Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akiwa Misungwi; Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa

Huyu Baba la Baba kachanganyikiwa.
Juzi jumapili kawafokea watu kwamba wakichagua upinzani watakoma. Hadi kabadilisha lugha ili wamuelewe.
Leo ana sema tusibaguane. Huyu mzee ana ndimi ngapi? Ni mtu wa kumuogopa sana
Laana ya Uonevu inamtafuna, na tutasikia mengi sana yasiyoeleweka kutoka kinywa chake
 
Dkt. Magufuli asubuhi hii amefanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Misungwi jijini Mwanza na kuwataka Watanzania tupendane.

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi kutobaguana kwa misingi ya chama cha siasa, dini au kabila kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Kadhalika Dkt. Magufuli amewataka wanamisungwi kuchagua Rais, mbunge na diwani kutoka CCM ili waendeleze maendeleo yaliyo katika ilani ya uchaguzi.

Source: Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!

==============

Rais Magufuli leo Jumanne anaendelea na kampeni za kuwania Urais na kuwanadi Wabunge na Madiwani wa chama anachokiongoza. Amepita Misungwi jimbo lilikuwa linaongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga ambalo kwa sasa CCM ilimpitisha ndugu Mnyeti, Hii ni sehemu ya hotuba yake fupi.

DKT MAGUFULI: Ninachowaambia mimi niko nyumbani, ninawashukuru sana watu wa Misungwi mmepitisha mbunge bila kupingwa, mmepitisha madiwani bila kupingwa, hongereni sana. Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? Asanteni sana.

Nataka nieleze ukweli, mlikuwa na mbunge hapa, Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi. Ni lazima tujue historia ilikotoka, mahali tulipo na tunapoenda na Mnyeti atakuwa Mbunge.

Katika mipango ambayo imefanyika hapa ni mingi, hata hili barabara halikuwepo, katika kipindi cha miaka mitano tulilifanya na alienisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nataka niyazungumze haya, bahati nzuri katika kazi zetu huwa sio za maisha. Palikuwa na Nyerere akamaliza muda wake, akaja Mwinyi akamaliza miaka yake kumi, akaja Mkapa akamaliza miaka yake kumi, akaja Kikwete miaka yake kumi na mimi mkitipisha hapa imebaki miaka mitano tu watakuja na wengine.

Hapa tuna mradi mkubwa wa maji ambao utagharimu bilioni 12 utakaonufaisha watu zaidi ya sitini na nne elfu.

Tumeanza vizuri, naomba mtuamini, naomba muendelee kuiamini CCM na hasa mnaona kazi nyingine ambayo inafanyika hapo Kigongo-Busisi, tunatengeneza daraja ambalo halijawahi kuonekana Tanzania na Afrika mashariki, daraja la kilomita 3.2.

Sasa msiache mkanichagua, yakaja mengine yakafuta haya mamiradi kwa sababu gharama ya daraja hili ni bilioni 699, bilioni 700 tunaziweka hapa. Ninachowaomba ndugu zangu wa Usagara na Misungwi endeleeni kushikamana, muwe wamoja. Haya mambo ya siasa yaliyokuwa yanawatenganisha myaache na bahati nzuri ndoa ya Mnyeti, alieiandaa ni Kitwanga.

MNYETI: Mheshimiwa Rais ni kweli kama ulivyosema, ndoa yangu aliiandaa mzee Kitwanga, namheshimu sana, nampenda sana siku zote.

MAGUFULI: Nampongeza Mnyeti kwa kushinda, nawapongeza waheshimiwa madiwani. Ninafahamu kuna appeal zitatokea tokea lakini tusubiri hilo ni kazi la tume pia nawapongeza wananchi wa hapa kwa kushikamana, maendeleo hayana chama.

Nina mke wangu nae nilimuoa Misungwi, mke wa Kitwanga hebu njoo hapa bwana.

MAMA JANETH MAGUFULI: Tunamuombea kura Rais, wabunge, madiwani, mtawachagua? Basi tunawashukuru sana asanteni.

MAGUFULI: Jamani nawapenda, nitakuja siku moja tufanye mkutano hapa.

Dr wake afanye consultation haraka sana kwa Neurologist
 
inategemea wewe unamuonaje,pengine wewe ndo hauko sawa.
So, hata kwenye hilo la kuropoka maneno yanayopishana bado nyinyi mashabiki wake mnaona yuko sahihi ? sio kwamba mnamsaidia kwa kumsifia hata anapoyakoroga bali mnamharibu, Nchi yetu imejengeka kwa kuwa na viongozi wenye staha katika kusema, sio huyo wa sasa
 
mweye staha ni nani Lisu au mtei?
 
Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Mzee choka mbaya....Ubishi tu,vinginevyo angeachia ngazi
 
Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Mzee amepanic huyu,, hakika 28th October tunamwelekeza Kibra asubuhi na mapema!
 
Tunataka mgombea urais anaehubiri amani Kama Dr John Pombe Magufuli hawa wengine wanaohubiri fujo na chuki hakika kura zetu hawatapata tutawaelekeza watoto wetu mama zetu na baba zetu hakuna kuchagua hao wahuni
Anayelazimisha wananchi wasitumie demokrasia yao kuchagua viongozi wawapendao ni nani?
2.Anaeweka hadharani vitisho kwa wananchi kama watachagua viongozi wa upande wa 2 ni nani?
3.Wakati huohuo anayeendelea kuuutumia ujinga wa kutokuwa na uelewa wa wananchi kwa kusema 'Maendeleo hayana vyama ni nani?' Natamani sn hofu ya Mungu ingewatawala wanaotuomba kura kwa mustakabali wa jamani ya nchi yetu.
Eti mkuuu umejifanya kauzu huelewi, muheshimu aliekuweka hai.
 
Dkt. Magufuli asubuhi hii amefanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Misungwi jijini Mwanza na kuwataka Watanzania tupendane.

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi kutobaguana kwa misingi ya chama cha siasa, dini au kabila kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Kadhalika Dkt. Magufuli amewataka wanamisungwi kuchagua Rais, mbunge na diwani kutoka CCM ili waendeleze maendeleo yaliyo katika ilani ya uchaguzi.

Source: Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!

==============

Rais Magufuli leo Jumanne anaendelea na kampeni za kuwania Urais na kuwanadi Wabunge na Madiwani wa chama anachokiongoza. Amepita Misungwi jimbo lilikuwa linaongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga ambalo kwa sasa CCM ilimpitisha ndugu Mnyeti, Hii ni sehemu ya hotuba yake fupi.

DKT MAGUFULI: Ninachowaambia mimi niko nyumbani, ninawashukuru sana watu wa Misungwi mmepitisha mbunge bila kupingwa, mmepitisha madiwani bila kupingwa, hongereni sana. Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? Asanteni sana.

Nataka nieleze ukweli, mlikuwa na mbunge hapa, Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi. Ni lazima tujue historia ilikotoka, mahali tulipo na tunapoenda na Mnyeti atakuwa Mbunge.

Katika mipango ambayo imefanyika hapa ni mingi, hata hili barabara halikuwepo, katika kipindi cha miaka mitano tulilifanya na alienisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nataka niyazungumze haya, bahati nzuri katika kazi zetu huwa sio za maisha. Palikuwa na Nyerere akamaliza muda wake, akaja Mwinyi akamaliza miaka yake kumi, akaja Mkapa akamaliza miaka yake kumi, akaja Kikwete miaka yake kumi na mimi mkitipisha hapa imebaki miaka mitano tu watakuja na wengine.

Hapa tuna mradi mkubwa wa maji ambao utagharimu bilioni 12 utakaonufaisha watu zaidi ya sitini na nne elfu.

Tumeanza vizuri, naomba mtuamini, naomba muendelee kuiamini CCM na hasa mnaona kazi nyingine ambayo inafanyika hapo Kigongo-Busisi, tunatengeneza daraja ambalo halijawahi kuonekana Tanzania na Afrika mashariki, daraja la kilomita 3.2.

Sasa msiache mkanichagua, yakaja mengine yakafuta haya mamiradi kwa sababu gharama ya daraja hili ni bilioni 699, bilioni 700 tunaziweka hapa. Ninachowaomba ndugu zangu wa Usagara na Misungwi endeleeni kushikamana, muwe wamoja. Haya mambo ya siasa yaliyokuwa yanawatenganisha myaache na bahati nzuri ndoa ya Mnyeti, alieiandaa ni Kitwanga.

MNYETI: Mheshimiwa Rais ni kweli kama ulivyosema, ndoa yangu aliiandaa mzee Kitwanga, namheshimu sana, nampenda sana siku zote.

MAGUFULI: Nampongeza Mnyeti kwa kushinda, nawapongeza waheshimiwa madiwani. Ninafahamu kuna appeal zitatokea tokea lakini tusubiri hilo ni kazi la tume pia nawapongeza wananchi wa hapa kwa kushikamana, maendeleo hayana chama.

Nina mke wangu nae nilimuoa Misungwi, mke wa Kitwanga hebu njoo hapa bwana.

MAMA JANETH MAGUFULI: Tunamuombea kura Rais, wabunge, madiwani, mtawachagua? Basi tunawashukuru sana asanteni.

MAGUFULI: Jamani nawapenda, nitakuja siku moja tufanye mkutano hapa.

Mzee wa utopolo katika viwango vyake.
 
Replica, Magufuli anajua pa kuanzia kampeni zake mfano katika miradi mikubwa aliyotekeleza na maendeleo kwa ujumla Sasa sijui wenzetu huwa wanaanzia wapi manake hawana reference.

Kwa heshima na taadhima tunakuomba urudi shule ukasome somo la uraia mpaka utakapotoa ujinga katika ubongo wako, serikali yako imejenga shule za kata usisite kurudi ukasome.

Wapinzani wawe na reference kwani wao ndio walikuwa wameshika nchi? Ni wao ndio walikuwa na serikali? Ni wao ndio walikuwa wanakusanya kodi? Mpaka lini tuwaeleweshe vitu vidogo vidogo kama hivi nyie wanyonge?
 
Nina uhakika usiku wa kuamkia leo, huko Mwanza walifanya kikao cha faragha cha kumkanya aache kauli zake za "sagala sagala"

Hakuna kikao cha ndani kinaweza kukaa kumuonya huyu mtu, amini nakwambia. Kinachomfanya leo ameact kama mtu ni umati wa watu waliokuwa kirumba, majuzi alikuwa amepanikishwa na watu waliokuwa kwa TL kwa ukanda wote ule wa ziwa. Hakuamini na hakujua kama viongozi wa CCM wangeweza kumkusanyia na yeye umati wa kutambia, ni kweli viongozi wamehenyaka kumkusanyia watu ikiwemo wanafunzi wa shule. Kukusanyika kwa watu kirumba kumemfanya ashushe pressure na kupunguza kufokea wananchi na kuwatisha. Magu anapanikishwa na vitu vidogo sana na anakuwa impressed na vitu vidogo vilevile kama kumsifia. Sijui ni lini waTZ wataelewa exactly tabia za huyu mtu, ni wa hovyo sana.

Kuwa na Rais anayepanikishwa na vitu vidogo kama “umati wa watu” ni jambo la hatari sana.
 
Dkt. Magufuli asubuhi hii amefanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Misungwi jijini Mwanza na kuwataka Watanzania tupendane.

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi kutobaguana kwa misingi ya chama cha siasa, dini au kabila kwa mustakabali mwema wa taifa letu...
Kuna vitu sivielewi.

Tupendane... tusibaguane kwa misingi ya vyama, kabila, dini.

Maendeleo hayana vyama.

Msiponichagulia watu wa chama changu siwapi maendeleo.

Siwezi kuwaacha watoto wangu na njaa nikawapa chakula watoto wa jirani!
 
So, hata kwenye hilo la kuropoka maneno yanayopishana bado nyinyi mashabiki wake mnaona yuko sahihi ? sio kwamba mnamsaidia kwa kumsifia hata anapoyakoroga bali mnamharibu, Nchi yetu imejengeka kwa kuwa na viongozi wenye staha katika kusema, sio huyo wa sasa

Wewe unaona mashabiki zake wako sawa? Hao ni wale wale hawana usawa wowote. Juzi nilisema humu anayemshabikia magufuli ana tabia kama zake.

Kwa kuongozwa na sheria za asili, binadamu ni kawaida yetu kushabikia vitu vizuri na kushabikia mtu mwenye tabia nzuri, hii ya kushabikia mtu Muongo, katili, mwenye jazba, asiyependa kupingwa, mropokaji, mdhalilishaji wa wanawake, fisadi, mbaguzi, mkurupukaji, mpenda kusifiwa hata kama sifa za uongo, mnafiki. Lazima tujiulize mara mbili mbili juu ya hawa wanaomshabikia huyu mtu mwenye mambo ya hovyo namna hii.
 
Hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu atawapigia kura CCM
Kwa hiyo tuipigie kura Chadema ambayo imeshindwa hata kujenga ofisi ya makao makuu ya chama licha ya kupata ruzuku ya zaidi ya bilioni tatu kila mwaka? wewe ndiyo akili yako haiko timamu.
 
Back
Top Bottom