Dkt. Kahyoza: Magufuli alifanya makosa makubwa kuhamishia Serikali Dodoma, gharama zimekuwa mara mbili

Maana yake ni kuwa serikali bado haijamaliza kuhamia dodoma mazima kabisa. Cha kufuatia wajenge dodoma international airport, ndege za kimataifa ziwe na uwezo wa kutua dar. Uwanja ukikamilika ofisi zote za umma ziwe zimeshahamia Dar
 
Nipe sababu moja tu ya maana ya kulazimisha kuhamisha makao makuu ya nchi baada ya kushindwa kutekelezwa kwa miaka zaidi ya 40 yaani umuhimu wake mkubwa hasa ni nini?
Sayansi na Technolojia vimekua sana, hakukuwa na umuhimu wowote ule wa kutumia fedha yote ile kuhamishia makao makuu Dodoma. Wangeboresha mifumo ya TEHAMA na kuwekeza zaidi kwenye software infrastructure. Aliyefanya maamuzi haya hakuwa mzalendo kwa nchi yake hata kidogo.
 
HUYO MSOMI WA PHD NI bwege kabisa. Empty empty headed. Tatizo hapo ni MISCONDUCT ya baadhi ya watumishi wa umma. SIYO maamuzi na utekelezaji wa kuhamia Dodoma. Uamuzi na utekelezaji wa kuhamia DODOMA bado ni sahihi kabisa, tukiachia mbali changamoto za hapa na pale, ambavyo ni vitu vya kawaida.
Note: Huyo msomi wa kwenye makaratasi ANAJIPENDEKEZA kwa wateuzi, anashindwa kujenga hoja kama darasa la pili. ELIMU YA TZ NI HATARI SANA, COPY AND PASTE. NO OBJECTIVE CRITICAL ANALYSIS.
 
Marehemu anawatesa sana nyoko hawa! Sasa kama hayo yanafanyika anayesimamia serikali ameshindwa nini kutoa maagizo? Tukubali tukatae, JPM hana spare! Hizi Rais zingine ni takatata tu!
 
Dar wanakuja kufanya nini? Wanatakiwa wakae Dodoma wafanye kazi angekuwepo alieanzisha angesimamia hili
Point ipo hapo tu mkuu,hao viongozi nao ni watumishi tu,mbon madaktari,maprofesa,walimu ,manesi na watumishi wengine wanapangiwa kituo cha kazi na wanakaa kwenye mikoa au miji wanayofanyia kazi iweje wao,
Wana dharau sana na kutaka kuhalalisha ulaji wa pesa kwa sababu zisizo za msingi hawana huruma na maisha ya watanzania
 
Wanaenda Dsm kufanya nini? Ni nini ambacho hakipo Dodoma?
 
Dokta tutusa ilo

Linaogopa kuwaambia viongozi watulie dodoma linaishia kulaumu magufuli
Ni kawaida ya watu waoga waoga kulaumu wenzao,watu makini kwenye maisha hawana muda wa kulaumu watu,
Alafu anakuja kusema leo kwamba kakosea kwanini asingeenda kumshauri kipindi yupo hai ?
 
Ni kweli, ila ifike kipindi huyo mzee aachwe apumzike huko aliko Kama kuna kupumzika.
Nafikir ame highlight makosa ya kimfumo, wabunge hawa hawa ndio wanasifia, halaf hao hao ndio wanalalamika. Yaani wanakwenda na upepo. Na si hilo tu kuna mengi
 
Mbona anaukwepa mbuyu. Hapo kosa la Magufuli ni lipi ! Serikali imeshamia Dodoma kinachowafanya waende Dar mara kwa mara ni kipi ?
 
Pumbavu kabisa
Kwa style hii, nimeghairi kusoma PHd kama hawa ndio phd holders wenyewe. Hovyo kabisa. Yan hapo Baba Levo ndio utafikiri msomi wa phd kuliko hiyo jamaa
Acha hizo Sasa unahamishia makao makuu Dodoma Halafu kutwa unashinda saluni kujipodoa Dar es salaam badala ya kukaa ofisini Dodoma unaona ni sawa Hilo?
 
Ni kawaida ya watu waoga waoga kulaumu wenzao,watu makini kwenye maisha hawana muda wa kulaumu watu,
Alafu anakuja kusema leo kwamba kakosea kwanini asingeenda kumshauri kipindi yupo hai ?
Alikua anashsurika by then?
 
Kwani hao viongozi lazima waje dar?

Kifupi hao viongozi ni wafujaji, wanafanya matumizi mabovu mnoo
 
Mbona anaukwepa mbuyu. Hapo kosa la Magufuli ni lipi ! Serikali imeshamia Dodoma kinachowafanya waende Dar mara kwa mara ni kipi ?
Actually kwa kiasi kikubwa serikali Iko settled dodoma

Safari to dar and other regions ni za kawaida

Dar haikwepeki… ni commercial capital,

Fikiria if hadi leo dar ingeku capital… mji ulishazidiwa

Huyo msomi hawazi kwa upana wa jambo… anaangalia only one factor
 
Acha hizo Sasa unahamishia makao makuu Dodoma Halafu kutwa unashinda saluni kujipodoa Dar es salaam badala ya kukaa ofisini Dodoma unaona ni sawa Hilo?
Nani kutwa anashinda dar?

Umeangalia economic impact ya serikali kuwa dar na congestions tulizonazo?
 
Ni kawaida ya watu waoga waoga kulaumu wenzao,watu makini kwenye maisha hawana muda wa kulaumu watu,
Alafu anakuja kusema leo kwamba kakosea kwanini asingeenda kumshauri kipindi yupo hai ?
alikua mwanafunzi wangu kwa kipindi kifupi pale KIU, hakua mwanafunzi wa maana sana, alikua team Lowasa mbishi sana, daima alimchukia sana magufuli bila sababu...

nilishanga baadae nilipotokomea kwa siasa, nilimkuta ni mwalimu anafundisha, nikasema dah iyo product yake itakua balaa 🐒
 
Watanzania tunakwama hapa, UNAFIKI unatukwamisha(hii si kwa msomi au kapuku).
Huyu msomi hoja yake kama nimemuelewa ni kwamba wakubwa wakubali kwamba wamehamia dodoma,shughuli zao zote zifanyike dodoma.
wasitumie gharama za serikali kuja Dar kwenye mishe zao,wanaiongezea gharama za bure serikali.
Lakini anaona kunyosha maelezo,labda itamgharimu endapo naye anavizia nafasi za uteuzi.
 
Jiwe alikurupuka na misifa yake!
 
Binafsi naona kama tunakosoa uamzi wa kuhamia dodoma,tuanze na mwalimu
Nyerere aliyeasisi wazo hili,nakumbuka tumeimba sana nyimbo za kuhamia dodoma na faida zake
tangu tupo shule ya msingi,lakini aliyethubutu kufanya hivyo,hadi nchi ilipompata rais mwenye uthubutu
JPM.
Ukitaka kujua jamaa alikuwa mwamba,angalia miradi aliyoianzisha kama haitatamalaki kwenye kuomba kura uchaguzi ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…