Dkt. Kitima: Baba Mtakatifu ametutaka tufuate ushauri wa Wanasayansi kuhusu ugunduzi wa chanjo

Dkt. Kitima: Baba Mtakatifu ametutaka tufuate ushauri wa Wanasayansi kuhusu ugunduzi wa chanjo

Ngoja nichomeke kaswali! Hivi wanasayansi wanaweza kufanya utafiti ili wajue kama kweli Yesu alikufa na kufufuka?
 
Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Dkt. Charles Kitima akiongea na BBC amesema Baba Mtakatifu ambaye ndio mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francisco amewataka kupokea ushauri wa wanasayansi kuhusiana na ugunduzi wa chanjo za Corona.

Dkt. Kitima amesema wao kama Kanisa watachukua tahadhari kama Mataifa yaliyoendelea yafanyavyo ikiwemo social distancing, kuvaa barakoa na kunawa mikono.

Fr. Kitima amesema kwa sasa wazee wengi wameacha kuhudhuria ibadani wakihofu maambukizi ya Corona.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia

Maendeleo hayana vyama!
Papa Mtakatifu amesahau kuwa hapa bongo kuna mkuu wa malaika wote
 
Bahati, hawataweza kwani myself "individually" ressurection is not a historical event.
 
Ni miongoni mwa wanasayansi ambao papa ametutaka tusikilize ushauri wao.

Hapo Chadema sidhani kama mna mwanasayansi hata mmoja maana mzee Sumaye na Dr Mollel walisharejea CCM!
Magufuli ni mwanasayansi ya afya? Au kwa vile anaitwa Dr ukadhani ni Doctor by professional.
 
Nani ampe Uasikofu! Hawezi pewa! Ana dharau na kiburi sana,hua ana wadharau hadi maboss wake! In short humujui Kitima wewe! Enzi akiwa VC Saut,tumeonja joto lake!
Mzee mangungu pamoja na kiburi ila jamaa ana msimamo ndio sababu anawafokea hata maaskofu wanaotaka kulamba miguu ya viongozi wa sasa. Take my word huyu jamaa atapata uaskofu ndani ya miaka 5 ijayo.
 
Mpuuzi kweli wewe... hakuna mungu kuna Mungu.
Hakuna mungu wala Mungu mkuu, ishi maisha yako vile utakavyo! Ukifa ndiyo mwisho wako, utarudisha hizo protons, neutrons and electrons kwa mmiliki wake, ambaye ni UNIVERSE!
 
Wa Catholic wana viongozi wao na wanaheshimu mamlaka zao sio wenzangu na mimi mashekh ubwabwa kimya utasema wamehama nchi. kurudi kwenye topic yeye katoa angalizo kwa waumini wao na hao ndio wataheshimu viongozi wao na sote tunajuwa kuna sababu ya Catholic kuwa na nguvu, sababu wana chain of command na wote wanatii. Mimi ni muislamu na nasema haya kwa uchungu. ndio maana project yao yoyote itafanikiwa tu kwa sababu NIDHAMU NA UTIIFU
 
Ukifuata wana sayansi kawaida, process ya kuvumbua dawa au chanjo zina chukua muda gani ?
Nafikiri Father Dr. Kitima anamaanisha ya kwamba Baba Mtakatifu anawashauri wasizitumie chanjo za Corona kwasababu hazijakidhi viwango vya Kisayansi kwasababu zimechukua muda mfupi sana kuanza kutumika. Kwahiyo anawatahadharisha waumini wake kama Rais Magufuli alivyowatadharisha raia wake dhidi ya hizi chanjo!
 
Kanisa linapokuwa nyuma ya mtu tustawishe tu misitu ili kuni ziwe nyingi kule Jehanamu
 
Nafikiri Father Dr. Kitima anamaanisha ya kwamba Baba Mtakatifu anawashauri wasizitumie chanjo za Corona kwasababu hazijakidhi viwango vya Kisayansi kwasababu zimechukua muda mfupi sana kuanza kutumika. Kwahiyo anawatahadharisha waumini wake kama Rais Magufuli alivyowatadharisha raia wake dhidi ya hizi chanjo!
Pope Francis ameshauri watu wafuate ushauri wa kisayansi na kwamba waumini wanapaswa kutumia chanjo kujikinga pale inapotolewa na mamlaka husika.
 
Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Dkt. Charles Kitima akiongea na BBC amesema Baba Mtakatifu ambaye ndio mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francisco amewataka kupokea ushauri wa wanasayansi kuhusiana na ugunduzi wa chanjo za Corona.

Dkt. Kitima amesema wao kama Kanisa watachukua tahadhari kama Mataifa yaliyoendelea yafanyavyo ikiwemo social distancing, kuvaa barakoa na kunawa mikono.

Fr. Kitima amesema kwa sasa wazee wengi wameacha kuhudhuria ibadani wakihofu maambukizi ya Corona.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia

Maendeleo hayana vyama!
Kibaraka hiki
 
Reasonable time ni kabla ugonjwa haujaleta vifo au madhara makubwa
Ok let me make it a little bit simple , what is the reasonable time to complete hiyo circle, and confirm it to be ready to be used by human beings
 
Back
Top Bottom