Tetesi: Dkt. Likwelile kupandishwa Kisutu, yupo mikononi mwa TAKUKURU

Tetesi: Dkt. Likwelile kupandishwa Kisutu, yupo mikononi mwa TAKUKURU

Hapo laweza kuwepo gundu? Au unasemaje mzee wa udaku Professor Lizaboni? Maana kuna ile ndoa tulichanga milioni 90 ikaishia kupigwa drip hospitalini. Halafu kuna ule wakati bwana mkubwa mzee wa totoz aliposema anataka kuonja asali yeye akaachia jumla bila kinga tukapata uzao.
Lakini bwana mkubwa akashtuka na kusema sitaki Wanawake na Maendeleo ya bongo flava nataka Wanawake na Maendeleo ya kitaasisi tuu.
Sasa Leo tena mtu unajitumbukiza shimo la fedha (hazina) linageuka shimo la choo?
GUNDU!
Fumbo mfumbie.....Dah! Watu mnajua kufumba nyie! Imenichukua saa nzima kustadi hadi kufumbua! Paliponitatiza na kutaka kunishikisha ziro ni pale....Hataki wanawake na maendeleo ya bongo fleva bali wama taasisi!
Imenisumbua, imenipotezea muda kuinyaka hiyo mkulu!
 
Aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha Dr. Likwelile muda wowote kuanzia sasa atapandishwa mahakamani Kisutu kujibu mashitaka ya ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, na kusaidia ukwapuaji wa fedha katika dili mbalimbali.

Taarifa nyeti zinasema tayari uchunguzi ushakamilika na muda si mrefu atapandishwa Kisutu na TAKUKURU. Kumbuka Dr. Likwelile alitenguliwa katika nafasi yake na Rais mzalendo Dr. John Pombe Magufuli..

Mytake: Kama aliiba na apandishwe tu, manake hakuna namna sasa!
Maajabu hayeshi nchi hii...wajumbe msijeshangaa mawakili watakaomtetea mtuhumiwa tunaemuongelea ikitokea bandiko hili likawa kweli...au mwaka wa uchaguzi akawa upande huu wa siasa....
 
Dah kwa kweli Watu watayakataa haya madaraka sasa hivi..
Utakuta kosa la mwingine unahukumiwa wewe kisa kiongozi ndio ulokuwa hapo..
Mambo mengine yangekuwa yanazungumzwa kimya kimya yanamalizwa sio kudhalilishana.
Hebu fikiri tuuu wewe unayeshabikia kama ndio wewe...usichekelee kisa ni mwenzio..sio wote wenyekupelekwa mahakamani katika hawa viongozi ni kuwa wamekula wao pesa, ila utakuta ni mfanyakazi wa chini lakini unayewajibishwa ni kiongozi .........
Hii sasa, kila kukicha issue hadi kero
Unauhakika na unachokitetea?
Fedha ziliwe, boss hajui na hatua hakuna! Uboss wake ni wanini? Jitambue bandugu.
 
Majizi yote yakamatwe Richmond,IPTL,LUGUMI NA WOTE.Sio kuonea dagaa tu huku mapapa yanatamba na yanaendelea kuiba IPTL+ESCROW
 
So Far Vibaka wote ambao washatumbuliwa ni kutoka Chama chetu cha CCMijizi
 
Kama ni kweli ni vita kati ya mkulu na shemeji.
Sii mnajua chombo cha mtuhumiwa ni Mbunge wa vitu maalumu kutoka mkoa ule wa dhahabu na ambao ile wilaya pekee nchini yenye traffic light ipo?
Ambacho bado kilikuwa kinasomeka bado kama Kifanyakazai pale TWIN tower Down Town DSM
 
tulisema sana mahakama ya mafisadi itawamaliza ccm... sasa ngoja ianze sisi wazalendo tutoe USHIRIKIANO wa kuwafichua mafisadi kwa nguvu ili hadi ikifika 2020 kazi iwe rahisi
 
Kwahiyo kipindi cha nyuma walikuwa hawapokei amri/maelekezo kutoka "juu"? Acha mchezo!
naona huelewi maana ya taratibu za fedha,kasome public finance regulations zinaeleza taratibu za fedha ya serikali inavyotakiwa kukusanywa na kutoka/kutumika..siku hizi ni amri ya mtu mmoja tu bila kujali accounting standards
 
Usiishi ktk fikra za kudhani ishi ktk ukweli! Unakoelekea hata wale watoto wako ambao sura zao ni tofauti nawe utaanza sasa hivi kudhani sio wako na ukiishi 'kwa kudhani' watakuwa sio wako kweli! Kingine punguza wivu wako wa kike!
Povu la nini au nimegusa mfupa?? Nilikuwa "nafikiri" kuhusu Likwelile na kumbe nilikuwa sambamba na takukuru, tatizo lako nini?? Mauza uza ya tanesco kabla ya JPM kuwa rais, mkurugenzi wa tanesco hawezi kuyakwepa, time will tell!!
 
Back
Top Bottom