Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Bunda walijichanganya wenyewe, Utawapelekeaje Barabara watu wanaokutukana?

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Bunda walijichanganya wenyewe, Utawapelekeaje Barabara watu wanaokutukana?

“Bunda walijichanganya wenyewe, Ilani hii lengo kutengeneza Barabara kutoka kwa Lugola kule tukaunganishe na ukerewe kuja hadi Bunda baadaye tunaipasua hadi Serengeti lakini utawapelekeaje Watu wanaokutukana?, hata kama ni Malaika utagoma kidogo”

"Lakini utawapelekeaje watu wanaokutukana hata kama ni malaika utagoma kidogo. Mimi sio malaika nina roho na moyo na hata ukiwa na chakula kizuri huwezi ukampelekea mtoto wa jirani utampelekea mtoto wako wa kuzaa kama ana njaa" - Magufuli

View attachment 1559749
Huyu jamaa asipoangalia anaweza kosa kura hata za wajinga anaowategemea

Maana sasa watu wanaanza kuona rangi zake halisi kuwa ni mtu Mwenye roho mbaya, chuki na visasi visivyo vya kawaida

Watu wanavinyongo sana. Kwani hizo pesa za kujenga barabara ni za ccm au ni kodi ya watanzania wakiwemo wananchi wa bunda? Matatizo ya watu wengine wakikataliwa basi unallazimisha ukubaliwe.
La ajabu hao hao wanaonyimwa haki wanaendelea kuishabikia serikali ya ccm. Wakome kabisa, huyo mtu si wa kuchaguliwa, na wakilogwa wakamchagua ataendelea kuwanyanyasa. HIYO NDIYO SURA HALISI YA CCM
 
Sehemu pekee nchini Tanzania ambapo waweza kudhani Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii ni Jamii Forums tu. Ila ukweli na uhalisia ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Tanzania. Sio 2020 tu, ni NEVER (KAMWE)
Nini kinachokufanya ujiaminishe hivyo

Kama

2005 Kikwete alipata kura Milioni 9
Sawa na 80%

2010 Kikwete kura milioni 5
Asilimia 61

2015 Maguful ccm pamoja na kuibakoote walipata
Asilimia 58.

Hapo ukumbuke mwenyekiti wa NEC ni wao (wanamteua wao)

Mkurgenzi ni wao (wanamteua wao)

Wakurugenzi wa halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi wanateuliwa na mwenyekiti wa ccm, ni makada wao.

Majeshi yote wanaamrisha wao

Kodi zetu (hazina) wanasimamia wao na wanazitumia sana kwenye kampeni

Unaweza ukaona CCM walivyo wepesi kuondoka madarakani kwakuwa wananchi ndio tunaamua
Na tumeamua tumeichoka ccm na tunaiangusha vibaya hakuna wa kutuzuia.

Mtabeba watu sana kwenye malori kuwalazimisha watumishi kuja kwenye mikutano yenu lakini ukweli unajulikana na hamtakuwa nao kwenye sanduku la kura.
 
Nani amekuambia ccm itashinda, ccm itatangazwa washindi na sio kushinda. Hapa tunachofanya ni kupush mkapewe huo ushindi wa mezani na sio wa kura. Ccm kutawala milele sio shida maana sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha dola kilichojivika koti la chama cha siasa. Hivyo kwetu tunachukulia ccm kutawala, ni kama nchi iliyopinduliwa na jeshi.
Tumeccm NECCCM wanatembea na matokeo mifukoni kwa njia haramu, hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu anaichagua CCM, kitakachokuja kufanyika ni NECCCM kuwatangaza CCM ni washindi kwa njia haramu za kishetani
 
Mimi binafsi sijawai muelewa jiwe, nashangaa baadhi ya watz wenzangu wanapomsifia huyu mtu
Ni watz waliojazwa hofu na wakukubali kuwa na uoga.
1599378743305.png
 
Mzee mkapa ametuachia kituko
Marehemu mkapa alikuwa kachoka vituko akataka kutema nyongo lakini wakamuwahi sasa yupo kaburini mungu amlaze mahala pema peponi
 
Naam!

Na amebugi kwelikweli kutoa kauli ya vitisho na dharau mkoa wa Mara yani amebugi kwelikweli na amerudia tena akiwa Musoma.

Alidhani yuko Dodoma au Tabora ndio ccm wamezoea kuwaburuza

Watakachomfanyia hataamini.
Maendeleo siyo Hisani ya CCM wala pesa binafsi tokea mfukoni mwa mtukufu mwenyekiti wa CCM bali maendeleo ni pesa za walipa kodi wa eneo husika
 
Nchi ina miaka 59 haina maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani kisa ni CCM kuwa na mfumo wa hovyo kuchota pesa Hazina BOT kienyeji pasipo idhini ya bunge, Tanzania ilipaswa iwe level ya America, German, India, UK, Canada, China, Urusi, na mataifa yote tajiri kutokana na kumiliki rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, lakini chini ya CCM inazidi kudidimiza demokrasia na kimaendeleo, pesa za viwanda pesa za maendeleo inatumika kuidhoofisha chadema kuua upinzani, pesa nyingi inapotelea kwenye mambo yasiyo na tija kwa Taifa.
 
Nini kinachokufanya ujiaminishe hivyo

Kama

2005 Kikwete alipata kura Milioni 9
Sawa na 80%

2010 Kikwete kura milioni 5
Asilimia 61

2015 Maguful ccm pamoja na kuibakoote walipata
Asilimia 58.

Hapo ukumbuke mwenyekiti wa NEC ni wao (wanamteua wao)

Mkurgenzi ni wao (wanamteua wao)

Wakurugenzi wa halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi wanateuliwa na mwenyekiti wa ccm, ni makada wao.

Majeshi yote wanaamrisha wao

Kodi zetu (hazina) wanasimamia wao na wanazitumia sana kwenye kampeni

Unaweza ukaona CCM walivyo wepesi kuondoka madarakani kwakuwa wananchi ndio tunaamua
Na tumeamua tumeichoka ccm na tunaiangusha vibaya hakuna wa kutuzuia.

Mtabeba watu sana kwenye malori kuwalazimisha watumishi kuja kwenye mikutano yenu lakini ukweli unajulikana na hamtakuwa nao kwenye sanduku la kura.

Kwa hiyo 80%,61%58%....
Hali Ni tete.
 
Kama siyo CCM mda huu Tanzania ingekuwa ipo kwenye G5 na ingekuwa na kura ya veto
 
Sehemu pekee nchini Tanzania ambapo waweza kudhani Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii ni Jamii Forums tu. Ila ukweli na uhalisia ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Tanzania. Sio 2020 tu, ni NEVER (KAMWE)
Ndugu mtabiri, ebu tutabirie ni nani atakaa awe Rais?
 
Lissu aje aseme yeye atashirikiana na kila mwananchi, nampenda JPM ili aje arudishe akili sawa za viumbe lakini kwa hili sikubaliani nalo sababu linamfanya aonekane ni mtu katili mpaka kuamua maamuzi ya watu.
 
Sehemu pekee nchini Tanzania ambapo waweza kudhani Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii ni Jamii Forums tu. Ila ukweli na uhalisia ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Tanzania. Sio 2020 tu, ni NEVER (KAMWE)
ni lini ulikaa na Mungu mkapanga hayo?
 
Back
Top Bottom