Dkt. Kahyoza: Magufuli alifanya makosa makubwa kuhamishia Serikali Dodoma, gharama zimekuwa mara mbili

Dkt. Kahyoza: Magufuli alifanya makosa makubwa kuhamishia Serikali Dodoma, gharama zimekuwa mara mbili

Sayansi na Technolojia vimekua sana, hakukuwa na umuhimu wowote ule wa kutumia fedha yote ile kuhamishia makao makuu Dodoma. Wangeboresha mifumo ya TEHAMA na kuwekeza zaidi kwenye software infrastructure. Aliyefanya maamuzi haya hakuwa mzalendo kwa nchi yake hata kidogo.
🙋‍♂️📝✍️👍👌👏👊🤝🙏💐🛡️
 
alikua mwanafunzi wangu kwa kipindi kifupi pale KIU, hakua mwanafunzi wa maana sana, alikua team Lowasa mbishi sana, daima alimchukia sana magufuli bila sababu...

nilishanga baadae nilipotokomea kwa siasa, nilimkuta ni mwalimu anafundisha, nikasema dah iyo product yake itakua balaa 🐒
Mkuu mtu asipompenda Mwendazake hapaswi kufundisha???

Kwamba kwa sababu alikuwa mfuasi wa Lowasa ndio maana hakuwa wa maana???

Common Mkuu, unautweza ukufunzi wako!!! Naona wewe ndiye mwenye shida ya kufikiri sio Dr.
 
Aisee hao viongozi kwanini waende Dar ?!!!!

Hivi anadhani Dodoma ilichaguliwa sababu ya jina lake au walirusha Sanda Kalawe au ni sababu ni katikati ya nchi hivyo ni rahisi kwa watu wote kwenda pale kuliko Dar ?
 
Mkuu kumbuka serikali haingalii miaka mitano hata kumi mbele ila sisi mtu mmoja mmoja ndo tunaangalia karibu karibu,serikali inatakiwa iangalie miaka hata hamsini na zaidi mbele ,sasa kuhamia Dodoma serikali imefanya hivyo imeangalia mbali sana idadi ya watu inakua sana ,mpaka sasa ukiangalia dar ina watu wengi.Na pia kama serikali baadhi ya majengo ilikuwa inapanga sasa itaendelea kupanga mpaka lini kama serikali? Kwa hiyo kuhamia dodoma ni muda muafaka na sababu sahihi zipo.
Tutajie ,Kwa mfano ni Wizara.ngapi zilikuwa zinapanga ?
 
Aisee hao viongozi kwanini waende Dar ?!!!!

Hivi anadhani Dodoma ilichaguliwa sababu ya jina lake au walirusha Sanda Kalawe au ni sababu ni katikati ya nchi hivyo ni rahisi kwa watu wote kwenda pale kuliko Dar ?
Kwa miaka hiyo ya 1970 inawezekana wazo hilo lilikuwa sahihi kabisa ukizingatia location ya Dodoma, uduni wa miundombinu na uduni wa teknolojia.
 
Magufuli aliona mbali sana, siku mkija kutafakari kwa kina mtaelewa ni kwanini Dodoma, maana wengine fikra zenu ni majengo tu na miundombinu tu

Lakini mkizingatia issue tu kama usalama basi mtajua ya kuwa Dodoma ni mara elfu
Mkuu Dunia ya sasa hivi umbali sio ishu, uwekezaji wa teknolojia ya kisasa na kiu salama na ulinzi inatosha.

Nchi nyingi duniani miji mikuu yao ipo ufukweni na zina usalama hiyo sio sababu hata kidogo.
 
Aisee hao viongozi kwanini waende Dar ?!!!!

Hivi anadhani Dodoma ilichaguliwa sababu ya jina lake au walirusha Sanda Kalawe au ni sababu ni katikati ya nchi hivyo ni rahisi kwa watu wote kwenda pale kuliko Dar ?
Anajua hasara tuliyokuwa tunapata kama taifa kwa misururu ya foleni inayosababishwa na misafara hapa Dar?

Anajua gharama walizotumia wananchi wa mikoa ya mbali kuja Dar kufuata huduma ila kwa sasa wanapata huduma karibu?
Kwa hizo hasàra zinazidi ,hasàra za kuhamia Dodoma,na bado Kuna ofisi zinafanya.kazi za Dar ikiwemo naniliii
 
Wakati wote Unapofanya Uamuzi wa kudumu ni lazima uzingatie sababu za kudumu.

Je, Nini hasa sababu za awali awali kabisa zilizosababisha kuwaza kuhamishia makao makuu ya nchi mjini Dodoma badala ya Dsm??
Je, sababu hizo bado zipo na bado zitaendelea kudumu miaka yote au hazipo??
Ukiwa na fikra nzuri huwezi kuyasema ulio ya sema, huwezi kukaa kusubiri sababu kwenye kitu unachojua ni mpango wa lazima unao paswa kutekelezwa. Basi namimi nikuulize, kwanini ilibidi kusubiri sababu ili kuhanisha mako makuu Dodoma? Kwani bunge kua dodoma na office za mawaziri kua dar uliliona ilo ni sawa? Swala la kutokua na mji wa kiserikali unaliona ni sawa?
 
Binafsi huwa siwaelewi wanaomponda JPM ambae ndiye rais pekee aliyeonyesha uthubutu mkubwa sana katika kuonesha nchi yetu inabidi iendaje .
Hivi asingetumia nguvu,tungeendelea na mwendo uleule wa kuita Dodoma makao makuu ya nchi ingekuwa na hali gani leo?tatizo mnafikiriaga njia nyepesi halafu hakuna linalotimia.Magufuli kwa hili na mengineyo bado ni shujaa...
 
Kwa miaka hiyo ya 1970 inawezekana wazo hilo lilikuwa sahihi kabisa ukizingatia location ya Dodoma, uduni wa miundombinu na uduni wa teknolojia.
Kwahio sasa hivi teknolojia imefanya Dar iwe karibu kuliko Dodoma ? Unamuongelea Mtanzania gani huyo na bei zipi za Miuondo Mbinu; Kwahio sababu hao so called viongozi hawawezi kutulia hapo Dodoma na sisi ndio tuwafuate Dar ?
 
Mkuu Dunia ya sasa hivi umbali sio ishu, uwekezaji wa teknolojia ya kisasa na kiu salama na ulinzi inatosha.

Nchi nyingi duniani miji mikuu yao ipo ufukweni na zina usalama hiyo sio sababu hata kidogo.
Bas elewa sababu kutokana na sisi nasio wao, kuhanishia serikali dodoma lilikua ni pendekezo lenye tija kwa nchi, kwanza dodoma bado iko empt kuliko dar kwaiyo ilikua ni rahisi kuijenga na kupa hadhi ya kiserikali mapema kabla haijaharibiwa miundo mbinu yake.
Mkapa aliwahi kusema kinachoikwamisha tanzania ni kila hawamu kua na mamuzi na mipango yake, nyerere aliweka map yote mezani swala lilikua ni kutekeleza kwa hawamu bila kurudi nyuma na Tanzania ingekua mbali sana.
 
Mkuu mtu asipompenda Mwendazake hapaswi kufundisha???

Kwamba kwa sababu alikuwa mfuasi wa Lowasa ndio maana hakuwa wa maana???

Common Mkuu, unautweza ukufunzi wako!!! Naona wewe ndiye mwenye shida ya kufikiri sio Dr.
alichukia kufundishwa bila kumtaja hayati lowasa au kuzungumzia siasa kwenye masuala au moduli zisozo husu siasa za majukwaani :pedroP:
 
Binafsi huwa siwaelewi wanaomponda JPM ambae ndiye rais pekee aliyeonyesha uthubutu mkubwa sana katika kuonesha nchi yetu inabidi iendaje .
Unaweza kufanya maamzi magumu lon ya siwe sahihi
 
Mbona yeye mwenyewe alishahamia chato, [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Chato alienda sababu za usalama wake tu kwa maana covid wakati imenea sana ,lkn muda mwingi angalau alikuwa yupo dom hata makamu wake muda mwingi alikuwa Dodoma.
 
Mtaalamu wa masuala ya Uchumi, Dr. Bravious Kahyoza amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwa ni kosa kubwa kwasababu umeongeza gharama zaidi za uendeshaji ikiwemo kutumia vibaya fedha za Walipa Kodi.

Ametolea mfano Safari za Viongozi na Watumishi ambao mara kwa mara wanaenda Dar au Dodoma kwa Ndege na wakati huo Magari yanasafiri kuwafuata Airport na kuwapeleka kwenye shughuli zao na baadaye wanarejea kwa Ndege tena huku magari yakiwafuata kwa njia ya Barabara.
View attachment 3017571
Pia Soma: Ilikuwa ni jambo jema Serikali kuhamia Dodoma maana Kivukoni na Posta ni Bandarini, Ashukuriwe Shujaa Magufuli!
Mbona hamsemi gharama za safari za nje ya nchi za viongozi ila mnaona ya magufuli kuhamishia makao dodoma
 
Mtaalamu wa masuala ya Uchumi, Dr. Bravious Kahyoza amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwa ni kosa kubwa kwasababu umeongeza gharama zaidi za uendeshaji ikiwemo kutumia vibaya fedha za Walipa Kodi.

Ametolea mfano Safari za Viongozi na Watumishi ambao mara kwa mara wanaenda Dar au Dodoma kwa Ndege na wakati huo Magari yanasafiri kuwafuata Airport na kuwapeleka kwenye shughuli zao na baadaye wanarejea kwa Ndege tena huku magari yakiwafuata kwa njia ya Barabara.
View attachment 3017571
Pia Soma: Ilikuwa ni jambo jema Serikali kuhamia Dodoma maana Kivukoni na Posta ni Bandarini, Ashukuriwe Shujaa Magufuli!
Ifike muda hawa mawakala wa mafisadi wa muache Jpm apumzike tumechoka na kauli zao za hovyo ina maana kila alilolifanya magufuli ni baya hana mazuri
 
Back
Top Bottom