Dkt. Gwajima: Tukatae utapeli, Binti aliyedai anaishi na nyoka akiri haikuwa kweli

Dkt. Gwajima: Tukatae utapeli, Binti aliyedai anaishi na nyoka akiri haikuwa kweli

Inshu ni kwamba serikali yetu haitaki kuamini kuhusu uchawi ila hayo mambo sio kwamba hayapo yapo sana tena sanaaa.

Mimi nadhani wewe kama waziri mwenye dhamana ya jinsia jikite sana kwenye maadili hususani mambo ya kukemea ushoga,usagaji tungeni sheria kali pia tazameni sana nyimbo za wasanii kama WASAFI

Zina matusi ya kutosha sana yule nasibu na wenzie ni ttzo.

Kwako daktari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la uchawi ni ugumu wa kuthibitisha kama upo na unafanya kazi, linabaki kuwa suala la imani na mapokeo tu.
 
KWA MANABII JE WANAOWAPA REHEASAL WAUMINI WAO ILI KULANGAI UMMA HAPO UNAFANYAJE MH., MAANA WANAPOTOSHA JAMII AMBAYO MH, NDIYO MWENYE DHAMANA.
-mtu ametapika nyoka
-mtu ametapika misumari wa nchi nne
-mtu ametapika viwembe,
Yaraabih!
Kuna mmoja alijisaidia bawaba 4 kubwa za milango. Ila Mwamposa, Mungu anakuzoom tu.
 
Ajabu ni kuwa wapi walioamini na wanakiri kabisa "mimi nilidhani ukweli". Tusipowalinda watu wetu Iko siku watabebwa na hawa matapeli wakamezwe na hayo machatu. Unakumbuka kisa cha ile nchi watu wakapelekwa msitu ule jina linaanza na Shakao....... Unadhani ni nini? Kuaminishwa....
Unaweza kuwa unafanya kazi nzuri sana na hilo halipingiki, ila bila ushirikiano wa taasisi zingine matokeo hayatakuwa mazuri sana. Hongera kwa kuchapa kazi
 
Binti anaitwa Veronica Bernard Anton lakini amevaa kama bint wa kiislam yote hiyo kuchafua waislam waonekane wanapenda kujishirikisha na ushirikina😂 ila hii nchi inavichaa sanaa
Sidhani kama jina linaweza kuwa sababu ya Kujua Dini ya mtu moja kwa moja...

Kuna Dada namjua anaitwa Neema na siyo Mkristo....na anavaa zile za kufunika hadi uso....Haya...Na wewe unatumia ID ya Cleopatra...😅
 
BINTI ALIYEDAI ANAISHI NA NYOKA AJISALIMISHA KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA

Aomba radhi, adai hajawahi kufanya hivyo alidanganya.

DAR ES SALAAM.

Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni kupitia televisheni ya MBENGO TV ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima , alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.

Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.

Leo 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.

Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.

Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.

MWISHO

NB; nawasihi wanajamii wote kuheshimu Sheria kwa maendeleo na ustawi wa jamii na kutunza maadili.

Pia soma: Epuka kusambaza maudhui yasiyo na maadili. Anayedai kumiliki nyoka na kushiriki naye tendo, ajisalimishe
View attachment 2995537
View attachment 2995538
Mwamba uko vizuri sana aisee
 
Wewe si ndio mtetezi wa mashoga humu, unahisi atakuskliza? Mumeharibu jamii.
Tena mumechokwa haswa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nakuja kupiga panapoumaa, na ntapiga haswaa.

Nweii yeye ameshaelewa na kasema nishirikiane nae. Ko wee tulizana bwasheee.
 
Mwandikie hivi kwani nini watoto wakiume wana.........[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Tulizana bas nawee, uzi utakua umejishato hashwaa,
Mbona utafurahi mwenyewe, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Binti anaitwa Veronica Bernard Anton lakini amevaa kama bint wa kiislam yote hiyo kuchafua waislam waonekane wanapenda kujishirikisha na ushirikina😂 ila hii nchi inavichaa sanaa
kuvaa hivyo ni uislam?.Hizi ndio akili tunazozisema kila siku.Kwanza jina au mavazi havina uhusiano na dini ya mtu.
 
Sasa mh Gwajima, hao wasiishie kuomba radhi. Sheria haitambui kuomba radhi, wanatakiwa wafunguliwe mashtaka. Kila mmoja na yake na yale ya pamoja.
Kula njama, kusema uongo, kurecord na kupakia mtandaoni, kudaganya majina yake huyo dada n.k

Na mnaweza kuomba mahakama ifunge kituo mpaka kesi itakapokwisha. Adha waliyoisababisha katika jamii na wao waipate. Dawa ya moto ni moto zaidi.
 
Wapumbavu wakubwa hao.

Lakini yeye amesema anaitwa Victoria wewe umeandika Veronica.
Kwanini unasubiri mwenye nyoka ajitokeze wakati wahusika wa kukupeleka kwa mwenye nyoka uko nao?
 
BINTI ALIYEDAI ANAISHI NA NYOKA AJISALIMISHA KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA

Aomba radhi, adai hajawahi kufanya hivyo alidanganya.

DAR ES SALAAM.

Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni kupitia televisheni ya MBENGO TV ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima , alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.

Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.

Leo 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.

Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.

Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.

MWISHO

NB; nawasihi wanajamii wote kuheshimu Sheria kwa maendeleo na ustawi wa jamii na kutunza maadili.

Pia soma: Epuka kusambaza maudhui yasiyo na maadili. Anayedai kumiliki nyoka na kushiriki naye tendo, ajisalimishe
View attachment 2995537
View attachment 2995538
Wale wasio na ajira, biashara wajikite kwenye uganga wa kienyeji wa kupiga Ramli, ushehe wa kudai wanasafisha nyota na kukuepusha na majanga.
Kwa wabongo na akili zao za kiimani imani UTAPIGA HELA MPAKA HUTAAMINI...
Mfano wakina Mwamposa...
 
Back
Top Bottom