Uchaguzi 2020 Dkt. John Magufuli amerudisha fomu ya maombi ya kugombea Urais Makao Makuu ya CCM

Huku ni sawa na kuanika madhaifu ya mkeo hadharani alafu ukajiona mjanja!!
 
Reactions: BAK
Jamaa utawala wake umekuwa wa propaganda zaidi na kwa kiasi fulani zimemsaidia kumuimalisha

Mtu ambaye si mbinafsi anatambua kazi za wenzake na anatambua kwamba wapo wanaowenza kufanya hata zaidi yake

Mbinafsi anaamini yeye ndo yeye na yeye ndo anastahili vizuri na yeye ndio pekee anaweza kufanya mazuri. Kifupi mbinafsi haamini kama Kuna mwingine anaweza kumzidi

Naomba mnisaidie kuelewa, anaposema yeye si mbinafsi wakati huo huo akasema haamini kama Kuna mwingine anaweza kufanya aliyoyafanya na kukamilisha mipango yake anamaanisha nini?
 
Mtanzania mwenzangu hata ukilialia haitobadilisha tusifuate na kuzilinda imani kuu za CCM zilizoifinyanga nchi hii.

Kamwe hatuwezi kuziacha kisa machozi yako ya mamba.

Yaani tuzifute imani HIZI;

1.Binadamu wote ni sawa.
JPM analisimamia hili kwa kuhakikisha raslimali za taifa zinawanufaisha RAIA WOTE na si wale kupe wachache.

2.Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
JPM analisimamia hili kuhakikisha YALE MAMBO YA "UNANIJUA MM" yamekwisha Zama hz.Yalikuwepo kipindi kile serikali ya mh.membe na WENZAKE.

3.Ujamaa na kujitegemea NDIYO njia sahihi ya kujenga jamii iliyo sawa na huru.
JPM kwake ni KAZI TU Mana HATUNA WAJOMBA wa kuwaomba....
Kujitegemea ni kule ambako MAZWAZWA WALIPOLOCK DOWN sisi tunaendelea kulima na kufanya BIASHARA ili tuendeleze kulipana MISHAHARA.Ili wanafunzi wa vyuo vikuu wapate bumu lao pale HESLB.
Wastaafu wetu waweze kujikimu kwa kulipwa mafao yao ya kila mwezi.

Nawashauri muwe mnakunywa maziwa badala ya kulamba Sana faru John ile hatimiliki ya mh.mwenyekiti.

Think thrice
 
Eti bado hajakamilisha, hajui kuwa hata miaka miwili inaweza isipite akafa.
 
Eti bado hajakamilisha, hajui kuwa hata miaka miwili inaweza isipite akafa.
Kwa kuwa tutakufa ndio tusipange mipango,ndio tusiwe na matumaini,ndio TUSINYOOSHE PASI NGUO ZETU ZA kuvaa kesho KAZINI,NDIO TUSISOGELEANE NA WAKE ZETU ili tuzaane?!!!
 
Mitandaoni ni Sehemu ya kutoa stress tu ukiamini mambo ya Twitter utaharibikiwa peke yako
 
Hata mimi sikuelewa anamaanisha nin kusema hakuwa mbinafsi wakati huo haoni mwingine wa kuongoza taifa hili.
 
Maji,umeme,2025, 100%; SGR 15 Yrs +++ kwa hoja hiyo na viwanda ...hakuna mwingine ni JPM pekee 4 life "atake asitake"
 
Ushahidi? Ama kweli watu ni vupofu Tena vipofu Hadi aibu, we unadhani ni Nani anaweza fanya matukio makubwa Kama haya Kama si huyo unaemtetea? Risasi kwenye eneo la bunge kwani sisi tuko Afghanistan? Haya tuambie mwenye nchi ninani?
Je unaushahidi ili kuthibitisha unachokisema ?
 
Sasa moderator ni kwa sababu ipi mmetoa post yangu page ya kwanza ya wimbo wa Magufuli Kwangaru.. na kuacha post zenye video za Chadema?.. Moderator
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…