji unakuwa chini Sana na wengi wanakuwa hawajui kabisa na matokeo yake ni mazoea ya makosa. Sasa wote kama jamii tuungane kuzitekeleza. ShukraniDr Gwajima nakukubali sana Mama umefanya vizuri.
Usiishie hapo Wanawake na wasichama wadogo wamejikuta wakijiingiza kwenye vitendo viovu kutokana na shuhuda za uongo.
Pia huko Instagram na face book wapo.
Na makanisani nako pia Wanawake wanaangamia kwa shuhuda za uongo zinazoambatana na imani za kidini
Mimi narejea sheria tu... Na wewe nisaidie tusome. Kisha naenda kwa msajili wa huduma yao. Mambo yasiwe mengi, tujue tunaitekeleza au tunaifuta hiyo sheria. Maneno yawe machache vitendo viwe vingi,KWA MANABII JE WANAOWAPA REHEASAL WAUMINI WAO ILI KULANGAI UMMA HAPO UNAFANYAJE MH., MAANA WANAPOTOSHA JAMII AMBAYO MH, NDIYO MWENYE DHAMANA.
-mtu ametapika nyoka
-mtu ametapika misumari wa nchi nne
-mtu ametapika viwembe,
Yaraabih!
Ajabu ni kuwa wapi walioamini na wanakiri kabisa "mimi nilidhani ukweli". Tusipowalinda watu wetu Iko siku watabebwa na hawa matapeli wakamezwe na hayo machatu. Unakumbuka kisa cha ile nchi watu wakapelekwa msitu ule jina linaanza na Shakao....... Unadhani ni nini? Kuaminishwa....Kama utakuwa uliamini ile story ya nyoka,wewe ni mmoja wa Watanzania wanaochangia umasikini na unatakiwa ufe kwani hauna faida yoyote hapa duniani.
Hatuwezi kufumbia macho, wa kuiponya Afrika ni mimi na wewe, tuungane tuSiku ujinga ukifutika vichwani mwa Waafrika, ndipo siku tutayouaga umasikini...
Yaani ujinga umekuwa ndio akili ya kwanza ya Waafrika
Ukiona umeenda kupata huduma ya serikali hupewi ushirikiano na watoa huduma, hilo nalo ni kosa. Toa taarifa kwa wakubwa wake kwenye taasisi hiyo. Mfano, Jeshi la Polisi Kila kituo wametangaza namba zao hapo wamebandika kuanzia ya IGP 0699998899 na mimi namba za kituo cha simu wizarani kwangu nilishatangaza nikaongeza na zangu binafsi muandike ujumbe 0765345777 kopi 0734124191. Mwisho kabisa, unaruhusiwa kusoma sheria uchukue hatua.. lengo la Serikali wananchi wapate huduma, sasa makosa ya mtu mmoja mmoja siyo lengo la Serikali tafadhali. Shukrani kwa mchango wako kwenye mjadala.Kazi nzuri muheshimiwa.
Japo na swali dogo nakunukuu
"Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali."
Muheshimiwa hivi ikitokea serikali haitoi ushirikiano kwa raia, je raia anatakiwa kufanya nini ama taratibu ipi inafanyika?
Pole na hongera kwa majukumu muheshimiwa
Ndugu yangu, Ili kusafisha jamii tunahitaji ushirikiano wa Kila mtu bila kujali itikado yake. Naomba ushirikiano wako.Zikiripoti habari za Chadema za Ukweli zinapigwa vita ila ziki ripoti habari za uongo na uchochezi ndio kwanza wanakaribishwa White house.
Tuna shida mahara Ndugu Waziri Dr Gwajima.
Ahsante Sana, naomba tu Kila anayeoona uongo uongo fulani kwenye Kila link basi tupeane ushirikiano. Maana naweza nikawa kuna link inaendelea mahali na mimi sijaiona na watu wanapotea.Dr Gwajima nakukubali sana Mama umefanya vizuri.
Usiishie hapo Wanawake na wasichama wadogo wamejikuta wakijiingiza kwenye vitendo viovu kutokana na shuhuda za uongo.
Pia huko Instagram na face book wapo.
Na makanisani nako pia Wanawake wanaangamia kwa shuhuda za uongo zinazoambatana na imani za kidini
Hawana lolote uongo utapeli kabisaWanafosi ionekane uchawi upo na wao wana miujiza ya kuutibu
Safi, werevu wachache, tunafahamu utapeli huo, lakini ni jukumu letu kuwalinda wale wengi dhidi ya mitego hii.Ajabu ni kuwa wapi walioamini na wanakiri kabisa "mimi nilidhani ukweli". Tusipowalinda watu wetu Iko siku watabebwa na hawa matapeli wakamezwe na hayo machatu. Unakumbuka kisa cha ile nchi watu wakapelekwa msitu ule jina linaanza na Shakao....... Unadhani ni nini? Kuaminishwa....
Yale yale mtu akivaa kanzu mnasema kavaa kiuslamu. Hayo si mavazi ya Kiislamu.Binti anaitwa Veronica Bernard Anton lakini amevaa kama bint wa kiislam yote hiyo kuchafua waislam waonekane wanapenda kujishirikisha na ushirikina😂 ila hii nchi inavichaa sanaa