Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Rais Samia amekabidhiwa shahada ya udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya 52 duru ya 5. UDSM imesema uongozi wa Rais Samia umeleta mageuzi ya kiuchumi na mengineyo, pia umeleta tumaini jipya.
Rais Samia amesemwa kuboresha elimu ikiwemo kujenga vyuo 25, kusaini na benki ya dunia mradi wenye thamani ya bililioni zaidi ya 900 wenye lengo la kuboresha elimu ya juu.
Rais Samia amemshukuru Dkt. Kikwete na baraza la seneti la chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kumpendekeza kupata tuzo hiyo na aliikubali kwa sababu siyo ya kwake pekee bali watanzania.
Rais Samia alisema alijaribu kutafuta shahada hiyo lakini muda haukumpa nafasi
Pia, soma=> Chuo kikuu Cha Dar es salaam kimpe Rais Samia Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa
PIA SOMA
- Rais Samia atunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, leo Aprili 18, 2024
- Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi ya Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), leo Desemba 28, 2023
- Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru chamtunuku Rais Samia Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), leo Oktoba 10, 2023