Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Basi akubali tu ukaguzi ufanyike kwenye mradi wa ndege
 
"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? ,ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11..hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli

Hoja za Wadau,wapiga kura hawajaridhika
expand...

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
Huo uwanja wa chato ni kwa ajili kuvuta watalii wa mbuga ya Burigi, watalii watatua Chato ambapo ni karibu na mbuga ya Burigi badala ya kutua mwanza
 
Kwani tusingekuwa na ATCL tungekosa huduma ya ndege? wakati mwingine si lazima umiliki chombo chausafiri ili uweze kutumia huduma zake

It is just about national pride. Some of these things hardly make business justification. Bit their existence is unquestionably
 
Ni kweli kabisa mkuu ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa wabongo wengi kutokana na maoni wanayoyatoa yamejaa ulalamishi sana na huwezi kujua ni nini hasa wanakihitaji. Wakati wa JK walimponda sana na kelele nyingi za ufisani na nchi kukosa mwelekeo. JPM kwa sehemu kubwa kafanyia kazi malalamiko mengi kwa vitendo kiasi cha kukipa chama cha CCM nguvu na watu kukiamini tofauti na kipindi cha JK. Vilevile kuna mwelekeo kama nchi tunauona na ni vizuri kutambua kazi kubwa ambayo JPM ameifanya licha ya mapungufu ya hapa na pale ambayo ni kawaida ya binadamu yeyote yule. Ukiondoa mihemko na kelele nyingi za hapa na pale na ukitafakari kwa kina bila msukumo wa kelele za nje utakubali kuwa JPM kaitendea haki Tanzania.
JPM karudisha nidhamu ya kiserikali na ya mtu mmoja mmoja.

Kulalamika, kukejeli ni sifa za dunia ya Twitter na facebook. Ni kuwavumilia tu hawa waungwana.
 
"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? ,ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11..hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli

Hoja za Wadau,wapiga kura hawajaridhika
expand...

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?

Haya ni maswali magumu sana ambayo msitegemee atoe majibu kwani kun siri kubwa imejificha, mtaambulia matusi tu, na hata wapambe wake na ccm kwa ujumla hawawezi kujibu hayo maswali kwani hata wao wenyewe hawajui kilichofanyika na kilichojificha nyuma yake.
Hivi hapa ilikuwa wapi na lini?
VID-20181228-WA0005.mp4
 
Attachments

  • VID-20181228-WA0005.mp4
    1.5 MB
..unaweza kuingia hasara au gharama ktk jambo la lazima.

..hakukuwa na ulazima wa sisi kubeba mzigo wa hasara na kuanzisha shirika la ndege la umma.

..watalii walikuwa wanaletwa na mashirika ya ndege ya nje bila matatizo yoyote.

..kwa usafiri wa ndani kulikuwa na mashirika ya ndege ya binafsi.

..matrilioni ya fedha tulizotumia kununua midege tungeyaelekeza kwenye sekta nyingine zenye mahitaji na zenye kuajiri watu wengi.

Shida yetu wengi tupo kisiasa kuliko uhalisia. Hata tukiziondoa hizo ndege, kesho zitadaiwa kama vile kuwa nazo ilikuwa lazima. We can't get satisfied as usual. But leadership is about making some choices and stand by them 100%. What remains thereafter, is the analysis of what were the successes and failures.
As of me, JPM aendelee na aliyochagua. Muda ndio utaamua kama alichemsha au la. Sababu tunahitaji national carrier kama mataifa mengine. Just for a national pride!
 
Kujenga kiwanja sio upotevu wa mapato,ni investment...miaka 50 toka sasa huo uwanja utawafaa vizazi vijavyo

Una zungumzia Miaka 50 Mkuu na hujaangalia gharama za kuutunza huo Uwanja ili uendelee kuwa kama ulivyo sasa ,yani Miaka 50 Watanzania Kodi zao zichomeke tu kwa jambo litakalo wanufaisha Miaka 50 ijayo ..umefikiri vizuri kweli Mkuu ?

Ni kwa nini tusiwe na Plan hata kwenye Kilimo ukizingatia Asilimia karibia 80% ya Watanzania wana tegemea Kilimo !?.Tufungue Masoko kwa Wakulima kuwa huru kuuza Mazao yao nje na kupata Faida zaidi ,hata huu utitiri wa Machinga ktk Miji mikubwa unge pungua na Serikali ingekusanya Kodi kubwa kutoka kwa Wakulima.

Mtu anae fikiri sawasawa na kwa ajili ya Watu wengine ni lazima atapima lile lenye Faida zaidi ya jingine na kuanza nalo kwa ajili ya Watu wako.
 
Economic of scale, ujengapo uwanja unaangalia vipaumbele, Ni heri ungejengwa Geita mjini Kama mkoa. Au mugumu Serengeti kwa lengo la kuwaleta watalii mbugani kiurahisi badala ya kutua KIA au Jomo Kenyatta kwa watakao kuja Serengeti kutalii
 
KWANI KUNASHIDA GANI KUJENGA UWANJA CHATO?
KWANI CHATO SIO TANZANIA?
KWANI UWANJA WA NDEGE CHATO SI UWANJA WAWATANZANIA WOTE?
KWANI UWANJA WA CHATO NI MALI YA MAGUFULU NA FAMILIA YAKEEE??

Hata huku kwetu Mafinga ni Tanzania. Ungejengwa huku basi...

Anyway nilikuwa najaribu kukusanifu kidogo....

Hata hivyo hebu tuwe free na serious kidogo kulijadili hili....

Honestly, hii hoja yako ya kutetea bilioni karibu 100 kutumika kujenga uwanja mpya wa ndege wa kimataifa kijijini na shambani kwa Rais, huko Chato ni butu sana na haisimami ktk vipimo vyote...

Katika KUPANGA na KUTEKELEZA mipango ya maendeleo ni lazima tuongozwe na vipaumbele (priorities)...

Hebu tujiulize maswali haya muhimu na msingi sana;

Kwamba;

å Hivi Rais kujiamulia kujijengea uwanja wa ndege i.e CHATO INTERNATIONAL AIRPORT kijijini na shambani kwake Chato ni busara kweli?

å Ilikuwa ni kapaumbele kweli kuliko kukipanua cha Mwanza ambacho ni cha muhimu ktk ku sevu naeneo ya utalii ya Sanane, Serengeti, Rupondo na Ziwa Victoria menyewe nk ili kiwe na hadhi ya kimataifa na kipo kilometa zisizozidi 150 kufika Chato kijijini kwake?

å Assessment ya faida na hasara ya kujenga New CHATO INTERNATIONAL AIRPORT ilifanyika kweli? Iko wapi?

å Je, hivi kweli hii siyo tamaa tu ya Rais Magufuli ya kutaka na kupenda ufahari ndiyo ilimsukuma kutenda hili?

å Je, haya siyo matumizi mabaya na yasiyo sahihi ya rasrimali fedha kweli?

Angetaka kushauriwa tungemwambia, hiyo fedha aliyojengea CHATO INTERNATIONAL AIRPORT (karibu Tshs billion 100), angeipeleka kutumika kupanua Mwanza Airport ili uwe ni uwanja wenye hadhi kimataifa...

Hapo hakuna ambaye angemshangaa wala kumlaumu. Kwa hili la CHATO AIRPORT, alichemka, ni ufisadi tu wala hakuna haja ya kupepesa macho ama kuuma uma ulimi kulitamka...!!
 
"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? ,ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11..hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli

Hoja za Wadau,wapiga kura hawajaridhika
expand...

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
Ndio sababu tunataka mdahalo wa wagombea Urais ili hayo majibu yake akayatolee ufafanuzi huko, tatizo yeye na CCM yake hawataki kabisa kusikia kuhusu huu mdahalo. Shida ni nini?
 
We umepanda ndege lini,nauli ya basi tu kwenda kwenu kijijini inakushinda,biashara ya ndege awaachie mashirika binafsi ,serikali ijenge viwanja tu
Duuu unasikitisha sana kufikiri kuwa mpaka wewe upande hizo ndege ndiyo itakuwa sawa kujenga uwanja wa Chato! Uwanja huu na ndege zilizonunuliwa zinakuja kukuza biashara ya utalii na madini katika kanda hii. Watalii wengi watapenda kuja kuona Hifadhi mpya k.m. Chato Burigi, n.k. Wameshaona Serengeti, Manyara, n.k. Huu ni mkakati wa kukuza pato la Taifa. Halafu mimi nawashangaa sana hivi Wana-Chato ni dhambi uchumi wao kuongezeka? Vilevile ukiona Chato kuzuri nenda tuu ukaanzishe bishara zako huko, ruksa.
 
"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? ,ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11..hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli

Hoja za Wadau,wapiga kura hawajaridhika
expand...

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
Pia mmiliki wa kampuni ya ujenzi huo uwanja Ni Nani.
Je kila raisi ajae nae ajenge uwanja kwao
 
Ni afrika pekee raisi ni mungu thus maendeleo tutayasikia ndotoni, afrika itakuwa na maendeleo Kama tukianza kuwafunga jela maraisi wahuni

Mfumo Mkuu ndio Shida Nchi hii ,wakiondoka hawa wenye Mawazo ya kidikteta Sheria kandamizi na zisizo kuwa na Faida zikiondolewa moja kwa moja tunakuwa tumeufuta huu Mfumo mmbovu unao toa mwanya kwa Mtu mmoja kuharibu Maisha ya wengine.
 
Ndio sababu tunataka mdahalo wa wagombea Urais ili hayo majibu yake akayatolee ufafanuzi huko, tatizo yeye na CCM yake hawataki kabisa kusikia kuhusu huu mdahalo. Shida ni nini?
Unataka ngumi zilike.Pia Ni ngumu kutazamana macho usoni na mtu uliyemtenda mabaya
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja

Weka faida kabla ya Corona.
 
Duuu unasikitisha sana kufikiri kuwa mpaka wewe upande hizo ndege ndiyo itakuwa sawa kujenga uwanja wa Chato! Uwanja huu na ndege zilizonunuliwa zinakuja kukuza biashara ya utalii na madini katika kanda hii. Watalii wengi watapenda kuja kuona Hifadhi mpya k.m. Chato Burigi, n.k. Wameshaona Serengeti, Manyara, n.k. Huu ni mkakati wa kukuza pato la Taifa. Halafu mimi nawashangaa sana hivi Wana-Chato ni dhambi uchumi wao kuongezeka? Vilevile ukiona Chato kuzuri nenda tuu ukaanzishe bishara zako huko, ruksa.

Mwanzo hatukuwa na hizo Ndege na Watalii wlaikuja ,sidhani na sioni upenyo wa kuikubali hoja yako kuwa tutakapo kuwa na Ndege nyingi tutakuwa tume ongeza idadi ya Watalii how ?
 
"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? ,ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11..hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli

Hoja za Wadau,wapiga kura hawajaridhika
expand...

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka chato?
5. Baada ya yeye kumaliza uraisi huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
Tunataka mdahalo
 
Back
Top Bottom