Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli achukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania Ofisi za NEC

mrafi wa madaraka hana jipya zaidi ya vitisho!!

Yeye na chama chake wanadhani wana hati milki ya Tanzania na Watanzania. Sitaki nataka tu huyo,njaa ya wana CCM mpya ni hatari.Huwa hawashibi,fikiria 10% za barabara,madaraja,vivuko(eg MV Bagamiyo),stigler's,sgr na bado ataanzisha miradi mingine ya kimkakati kabla hata hajakamiliaha iliyopo.Miaka mitano anayotuaminisha anaomba haitomtosha.

Watanzania, kutenda kosa siyo kosa Bali kosa ni kurudia kosa.Tuzinduke,kama aliona kazi ya Urais ni ngumu,mbona yeye ndiyo namba moja katikà kuchukua fomu?
 
Nimeiangalia hotuba ya mhe rais nimeona tofauti kubwa sana na wagombea wengine. Kila neno lilikua ni kuwasadia watanzania. Sio tu kuingia ikulu badi kuwasadia watanzania na changamoto zinazo wazunguka. Hongera sana mhe rais 2020-2025.
 

Nashauri ofisi za Tume kusiwe na picha ya Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania [emoji1241]
 
Baada ya Rais Magufuli kutoka kuchukua form ya Kugombea U Rais Alipokua Dodoma kwenye Ofisi za ccm Kuna Maneno ya kimitego kayaongea na Wote tunafaham Lazima Nyumbu wataingia kichwa kichwa tu kwenye huo Mtego.

Ngoja siku zisogee Mpaka pale Mgombea Kupitia Tiket ya chadema Atakapo Enda kuchukua Form Watu wakisha Nasa tawaambia kua Ni Mtego gani ila kwa Sasa acha wenye akil ndio waelewe kwanza.

Ila Vyama vya upinzan hasa Chadema viwe Makin mana naamin kwa Asilimia 100% wao ndio Watanasa kwenye huu Mtego sababu ya Aina ya Mgombea wao na siasa zake za kutaka kunanin hiiiii.

Time will tell
 
Aksante kwa kutufanyia haya yote baba. Mungu akubariki. Ila ka-njaa kanatuuma baba.
 
Sasa mbona huduma za afya ni Bora kipindi bajeti 31B
 
Huyu jamaa Leo ndo anauaga uraisi rasimi,
Nenda baba kavue samaki huko chato
Tuta kumbuka kwa:
Kuteka
Kuua.
Kubambika kesi,
Kejeli kwa wanyonge
Kibri,
 
Hahaha, eti Mgombea wakati ana shikilia na kukalua kiti kinachogombewa.

Wagombea ni wale wengine yeye hastahili kuitwa mgombea.

Muda huu hakupaswa kuwa ofisini kama rais.

Kwanini aliwatumbua wenzake kwa kutia nia tu, ni ili kuwe na usawa katika nafasi wanazozigombea, naye alipaswa kuachia urais ashiriki kugombea nafasi ya irais.
 
Urais mgumu, kwann kachukua ?
 
Miaka 5 hii ameshindwa kutengeneza hizo ajira,kutoa ajira zilizo rasmi haijawahi kua kipaumbele chake na wala haitakua na kwny awamu yake vibarua/saidia fundi imekua ndio ajira rasmi sasa kwa maono yake yeye.

Mwambie wanyonge wanamshukuru sana.
Ingia tovuti ya ajira serikalini uone jinsi vijana walivyoramba ajira
 
Amefanya mengi sana mazuri, anaendelea kufanya mazuri. Akirudi tena aboreshe maisha ya wananchi wake huku akiendelea na hayo mengine. I like his politics, I like the way he makes decisions. My vote for him(though I will not cast it[emoji39])
 
Nina kura mia moja hapa nilipo za JPM, ni kwa ajiri ya pongezi tu.
 
Ingia tovuti ya ajira serikalini uone jinsi vijana walivyoramba ajira
Hahahah nenda kajionee nafasi za watendaji zinatoka 12 waombaji wako 800,kweli ajira zinatolewa nyingi balaa.

Tangu 2015-leo mnaajiri waalimu wote na madaktari kama kawaida,mishahara mmeongeza mpk watumishi wamesema mkuu inatosha sasa hahah.
 
Achukue tu ila kama atasoma hii post yangu atambue kuwa sisi watumishi wa umma hatumpendi.

Wafanyabiashara nao hawampendi, Wakulima wachache about 30 ndio wanampenda.

Kwahiyo akishinda basi ajue kuwa anawaongoza watu wasiompenda.

Wanaompenda wangemfikishia hii post ingemsaidia kushinda uchaguzi. Vinginevyo he's in for a big surprise.

Watanzania wanataka kiongozi huyu:



Ni bora akashughulikia hayo hapo juu hata kabla ya haya hapa chini:

Madhila ya Barabara Rusahunga -Rusumo

Kila la kheri mzee baba.

Ila habari ndiyo hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…