Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Anatakiwa kujibu hoja :
  1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
  2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
  3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
  4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
  5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
  6. Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
  7. Mbona anakuwa anatoa majibu kiukali kwani kuna nini vile?
  8. Asititufokee, lazima ajue sisi ndiyo tunamlipa mshahara na kiinua mgongo mara akistaafu.
Hoja zile zile za kukaririshana. Anunue ndege kwa mkopo halafu tulipe pesa nyingi kwenye riba.

Baada ya yeye kumaliza urais uwanja unatumiwa na watu wa Geita. Uwanja wa KIA upo Hai kwa Mbowe na hakuna anayeuhusisha na siasa za vyama kwani upo ulikuwepo na utakuwepo.

Tukumbuke kuwa uwanja wa Mwanza umepanuliwa na unakuwa ni hub ya Tanzania na unapokuwa na hub ni lazima uwe na strategic aerodrome yaani uwanja wa akiba ambao haupo mbali nao. Mfano uwanja wa Dar unayo akiba ya Zanzibar uwanja wa KIA unayo akiba ya uwanja wa Arusha.

Sekta ya anga inatazamwa kisiasa badala ya kuangaliwa kama ni fursa kubwa huko tuendako.

Hoja nyingi ni za kisiasa zisizo na maono ya mbali.
 
Sio hivyo,,kipindi cha jk wapinzani walimlaumu sana kwa kufa kwa shirika la ndege,,jpm akaona hili tatizo aliondoe,ndiposa akaamua kulifufua shirika la ndege
Ttzo la ATC sio kuwa na ndege ttzo Ni management Nyerere alizinunua zaidi ya kumi na kitu ,idi amini alizinunua 62 lakini zote zilikufa.

Pesa ya kujenga Chato angeboreshea maisha ya wanachato kwa kujenga vitu vinavowagusa wananchi mfano vyuo, schems za umwagiliaji, usambazaji maji vijijini, vyuo vya ufundi, mashule, maghala, viwanda vya mifugo na mazao, Chato nzima wenye kumudu kupanda ndege awafiki hata 5 Sasa hapa uwanja unafaida gani kwao.

Kesho Lisu anakuwa raisi nae akajenge ikungu uwanja wa ndege, kesho kutwa bashite anakuwa raisi akajenge koromije uwanja je hio Ni nchi au Ni shamba la Bibi.
 
We umepanda ndege lini,nauli ya basi tu kwenda kwenu kijijini inakushinda,biashara ya ndege awaachie mashirika binafsi ,serikali ijenge viwanja tu
Du! Rwanda air,Kenya air,Qatar air,egpty air,Ethiopia air hizo za sekta binafsi ,nakushauri uwe unaperuzi kupata taarifa kwa kina duniani kote mashirika muhimu umilikiwa na serikali ili kuepusha tabia za wafanyabiashara kuhujumu,mfano:hapa Tanzania tulihujumiwa kwenye umeme baada ya magu kuingia mgao hamna tena,sukari pia magu kampa bahresa ardhi ajenge kiwanda kikubwa na kingine kinajengwa na huko huko,mambo mengi ukiachia kila kitu sekta binafsi hipo siku watawahujumu ikizingatiwa kuwa makampuni hayo yote ya wazungu ni rahisi sana kutuhujumu,ndio maana uchaguzi wa mwaka huu husikii maelekezo ya wazungu kwa sababu umegharamiwa na serikali 100% ,sasa endeleeni kumuunga mkono huyo lisu anampango kila kitu kiwe kinafanywa na wazungu mtatawaliwa kwa Mara ya pili.
 
Ndege gani imetua hicho kiwana cha chato ?
Ni mbili had Sasa ya museveni,ya Kenyatta,na atc Tena kwa mwaka Mara moja huu Ni ufisadi na ubinafsi wa Hali ya juu na kuchezea Kodi zetu,heri zingetumika kuwalipa watu mafao yao mwaka wa pili huu wanasota
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
Wewe sio kamanda umejiunga September hii 13, 2020.

Acha shobo ukisema wewe ni yumbu wa kijani kuna tatizo?[emoji23][emoji23]
 
Sio hivyo,,kipindi cha jk wapinzani walimlaumu sana kwa kufa kwa shirika la ndege,,jpm akaona hili tatizo aliondoe,ndiposa akaamua kulifufua shirika la ndege

Watanzania tumejaa chuki za kipuuzi mpaka tunasahau siku za nyuma tulisema jambo gani.

Hao hao waliomcheka JK kwa kushindwa kuwa na shirika la ndege ndio hao wanaosema leo kuwa ndege hazina faida.

Watanzania ni kuwasikiliza na kuendelea na shughuli zako kama vile hawapo.
 
Ttzo la ATC sio kuwa na ndege ttzo Ni management Nyerere alizinunua zaidi ya kumi na kitu ,idi amini alizinunua 62 lakini zote zilikufa.
Pesa ya kujenga Chato angeboreshea maisha ya wanachato kwa kujenga vitu vinavowagusa wananchi mfano vyuo, schems za umwagiliaji, usambazaji maji vijijini, vyuo vya ufundi, mashule, maghala, viwanda vya mifugo na mazao, Chato nzima wenye kumudu kupanda ndege awafiki hata 5 Sasa hapa uwanja unafaida gani kwao.
Kesho Lisu anakuwa raisi nae akajenge ikungu uwanja wa ndege, kesho kutwa bashite anakuwa raisi akajenge koromije uwanja je hio Ni nchi au Ni shamba la Bibi.
Sasa unataka rais akitaka kutua kwao anatua vipi?,uwanja wa ndege ni muundo mbinu tu,wala nchi haitafiriska eti sababu ya huo uwanja,,mbona viwanja vipo vingi tu,
Huu uwanja sio big ishu kivile..
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
Tuambie wewe ilikaguliwa lini tangu 2016 na ripoti ya ukaguzi ilisomwa wapi?
 
ATCL ina madeni mengi sana. Kama ndege zingeinyizwa huko lazima zingechukuliwa na wadai. Airline nyingi zina hasara. Ina maana sababu ya hasara ndio hatuhitaji ndege?

..unaweza kuingia hasara au gharama ktk jambo la lazima.

..hakukuwa na ulazima wa sisi kubeba mzigo wa hasara na kuanzisha shirika la ndege la umma.

..watalii walikuwa wanaletwa na mashirika ya ndege ya nje bila matatizo yoyote.

..kwa usafiri wa ndani kulikuwa na mashirika ya ndege ya binafsi.

..matrilioni ya fedha tulizotumia kununua midege tungeyaelekeza kwenye sekta nyingine zenye mahitaji na zenye kuajiri watu wengi.
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
We jiropokee tu.
Screenshot_2020-09-14-15-38-39-1.jpg
 
Hivi ni ujinga au mazoea mabaya kusema ndege hazina wapandaji,tatizo hamna akili kama taifa tunaitaji ndege na viwanja kila wilaya ili use usafiri wa kawaida tu kwa wananchi MTU achague mwenyewe ahende kwa ndege,gari,meli au treni hayo maujinga ya kuamini kuwa ndege ni anasa ukome huko huko kwa uyo alirudi kutoka Belgium kwa pikipiki.
Hatuna shida na ndege tuna shida na haya

  1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
  2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
  3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
  4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
  5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
  6. Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
  7. Mbona anakuwa anatoa majibu kiukali kwani kuna nini vile?
  8. Asititufokee, lazima ajue sisi ndiyo tunamlipa mshahara na kiinua mgongo mara akistaafu.
 
Sio hivyo,,kipindi cha jk wapinzani walimlaumu sana kwa kufa kwa shirika la ndege,,jpm akaona hili tatizo aliondoe,ndiposa akaamua kulifufua shirika la ndege
Hapo ndio upeo wako wa kufahamu Hilo suala ulipoishia.?
Au kuna lingine unalolifahamu!!?
 
Back
Top Bottom