Dkt. Gwajima: Tukatae utapeli, Binti aliyedai anaishi na nyoka akiri haikuwa kweli

Yule nyoka kwenye video alikuwa wa ukweli au photoshop? Mbona huyu dada hakuzungumzia alipompeleka huyo nyoka wake baada ya kuomba radhi?
 
Mama Gwajima Shkamoo...

Vipi lile jambo letu la ndoa za kikatoliki tunaomba kupewa kibali, nataka nifunge ndoa takatifu na Poor Brain kwenye kanisa la ST PETERS hapo dar mwezi ujao.

Natumai nitapata leseni kutoka ofisi yako yenye uzalendo mkubwa. Ahsante.

Ni mimi katika ujenzi wa Taifa, BICHWA KOMWE.

Cc: Lamomy cocastic
 
Kama utakuwa uliamini ile story ya nyoka,wewe ni mmoja wa Watanzania wanaochangia umasikini na unatakiwa ufe kwani hauna faida yoyote hapa duniani.
Tatizo siyo kuiamini, tatizo kubwa zaidi ni kule kuitazama na kuisikiliza kuongeza viewers.

Hata wewe ulishiriki kosa hilo, unatakiwa uwe umeuawa kwa kubutuliwa komwe lako.
 
BINTI ALIYEDAI ANAISHI NA NYOKA AJISALIMISHA KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA

Aomba radhi, adai hajawahi kufanya hivyo alidanganya.

DAR ES SALAAM.

Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni kupitia televisheni ya MBENGO TV ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima , alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.

Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.

Leo 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.

Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.

Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.

MWISHO

NB; nawasihi wanajamii wote kuheshimu Sheria kwa maendeleo na ustawi wa jamii na kutunza maadili.

Pia soma: Epuka kusambaza maudhui yasiyo na maadili. Anayedai kumiliki nyoka na kushiriki naye tendo, ajisalimishe
View attachment 2995537
View attachment 2995538
Utapeli upo hadi makanisani hawaoni?
 
kuvaa hivyo ni uislam?.Hizi ndio akili tunazozisema kila siku.Kwanza jina au mavazi havina uhusiano na dini ya mtu.
Akili unazozisema kilasiku zinanini? Hebu nenda sehem inayoishi jamii ya waislam wengi ukaone mavazi yao mfano Saudiarabia, dubai, Iran na Zanzibar,tuu hapo katizame wanavyo vaa
 
Utapiga pigaje sasa, isije kuwa unaomba Dkt.Mheshimiwa, Eti Aombe ruhusa kwa papa wa italy eti halalishe ushuwaini wa matacooo[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mbonaa km unaogopaa sanaa? Mie nitaongea nae km kiongozi wa idara.
 
Mama Gwajima Shkamoo...

Vipi lile jambo letu la ndoa za kikatoliki tunaomba kupewa kibali, nataka nifunge ndoa takatifu na Poor Brain kwenye kanisa la ST PETERS hapo dar mwezi ujao.

Natumai nitapata leseni kutoka ofisi yako yenye uzalendo mkubwa. Ahsante.

Ni mimi katika ujenzi wa Taifa, BICHWA KOMWE.

Cc: Lamomy cocastic
Wizooo naomba niwe MC Plz. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huko makanisani kumechafuka hatari kunashuhuda ambazo hata kuskia mbele yafamilia ni aibu kubwa mno kwani zinafedhehesha sana na ni aibu mno.
Hivi nilini majanga kama haya nayo yatafanyiwa kazi ipasavyo.
 
Wewe ndio acha udini tizama umekosa la kusema unaanza kusema naingia msikitini kwa jina la cleopatra😂 unashindwa kusema ukweli kwakuwa upo dini fulani pole wee unaumaskin wa fikra jombi
Hiyo Spana nimekupiga m,Acha udini na usijizungushe.Panua mawazo yako ya fikra usigawe watu kwa mavazi kama hawa wana haki miliki na Hilo ni vazi Lao.
 
Sasa spana imenipiga vipi mjomba mbona unamameno ya kishangingi😂 nenda basi kwenye nyumba za maaskofu na mapadre kisha unambie kunamwanafamilia gani wa kike utamkuta anashinda na mabaibui na mitandio nyumbani😂 kisha sina muda wa kubishana mwanaume mzima unashindana na mtoto wa kike unamapungufu ww kajichungulie
 
BINTI ALIYEDAI ANAISHI NA NYOKA AJISALIMISHA KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA

Aomba radhi, adai hajawahi kufanya hivyo alidanganya.

DAR ES SALAAM.

Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni kupitia televisheni ya MBENGO TV ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima , alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.

Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.

Leo 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.

Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.

Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.

MWISHO

NB; nawasihi wanajamii wote kuheshimu Sheria kwa maendeleo na ustawi wa jamii na kutunza maadili.

Pia soma: Epuka kusambaza maudhui yasiyo na maadili. Anayedai kumiliki nyoka na kushiriki naye tendo, ajisalimishe
View attachment 2995537
View attachment 2995538
Mheshimiwa Waziri Hongera sana sana, Mwenyezi Mungu akulinde na kukutia nguvu ili tuliokoe Taifa na watoto wetu kwa manufaa ya kizazi kijacho. Kuna mapendekezo mazuri naandaa nitakutumia ili endapi yatafanikiwa yatarahisisha kutoa suluhisho la kudumu kuhusiana na tatizo hili kubwa la mmomonyoko wa Maadili.
 
Back
Top Bottom