Hahah 2015 alisema hivyo hivyo tena,sijui amesahau?"Tumechoka Taifa hili unalima pamba unaisafirisha kama malighafi, halafu wakishatengeneza nguo wanazivaa wanakuletea mitumba wakati pamba ni yako. Sisi tunataka tukilima pamba tunaichakata hapa zile nguo tunawapelekea ikiwezekana tunazivaa kwanza." -Rais
@MagufuliJP
Hii kauli kaiongea tangia mwaka 2016!"Tumechoka Taifa hili unalima pamba unaisafirisha kama malighafi, halafu wakishatengeneza nguo wanazivaa wanakuletea mitumba wakati pamba ni yako. Sisi tunataka tukilima pamba tunaichakata hapa zile nguo tunawapelekea ikiwezekana tunazivaa kwanza." -Rais
@MagufuliJP
Alituambia hivyo tena 2015,sasa sababu ni miaka 5 imepita nadhani sasa tutakua tumefikia level za South Africa mkuu.Ashatuambia anataka Tanzania iwe kama ulaya
Ova
Duh!Ajira?
Yeye anajua mambo ya ujenzi tu.
Yeye ajira hua anaona vijana waliosoma wakiwa vibarua/saidia fundi huko kwny ujenzi wa shule,zahanati,barabara inatosha kabisa.
Ajira ni janga la dunia kichwa umefugia nywele tuMiaka 5 hii ameshindwa kutengeneza hizo ajira,kutoa ajira zilizo rasmi haijawahi kua kipaumbele chake na wala haitakua na kwny awamu yake vibarua/saidia fundi imekua ndio ajira rasmi sasa kwa maono yake yeye.
Mwambie wanyonge wanamshukuru sana.
Hana mda na vijembe, vijembe tunamuachia Lisu maana kila akilala na kuamka anamuona magufuli sasa anabaki kuweweseka.
Hawezi taja sentesi bila maguguri, na bado ataiimba saana.
Viwanda hajasema ni vingapi vimejengwa? Atasema siku ya uzinduzi wa kampeni.Kumekucha salama,
Leo tarehe 06.08.2020 mgombea nafasi ya kazi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa Chama cha Mapinduzi, atachukua fomu kwenye ofisi ya NEC makao makuu ya Dodoma.
Baada ya kuchukua fomu ataongea na wananchi pia wanachama wa CCM kwenye ukumbi wa white house jijini Dodoma.
Watanzania wanatakiwa wanaombwa kumsikiliza.
UPDATES:
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mh. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto)katika Ofisi za Tume, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles na Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk.
View attachment 1528677
Mgombea wa Urais, Dkt. Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan wakionesha begi lenye fomu ya Urais
Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM:
Ushindi wa mwaka huu ni wa kishindo kikubwa. Tutashinda nafasi za kutosha. Tutashinda nafasi za kutosha za udiwani. Tutaongoza halmashauri zote nchi nzima. Tutakuwa na wingi wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Rais Magufuli:
Napenda nikiri. Sikutegemea ningekuta watu wengi hivi hapa, kwasababu mimi nikawaida yangu kuheshimu sharia.
Kitabu cha mwaka huu cha ilani ni kikubwa kuliko miaka iliyopita, kina mambo mengi sana. Siwezi nikayasema hapa yote. Tutayasema siku ya uzinduzi wa kampeni.
Na ninawaomba viongozi viongozi wenzangu, kuzindua kampeni hizi ikiwezekana kuzianzia hapa Dodoma, kwakuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi.
Nilipomaliza kuchukuwa fomu pale kwenye jengo la NEC pamoja na Mama Samia, Mama mchapa kazi, jabali la kwelikweli, nilipokuwa nateremka kwenye gari nikiwa pale juu nikakiangalia Chuo Kikuu cha Dodoma, nikaangalia chini nyumba na maghorofa yalivyojengwa katika eneo hili la Dodoma, nikajaribu kutupa macho yangu mpaka Chuo cha Mipango kule. Nikaangalia kila mahali. Hujagusa Chuo Kikuu cha St. John, unaenda pale CBE na maeneo mengine. Hombolo sijakisahau jirani yetu kule.
Lakini nilivyoiona Dodoma ilivyo, nilijiuliza nikiwa njiani nikasema: “Dodoma kweli imekuwa hivi? Mbona sikuikuta hivi nilivyoteuliwa kuwa Rais” Nikafurahi kuwa ndoto za Baba wa Taifa zimekamilika kwamba Dodoma ni Makao Makuu ya nchi yetu.
Tulipochaguliwa kuongoza taifa hili kupeperusha bendera ya CCM, tumefanya mengi…kila mahali katika nchi hii, pamefanyika kitu.
Kwa kumbukumbu zangu tu, shule zaidi ya 908 za msingi zimejengwa katika nchi hii. Hizo ni za msingi. Za sekondari ni 228, vituo vya afya karibu 500. Mambo mengi.
Ajira ni janga la dunia kichwa umefugia nywele tu
Hadi UDOM ameijenga yeye aisee.Rais Magufuli kajenga mpaka Saint John's yani ukiwa mshangiliaji wa Magufuli jiandae kumeza mpaka mawe!
Mrima = MlimaCCM wanalazimisha maji kupanda mrima, Mimi sitowapigia kura mpaka waoneshe hela za tetemeko hapa Bukoba mjini , watu bado wanalala nje kwenye matrubai ,wao hela wanakula.
Ni kweli, ni moja ya njia ya kuondoa hofu na kuvuna kura kutoka kwa wapiga kura (wale wasio wanachama wa vyama vya siasa) na ambao hawataki kuwa na Rais wa maisha.Sidhani kama anaweza kuwa na guts za kuongea hivyo kama mwenyekiti wake hajazungumz naye, maana watu wanaongea kile kinachomfurahisha mwenyekiti
Kaiongea leo tena as if ndo anataka kuchukua nchi kutoka kwa JKHii kauli kaiongea tangia mwaka 2016!
Kaiongea leo tena as if ndo anataka kuchukua nchi kutoka kwa JKHahah 2015 alisema hivyo hivyo tena,sijui amesahau?
Ulitaka aseme nimewagawia kila shilingi laki mbili mbili?'Nilipomaliza kuchukuwa fomu pale kwenye jengo la NEC pamoja na Mama Samia, Mama mchapa kazi, jabali la kwelikweli, nilipokuwa nateremka kwenye gari nikiwa pale juu nikakiangalia Chuo Kikuu cha Dodoma, nikaangalia chini nyumba na maghorofa yalivyojengwa katika eneo hili la Dodoma, nikajaribu kutupa macho yangu mpaka Chuo cha Mipango kule. Nikaangalia kila mahali. Hujagusa Chuo Kikuu cha St. John, unaenda pale CBE na maeneo mengine. Hombolo sijakisahau jirani yetu kule.'
'Kwa kumbukumbu zangu tu, shule zaidi ya 908 za msingi zimejengwa katika nchi hii. Hizo ni za msingi. Za sekondari ni 228, vituo vya afya karibu 500. Mambo mengi.'
Angalia hapo juu mkuu,Masaa yeye 24 hua anawaza ujenzi tu mambo mengine hua anaona hayamhusu kabisaa.
Kazi ipo.