Dkt. Harrison Mwakyembe ajilipua suala la Ushoga; Kukabidhi jina la Mwenyekiti wao kitaifa na mikoa kwa Serikali

Dkt. Harrison Mwakyembe ajilipua suala la Ushoga; Kukabidhi jina la Mwenyekiti wao kitaifa na mikoa kwa Serikali

Wanasema Wazungu wanataka tupotee wote halafu wao waje kuishi Africa sababu Africa kuna resources nyingi wanazitaka [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]

Nimewauliza pia wale Mashoga wa Sodoma na Gomora Wazungu nao waliwapa Dawa za Meno na Perfumes?

Wameishia kutukana [emoji28]

The thought process ya watu wetu ipo flawed hadi huruma 🤣
 
Umenifungua macho kumbe kulikuwa na Viongozi wa dini Wengi?
Mwakyembe ni agent WA Taasisi moja ya kidini.....


Lakini Vile vile huyo dada aliechora tattoo inasemekana ni lesbian maarufu na alikuwa na tattoo ya mbunge mmoja viti maalum kaifuta...

Halafu kama ni toka mwaka 2016 yeye Mwakyembe alishindwa nini kuja na hizo sheria alipokuwa waziri wa sheria??....why makelele now??
Kheee! mapya yanafunguka kumbe mwanahabari na yeye ni blender akaamua kuwasagia kunguni wenzie [emoji28]

BICHWA KOMWEE
Yoda
cocastic

Mkuje mkuje
 
Acha kujinyongesha na wewe, sipendi watu wanaojitilisha huruma bila sababu hiyo 'maskini' haipo hapo kama hali bali imetumika kama kivumishi, (umehurumiwa) sasa mambo ya utajiri, hewa yametoka wapi? Kama upo soft heart kaa mbali na mijadala ya hivi, utapata presha shauri zako,

Wewe huwezi kunipa mimi ushauri nipo jf tangu mwaka 2014, ushauri wako ukurudie wewe mwenyewe mimi sihitaji kujitilisha huruma ili nionekane mchangiaji bora, nachangia kulingana na mada,

Fyi, boss wangu mwenyewe ni mzungu usiniambie kuhusu ngozi nyeupe nawajua vema,
Umeulizwa swali jepesi sana kati ya Wazungu na Weusi ni wakina nani wanajazana kwenda kwa wengine? Unasema eti Weupe wakija hawataki kurudi lol wangapi hao si tungekua tunapishana nao kila pembe kama sie tulivyojazana kwao,

Endelea kujifariji lakini ni nzuri kwa Afya yako ya Akili [emoji847]

Sasa kama wewe hautaki kushauriwa mbona na wewe unalazimisha watu waamini unachoongea? Itoshe kusema kila mtu abaki na misimamo yake...Kama wewe unaamini katika ushoga endelea kuamini Ushoga na usillazimishe watu wazibuliwe mitaro ila sisi tunaoamini kwamba ushoga siyo sawa unapawa kukemewa tunaendelea na hiyo misimamo.

Mimi siyo mnyonge ndiyo maana nimepata Guts za kukujibu ,ningekuwa mnyonge nisingeweza hata kuanza mikiki na wewe,mimi nia bandidu siwezi kuwa heartbroken na trollers wa JF.

Wanajazana kivipi ,ulishwahi kufanya utafiti waafrica wangapi wapo bara la ulaya na wazungu/ngozi nyeupe wangapi wapo bara la africa? Kisha angalia % yao kisha ulete majibu ,hatutaki nadharia tu za vijiweni ,wewe ulishawahi kuwa mzungu huko bara la ulaya ukaona unapishana na waafrica wangapi? Sasa kama unakaa Buza utapishana na wazungu wapi? Ushawahi kukaa Prime areas africa? Ushawahi kwenda Migawaha iiyopo prime areas? Wateja wa pale ni watu wa aina gani? Kila sehemu kuwa na watu wa aina fulani na ndiyo maana ukienda DC Washington blacks ni wa kuwatafuta. ...Ungekuwa unakaa Obay au masaki ungekuwa unapishana na wazungu daily.
 
Utakuwaje mtafiti umejikoboa juso lote limeiva kama TUZI YA PANYA?

Kwanza anaonekana ni MENTALLY RETARDED, kwa sababu huwezi kuwa na akili timamu ukajisindika makemikali kwenye juso lako. Hata huo utafiti wake umejengwa juu ya MENTAL INCAPACITY, hence NULL AND VOID.

Angeanza kwanza kutafiti mikorogo anayotumia kabla ya kujisindika na kujikoboa juso lote ndembendembe jekundu nduuu nduuu!!!

Huyu hana utafiti wowote ule, ni kahaba limeokotwa BUGURUNI MALAPA ili kutuzuga watanganyika kwa hadithi za kusadikika.

Anatikisa vikalio vyake viko kama NUKTA FAKTI anajizungurusha huku anawasha screen eti anaonyesha picha ya mzungu!
Jamaa n wewe ni mwanaupinde Nini?....mbna unamshambulia huyu dada wakat aliyosema yanaonekana kweny jamii zetu kipnd hiki?
 
Mkuu waulize swali moja tu la msingi; ni nani humu ndani anamjua shoga hata mmoja tu personally achana na hawa wa mitandaoni? Watu wanaua nzi kwa nyundo kwenye hii ishu. Wanatumia nguvu kubwa kupambana na a non-existent issue wakati mambo ya msingi yapo kibao ya kujadili yanayomgusa kila mmoja.
Hilo swali wanaulizwa kila siku wanaishia kuwataja watu maarufu ambao nao ni hearsay tu, huwezi ukasema fulan ni shoga kama yeye hajajisema,

Sahihi kabisa wanalazimisha watu tuone ushoga ni tishio kubwa wakati hamna kitu chochote, wajanja wanatembea na hii kiki huku mambo yao yanaenda bila vikwazo
 
Hivi wewe unajielewa kweli?
Mabaunsa wanatumia dawa za kutumisha misuli baadae wanakua mashoga unajisikia hata unachokiandika?

Nipe maana ya Ushoga kwanza ili nijue kama una uelewa au ndio wale wale wa vijiwe vya kahawa na kubet

Najielewa sana wew mtetea mashoga LBGT ,mimi nazungumzia Mashoga Mabaunsa nimekuwa specific siwazungumzii nyie mashoga wakoboaji.
 
This is far-fetched.

Kwanza ijulikane estrogen (female hormone) hata wanaume wanazo naturally and vyakula vya Kila siku vina ongeza estrogen kwa wanaume na bado wengi tu sio mashoga. Haiwezekani a one time dosage tena ya toothpaste na perfume imfanye mtu awe shoga. Haiwezekani. Halafu wewe mwanaume na ndevu zako unakubali zawadi ya perfume na toothpaste kweli? It will take a truckload of it kumgeuza mtu awe shoga.

Hivi mizungu iwafanye nyie muwe mashoga kwa umuhimu gani hasa?

Ushoga unaanza au kupingwa at a family-level. No more, no less. Msikimbie majukumu yenu. Mashoga wengi wameanza hii michezo majumbani mwao sio shuleni wala sehemu nyingine.

Kila research Ina agenda yake sijui huyu dada agenda yake ni ipi. Itakua kasoma upepo kaona mitanganyika inapenda story za ushoga kajiongeza.
"Hivi mizungu iwafanye nyie muwe mashoga kwa umuhimu gani hasa?"

Wale Wajerumani waliowahi kufukuzwa nchini sababu ya kuwalazimisha Ke kufanya ngono na mmbwa walikuwa na umuhimu gani kwa hao Wazungu?

Ulikuwa hujazaliwa nini?

Akili, Akili, Akili......[emoji848][emoji57]
 
Kheee! mapya yanafunguka kumbe mwanahabari na yeye ni blender akaamua kuwasagia kunguni wenzie [emoji28]

BICHWA KOMWEE
Yoda
cocastic

Mkuje mkuje
Kwani hata huyo mwakyembee?? Alivyowaharibu wanafunzi wa Udom?? Mwingne si yupo UVCCM palee,

Kwan yeye hajui hilo? atulie km hapati bottom kisa uzee wake, akae kwa kutulia tyuuh. Lol
 
Sasa kama wewe hautaki kushauriwa mbona na wewe unalazimisha watu waamini unachoongea? Itoshe kusema kila mtu abaki na misimamo yake...Kama wewe unaamini katika ushoga endelea kuamini Ushoga na usillazimishe watu wazibuliwe mitaro ila sisi tunaoamini kwamba ushoga siyo sawa unapawa kukemewa tunaendelea na hiyo misimamo.

Mimi siyo mnyonge ndiyo maana nimepata Guts za kukujibu ,ningekuwa mnyonge nisingeweza hata kuanza mikiki na wewe,mimi nia bandidu siwezi kuwa heartbroken na trollers wa JF.

Wanajazana kivipi ,ulishwahi kufanya utafiti waafrica wangapi wapo bara la ulaya na wazungu/ngozi nyeupe wangapi wapo bara la africa? Kisha angalia % yao kisha ulete majibu ,hatutaki nadharia tu za vijiweni ,wewe ulishawahi kuwa mzungu huko bara la ulaya ukaona unapishana na waafrica wangapi? Sasa kama unakaa Buza utapishana na wazungu wapi? Ushawahi kukaa Prime areas africa? Ushawahi kwenda Migawaha iiyopo prime areas? Wateja wa pale ni watu wa aina gani? Kila sehemu kuwa na watu wa aina fulani na ndiyo maana ukienda DC Washington blacks ni wa kuwatafuta. ...Ungekuwa unakaa Obay au masaki ungekuwa unapishana na wazungu daily.
Nani kakulazimisha uwe shoga?
Yaan kuna mtu kakwambia Savimbi njoo tuku^^^, acha masikhara bhana, sidhani kama kuna watu wamefikia huko [emoji2296]
 
Kwani hata huyo mwakyembee?? Alivyowaharibu wanafunzi wa Udom?? Mwingne si yupo UVCCM palee,

Kwan yeye hajui hilo? atulie km hapati bottom kisa uzee wake, akae kwa kutulia tyuuh. Lol
Aweeee, kumbe ana makando kando yake yake [emoji15]
Kuna mtu kamblackmail nini akaona ajiwahi kujisafisha kabla file halijawekwa mezani [emoji23]
 
Wenye enjio zenu zenye ma sponsa huko nje mmekuja kwa Kasi sanaa kumshambilia dada wa watu
Wanadai mara oooh...Dada wa Watu kajichubua, mara oooh! Uchunguzi wao ni batili.

Mara oooh Waziri Mstaafu Mwakyembe alikuwa wapi kutoa hizi inshu alipokuwa madarakani, kila kitu kina taratibu zake kiuchunguzi na kiushahidi.

Mashoga yamechemka vibaya sana kujibu hoja na kukimbilia kumshambulia yeye binafsi Dr. Mwakyembe na Bi Catherine.
 
Hii stori ya mwakwembe inataka kufanana kama ile ya vigogo wa dawa za kulevya ambayo tuliambiwa tutatajiwa majina yao wakiwemo watu mashuhiri ila hatukuambiwa hadi leo. Ni habari sensintive inayoweka watu attentive kusikia majina ya hao vigogo wa ushoga. Isije ikawa ni approach ya kisiasa mwakwembe anataka kuifanya kupitia mvumo wa ushoga
 
Nilimsikiliza Mwakyembe wakati anatoa hoja kuhusu Ushoga na Usagaji.

Ni ukweli kuwa Ushoga na usagaji ni matendo machafu mbele ya jamii na mbele za mungu. Hilo halina ubishi labda uwe mwendawazimu.

Uwasilishaji wa Mwakyembe ulikuwa wa kisiasa zaidi kwa lengo la kupata umaarufu wa kisiasa (Cheap politics). Mwakyembe alikuwa waziri mwandamizi kwa miaka mingi.

Kitendo cha kuihusisha serikali na ushoga na usagaji na kuitolea shutuma nzito kuwa wizara ya afya ina engineer na kwamba kila kitu kinajulikana kwa miaka mingi tangu yeye akiwa waziri mwandamizi ni upotoshaji wa wazi wenye kutafuta umaarufu tu.

Mbona siku zote hizo mwekyembe alikuwa kimya huku akijua ushoga na usagaji ni jambo baya. Kwa nini hakuwahi kusema hata bungeni? au kujiuzuru uwaziri kuonyesha kuwa anapinga serikali ku support mashoga na wasagaji?

Kuituhumu Marekani kuwa inatuletea ushoga na kwamba hataki pesa za wamerekani na nchi zingine zilizo na sheria zinazolinda haki za mashoga na wasagaji ni kuichonganisha serikali yetu na marekani ili ku gain cheap politics.

Marekani na nchi zingine zinazotupa misaada (Grants) hawajawahi kutuwekea sharti la kukubali ushoga ndo watupatie misaada.

Kuanza siasa za kuituhumu marekali kuwa inatuletea ushoga bila hata ushahidi na kwenda mbali zaidi eti hatutaki hata pesa zao ni ulimbukeni na ujinga uliokithiri. Nitatoa mifano michache ili hoja yangu ieleweke vyema.

Marekani na nchi zingine ni washirika wetu wakubwa tena wanaotusaidia mambo makubwa kwa sekta muhimu inayogusa maisha ya watanzania wengi.

1. USA inafadhiri mifuko (Funding) lukuki kama Grants. Hatukopi ila tunapewa bure. Nitataja miwili tu mikubwa ambayo ni Global Fund na President's Emergency Plan for Aids Relief (PEPFAR) kupitia Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Mifuko hii ina zaidi ya miaka 15 ipo hapa nchini na imenufaisha watanzania wengi kwenye miradi ya Afya kama Malaria, TB & Leprosy, HIV AIDS na mingine mingi.

2. Miradi niliyoitaja hapo juu watanzania wengi imewagusa mmoja mmoja. Kama nchi tunapata dawa za chanjo kutoka WHO kupitia mfuko wa Global Fund. Tunapata dawa wa kufubaza virusi vya ukimwi kwa vituo vyote Tanzania (CTC centers) kupitia mfuko wa PEPFAR, Tunapata dawa za malaria kupitia mfuko wa Global fund, tunapata Dawa za TB na Ukoma (Leprosy) kupitia Global Fund etc

3. Kuna mfuko mwingine unaitwa Health Basket Funding (HBF), pia hii ni Grant siyo mkopo ambao unachangiwa na World Bank na nchi zaidi ya 15 ikiwemo Canada, Denmark, Ireland, Switzerland, German etc. Bila hawa jamaa Health system ya Tanzania ingekuwa ime collapse. Hawa ndo wanatupa pesa za kununua dawa na vifaa kwa ajili ya hospital zetu nchi nzima. Huu mfuko ni mkombozi kwa watanzania kwa afya zetu.

4. Kama kweli nchi zote nilizozitaja hapo juu 1, 2 & 3 zote zina sheria zinazowalinda mashoga ikiwemo marekani. Mbona hakuna kigezo walichoweka cha kwamba lazima ukubali ushoga kama sharti la kupewa fedha zile ambazo tunazipata kila mwaka kwa zaidi ya miaka 15 sasa kama anavyodai Mwakyembe?

5. Ni ujinga wa kiwango cha juu kwa mtu ambaye amekuwa waziri tena mwandamizi kusema hadhalani eti hatutaki misaada ya marekani kwa sababu wana support ushoga huku akijua kuwa marekani na washirika wengine hawajawahi kutuwekea sharti la kutupa pesa ili tukubali ushoga. Hizo ni cheap politics za Mwakyembe.

Hitimisho
1. Ni ujinga kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa mwamvuli wa ushoga. Mtu kama anaichukia marekani na washirika wengine kwa sababu zake basi aichukie kama yeye lakini siyo nchi. Marekani na nchi nilizozitaja zikikata Grants, Health system ya Tanzania ita collapse sababu ya wanasiasa wachache wanaotaka kuharibu mahusiano na nchi yetu na Marekani

2. Kama nchi tuangalie chanzo cha tatizo la ushoga na usagaji siyo kuhangaika na matokeo. Ushoga na usagaji ni matokeo tu, hao ni waathirika. Tuanze kuhangaika na mabasha na wasagaji siyo waathirika. Tuwekeze kuihamasisha jamii ichukie mabasha na tutunge sheria kali ya ku deal nao ili tukomeshe ushoga.

3. Kumwadhibu muathirika wa ushoga na usagaji ni uwendawazimu. Haina tofauti na kumwadhibu mtu anayevuta madawa ya kulevya ukamwacha muuza dawa za kulevya.
 
Aweeee, kumbe ana makando kando yake yake [emoji15]
Kuna mtu kamblackmail nini akaona ajiwahi kujisafisha kabla file halijawekwa mezani [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan alivokua anaongea, unajua kabisa yeye ni mdau, anajisafisha na hana chembe ya utakatifu. Lol.
 
Nakubaliana na Wewe na hatakwenye Tasnia ya Burudan kuna wabunge na wanamuziki nliambiwa yaani sikuamini macho yangu
Wapo tele! Yaan hata ukiambiwa fulani nae pelo... hutaamini

Wazee wa kazi mpaka mawasiliano washayafuatilia na wanayo wakajihakikishia kisha wakanyuti zao kimya wanautazama mchezo tu.
 
Mwakyembe amefilisika kisiasa.
Tangu atumike kumchafua lowasa kipindi kile huyu jamaa namuonaga kama mnafiki flani ivi.

Nikipiga hesabu jinsi ambavyo hili swala la ushoga limetrend wakati huu hesabu zinakataa kabisa kukubali kuwa ni campaign ya kawaida. Hapana hapa kuna mtu ama/taasisi ametenga pesa ili kutu-keep busy na hii mada yenye ukakasi.

Sasa ni nani/ kina nani? sijui
Kwanini sasahivi? Sijui
Ana/ wanamalengo gani? Sijui

Inawezekana ni kwakua tunadai KATIBA MPYA!
Ama kuizima mikutano ya hadhara iliyo-ondolewa kizuizi haramu

Mimi sijui lakini mimi sio mbuzi wakupelekwapelekwa hovyo!
 
Back
Top Bottom