Uchaguzi 2020 Dkt. John Magufuli amerudisha fomu ya maombi ya kugombea Urais Makao Makuu ya CCM

Uchaguzi 2020 Dkt. John Magufuli amerudisha fomu ya maombi ya kugombea Urais Makao Makuu ya CCM

Kwa hiyo Baba ukifa nchi yetu nayo imekufa?
Kwa nini uwaze kufa? Hajafa na katiba ya nchi inamruhusu kiomba kipindi kingine kuendeleza mipango yake. Ndio maana tulitengua Katiba ya chama, Mwamba hana ukomo tunaogopa akiongoza mwingine Chadema itakufa, hatukujali kuwa na yeye anaweza kufa😂😂
 
😂😂😂😂😂😂hivi Mwenyekiti wa chama ni nani vile? Hivi aliyemfukuza Membe ccm ni nani vile? Halafu ashindwe kuruhusu wengine wachukue form!? 🤣🤣🤣🤣🤣
Wangeimba "...tuna imani na mtu fulani inhiiiiii..." ndipo wangejua...
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Kwa nini uwaze kufa? Hajafa na katiba ya nchi inamruhusu kiomba kipindi kingine kuendeleza mipango yake. Ndio maana tulitengua Katiba ya chama, Mwamba hana ukomo tunaogopa akiongiza mwingine chama kitakufa, hatukujali kuwa na yeye anaweza kufa[emoji23][emoji23]
Hivi nyie mnaosema iliandaliwa fomu moja mna ushahidi? kuna mtu kaenda kuchukua fomu kanyimwa au kaambiwa zimeisha? Mimi sijasikia.
 
Kwa hiyo na hiyo mitano anayo omba ikiisha tena hajakamilisha mambo yake aombe tena mingine si ndio hivyo?

Magufuli acha kujiona kwamba bila wewe hii nchi si kitu, hii nchi umeikuta na shida na raha zake na utaondoka utaiacha na shida na raha zake vilevile.
Alionywa
 
Nchi nzima hakuna wa kufanya kazi
Yupo, huyu hapa anaweza kabisa kukamilisha kazi hii
tapatalk_1593528776616.jpeg
 
“...hapa tumegusana tu, unaambiwa usimsogelee mtu mpaka mita moja mke wako utaacha kumsogelea au mume wako, mtapataje mtoto bila kusogeleana...ni mambo ya ajabu na ndio nikasema sisi tutasogeleana ”-.Rais Magufuli.

Hata Mimi Mzukulu niliwashangaa mno hawa Wataalam wa Afya na Watu wa ( WHO ) waliposema eti tusiwe tunasogeleana. Ni Wapuuzi mno!
 
CCM moto ni mkali sana.

Hakuna mwenye ubavu wa kuprint fomu zaidi ya 1 kwenye nafasi ya Urais ndani ya CCM...

Hakuna mwenye uwezo na ubavu wa kuchukua fomu No 2...

Na hakuna mwenye nia ya kuwania Urais ukiacha jembe , Rais JPM

Ambaye hajipendi afanye hivyo..

Kelele za Tweeter hazinaga msaada.
Yani unaanika udhaifu wa ccm halafu unajiona mjanja..!? Hahahahaha..
Soma tena ulichoandika Mbwiga.
 
Mtanzania mwenzangu hata ukilialia haitobadilisha tusifuate na kuzilinda imani kuu za CCM zilizoifinyanga nchi hii.

Kamwe hatuwezi kuziacha kisa machozi yako ya mamba.

Yaani tuzifute imani HIZI;

1.Binadamu wote ni sawa.
JPM analisimamia hili kwa kuhakikisha raslimali za taifa zinawanufaisha RAIA WOTE na si wale kupe wachache.

2.Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
JPM analisimamia hili kuhakikisha YALE MAMBO YA "UNANIJUA MM" yamekwisha Zama hz.Yalikuwepo kipindi kile serikali ya mh.membe na WENZAKE.

3.Ujamaa na kujitegemea NDIYO njia sahihi ya kujenga jamii iliyo sawa na huru.
JPM kwake ni KAZI TU Mana HATUNA WAJOMBA wa kuwaomba....
Kujitegemea ni kule ambako MAZWAZWA WALIPOLOCK DOWN sisi tunaendelea kulima na kufanya BIASHARA ili tuendeleze kulipana MISHAHARA.Ili wanafunzi wa vyuo vikuu wapate bumu lao pale HESLB.
Wastaafu wetu waweze kujikimu kwa kulipwa mafao yao ya kila mwezi.

Nawashauri muwe mnakunywa maziwa badala ya kulamba Sana faru John ile hatimiliki ya mh.mwenyekiti.

Think thrice
[/QUOT]
Imba tu pambio zote lkn hayo maswali yanahitaji majibu, awe hai awe mfu lkn majibu lazima yatolewe.

Hata Mungu hamsamehi asiyetubu hata uwe unamtaja jina kila baada ya dakika moja ni kazi bure tu.

Pipa lililojaa asali ukilitia tu hata katone ka mkojo tayari asali yote inakuwa ni NAJISI.
 
Je, unaushahidi ili kuthibitisha unachokisema?
Sina ushahidi, unless hujanielewa. Ninachomaanisha ni kuwa rais ndio kikatiba ana jukumu la kusimamia ulinzi wa raia wote na mali zao.

Na inapotokea raia yeyote hajulikani alipo lazima afuatilie na ashee majibu kwa taifa, je katika swala la hao akina Saanane na Azory, hilo limefanyika??? Kama wewe sio mnafiki nafikiri jibu utakuwa nalo.

Haiwezekani uchaguzi ukiwadia ndio anaanza kuzunguka kwa hao hao ambao wengine wao hawajulikani walipo eti kuwaomba wampe kura, wampeje kura wakati hawezi kuwahakikishia usalama wao....????? This is not only hypocritical but a flagrant criminal unaccountability deserving indictment.
 
Nimeupenda sana huu mwongozo wa mwenyekiti wa CCM Dr Magufuli kwamba watia nia hawana sababu za kuchafuana kwani atakayeteuliwa ni mgombea mmoja tu.

Kuanzia leo majimbo yote ya ubunge yako wazi......naelekea Iringa mjini kutathmini utaratibu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ushahidi? Ama kweli watu ni vupofu Tena vipofu Hadi aibu, we unadhani ni Nani anaweza fanya matukio makubwa Kama haya Kama si huyo unaemtetea? Risasi kwenye eneo la bunge kwani sisi tuko Afghanistan? Haya tuambie mwenye nchi ninani?
Mi swali langu lilikua rahisi tu sikupingi JE UNA USHAHIDI KUTHIBITISHA UNACHOKISEMA?
 
Sina ushahidi, unless hujanielewa. Ninachomaanisha ni kuwa rais ndio kikatiba ana jukumu la kusimamia ulinzi wa raia wote na mali zao.

Na inapotokea raia yeyote hajulikani alipo lazima afuatilie na ashee majibu kwa taifa, je katika swala la hao akina Saanane na Azory, hilo limefanyika??? Kama wewe sio mnafiki nafikiri jibu utakuwa nalo.

Haiwezekani uchaguzi ukiwadia ndio anaanza kuzunguka kwa hao hao ambao wengine wao hawajulikani walipo eti kuwaomba wampe kura, wampeje kura wakati hawezi kuwahakikishia usalama wao....????? This is not only hypocritical but a flagrant criminal unaccountability deserving indictment.
Kama sijakosea watu wengi wanapotea Tanzania wasijulikane wako wapi tunaona hata matangazo kwenye vyombo vya habari kila siku... na haijawahi kutokea rais akahisishwa au kujibu kuhusiana na upotevu huo kwanini hawa ? Je unaushahidi kuthibitisha kwamba Rais anahusika moja kwa moja na kupotea kwa watu
 
Soma andiko langu vizuri ulielewe. Rais ni Accounting Officer kwa kila jambo linalotokea katika nchi, wewe huoni Trump analaumiwa kwa ku-mishandle the Corona pandemic.

Huoni makocha wanafukuzwa pale timu inapofanya vibaya pamoja na kwamba hawaingii uwanjani kucheza.

Tatizo lenu mnamuona rais kama Mungu vile ambaye hawezi kukosea wakati ni binadamu tu kama wengine. Mbona akifanya kile kinachoonekana kuwa kizuri anasifiwa?

Sasa wewe kwa akili yako watu wakipotea au kujeruhiwa na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa unataka tumuulize nani. Jaribuni kuwa rational ktk kufikiri.
 
Kama mpoteaji ameamua kupotea kwa mapenzi yake na kama muumiaji ameamua kutokutoa ushirikiano kwenye upelelezi wake nani alaumiwe kwa hilo?
 
Back
Top Bottom