The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Ubaguzi wanauleta wenyewe halafu wanaleta propaganda kuwageuzia wenzao.Ikiwa ni siku saba zimebaki kuelekea uchaguzi mkuu, mgombea wa Urais kupitia CCM Mhe. Dkt. John Magufuli, amewataka watanzania kujitenga na propaganda za ubaguzi zinazoenezwa na baadhi ya wagombea.
Pia amewatahadhalisha watanzania wakiona mtu anaongea kuhusu chuki, wafahamu kwamba hayupo kwa maslahi ya Taifa, bali ana malengo mabaya ya kuleta machafuko nchini.
Alitoa rai hiyo jana wilayani Korogwe mkoa wa Tanga wakati akihutubia wanachama wa CCM waliojitokeza kwenye viwanja vya chuo cha walimu Korogwe.
Mbowe ameomba mpaka maridhiano, jamaa hakumsikiliza kwa kuwa alifikiri upinzani umekufa na watu wanampenda kuliko. Sasa naona habari ameanza kuisikilizia na ujumbe kaupata.
Tunajua kuwa lazima atashinda uchaguzi huu, whether kwa halali au kwa haramu ..... kitu cha kufanya ajirekebishe. Hivi haoni ni kwa nini yeye anashambuliwa sana na wananchi bado akiwa madarakani tofauti na watangulizi wake ...!!? Kwa kuwa nchi yetu AMANI ipo cha kukazania sasa ni HAKI .... hiki kitu jamaa hawataki kukizungumzia kabisa. Inaelekea dhuruma imeshawalewesha!!