Kumekucha salama,
Leo tarehe 06.08.2020 mgombea nafasi ya kazi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa Chama cha Mapinduzi, atachukua fomu kwenye ofisi ya NEC makao makuu ya Dodoma.
Baada ya kuchukua fomu ataongea na wananchi pia wanachama wa CCM kwenye ukumbi wa white house jijini Dodoma.
Watanzania wanatakiwa wanaombwa kumsikiliza.
UPDATES:
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mh. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto)katika Ofisi za Tume, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles na Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk.
View attachment 1528677
Mgombea wa Urais, Dkt. Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan wakionesha begi lenye fomu ya Urais
Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM:
Ushindi wa mwaka huu ni wa kishindo kikubwa. Tutashinda nafasi za kutosha. Tutashinda nafasi za kutosha za udiwani. Tutaongoza halmashauri zote nchi nzima. Tutakuwa na wingi wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Rais Magufuli:
Napenda nikiri. Sikutegemea ningekuta watu wengi hivi hapa, kwasababu mimi nikawaida yangu kuheshimu sharia.
Kitabu cha mwaka huu cha ilani ni kikubwa kuliko miaka iliyopita, kina mambo mengi sana. Siwezi nikayasema hapa yote. Tutayasema siku ya uzinduzi wa kampeni.
Na ninawaomba viongozi viongozi wenzangu, kuzindua kampeni hizi ikiwezekana kuzianzia hapa Dodoma, kwakuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi.
Nilipomaliza kuchukuwa fomu pale kwenye jengo la NEC pamoja na Mama Samia, Mama mchapa kazi, jabali la kwelikweli, nilipokuwa nateremka kwenye gari nikiwa pale juu nikakiangalia Chuo Kikuu cha Dodoma, nikaangalia chini nyumba na maghorofa yalivyojengwa katika eneo hili la Dodoma, nikajaribu kutupa macho yangu mpaka Chuo cha Mipango kule. Nikaangalia kila mahali. Hujagusa Chuo Kikuu cha St. John, unaenda pale CBE na maeneo mengine. Hombolo sijakisahau jirani yetu kule.
Lakini nilivyoiona Dodoma ilivyo, nilijiuliza nikiwa njiani nikasema: “Dodoma kweli imekuwa hivi? Mbona sikuikuta hivi nilivyoteuliwa kuwa Rais” Nikafurahi kuwa ndoto za Baba wa Taifa zimekamilika kwamba Dodoma ni Makao Makuu ya nchi yetu.
Tulipochaguliwa kuongoza taifa hili kupeperusha bendera ya CCM, tumefanya mengi…kila mahali katika nchi hii, pamefanyika kitu.
Kwa kumbukumbu zangu tu, shule zaidi ya 908 za msingi zimejengwa katika nchi hii. Hizo ni za msingi. Za sekondari ni 228, vituo vya afya karibu 500. Mambo mengi.