Dkt. Hussein Mwinyi adai Mzee Mwinyi hakuagiza azikwe Mkuranga

Dk. Hussein aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga kama sijakosea. Mbona Mkuranga ile ile suddenly imekuwa mbaya hivyo hata kuzikia tunapakimbia? Dah! Mkataa kwao?
Kama wewe ukiwa na option Mkuranga au Zanzibar unachagua wapi?
 
Dk. Hussein aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga kama sijakosea. Mbona Mkuranga ile ile suddenly imekuwa mbaya hivyo hata kuzikia tunapakimbia? Dah! Mkataa kwao?
Mkuu ukiona mtu anatumia nguvu nyingi kukanusha kinachosemwa ukweli uliowazi ujue anaogopa!

Pili, ukweli ni kwamba Hussein bila kubebwa hawezi kutoboa, hajiamini na bahati mbaya zaidi nguzo yake imeng'oka! Kina cha maji ya Zanzibar ni kirefu mno!

Meza zilishapinduliwa, hana political influence yoyote bara na visiwani! bila msaada wa Kingmakers, kuingilia kati hana chake!
 
📝🆒👍
 
Kutumia akili zetu kutafakari kilichotokea kwenye msiba wa aliyewahi kuwa kiongozi wa kitaifa, hakuwezi kuwa sawa na kumkosea heshima, usipotoshe.

Wewe ndie unayetukosea heshima sisi kwa kutaka tuwe wazembe kama wewe wa kukubali kila tunachoambiwa, ukweli ni kwamba wameenda kumzika Mwinyi Zanzibar kwasababu za kisiasa.

Na hata hilo jibu alilotoa Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar, nalo pia ni la kisiasa, sema kwasababu umeamua kulishwa kila kitu kama mtoto mchanga kwenye hili jambo, huwezi kuona hilo.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

Familia ya Mwinyi ina haki ya kumzika baba yao popote inapotaka bila kunyanyapaliwa.

Mnachofanya hapa kuleta majungu yasiyo na ushahidi wala uthibitisho ni kuinyanyapaa familia hii katika wakati wa msiba wao.

Mnajionesha nyie ni watu mliokosa hata chembe ya ustaarabu ya kusema tuwaache watu wazike wanavyotaka, kama siasa tutafanya kwingine, si kwenye mazishi.

Familia iliwaomba faragha tangu Mzee Mwinyi anaumwa, kwa kujua kuwa kuna watu wana majungu.

Na sasa Rais Hussein Mwinyi karudi kunyoosha maneno kwamba huo wosia mnaousema wao familia ndio wanaouhusika.

Sasa wewe ni mtu wa familia ya Mwinyi kuliko Hussein Mwinyi?

Mbona unashangaza sana?

Yani katika mabaya yote ambayo unaweza kuisema familia ya Mwinyi, umechagua hili la wapi wamemzika baba yao?

Hili ndilo umeliona la muhimu kabisa? Ulitaka kuwapangia wewe pa kumzika baba yao?

Hivi angezikwa Mkuranga napo mngeshindwa kusema kazikwa huko kisiasa kwa sababu Hussein anataka kugombea urais bara?

Acheni maneno yenu ya majungu yasiyo na ushahidi wala uthibitisho. Waacheni wenzenu wamalize msiba wa mzee wao bila maneno ya ovyo yasiyo na kichwa wlaa mguu.
 
Hayati mzee Mwinyi katuachia urithi mzuri sana, yaani kile kitabu chake. Humo kaeleza mengi tu. Hayo yanayotokea ni 'Uzanzibari na Uzanzibara.'
 
Mheshimiwa ni vyema ukawa mpole tu, kwani huko Zenji wana siasa zao. Ingawaje sijui kama wewe sio Mzenji. Ila kama ni Mzenji, hiyo ndio siasa yenu.
 
Na huyu aliyewahi kuwa mbunge wa Mkuranga ni Mzanzibari au Mtanganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…