Uchaguzi 2020 DKT. Magufuli: Sasa ni wakati wa kujali maslahi ya Wafanyakazi

Uchaguzi 2020 DKT. Magufuli: Sasa ni wakati wa kujali maslahi ya Wafanyakazi

Baada ya JPM kutuumiza wafanyakazi kwa miaka mitano HATUDANGANYIKI kwa ahadi zake zenye harufu ya kitapeli
 
Ameanza kutapatapa.

Kwani ofisi inaongoza watu au watu wanaongoza watu, yeye si aliona anaongoza watanzania misukule sasa atautapika msukule wake
 
Heeeee heeeeee eeeee
Tuendelee tu na hizi kampeni ila heee
 
Shekhe Ponda kasema CCM wamekuwa Waongo kwa sababu wanatuona sisi Watanzania ni Mambumbumbu

Tarehe 28 ndio wanatakiwa tuwafukuzie Vijijini mwao
 
Tena katili haswa
Mimi Mtumishi wa Umma, nipata salary incliment 98,000/=, Mwaka 2016, salary incliment 102000 Mwaka 2017 up to date naendelea kupata.
Ubora wake Kiuchumi wa Mtumishi: Haijaongeza Mfumuko wa Bei, tofauti na zamani ukiongezewa 15,000 na bei ya kila bidhaa inapanda. Naamini mmenielewa JPM anaakili kuliko kikosi chote cha Mihemko Forum
 
Mimi Mtumishi wa Umma, nipata salary incliment 98,000/=, Mwaka 2016, salary incliment 102000 Mwaka 2017 up to date naendelea kupata.
Ubora wake Kiuchumi wa Mtumishi: Haijaongeza Mfumuko wa Bei, tofauti na zamani ukiongezewa 15,000 na bei ya kila bidhaa inapanda. Naamini mmenielewa JPM anaakili kuliko kikosi chote cha Mihemko Forum
Mpuuzi wewe labda mtumishi wa ibilisi, mtu hata kuandika hujui utakuwa ladba umeajiriwa na ukoo wa panya
 
Wakuu wa mikoa wanahangaika kupita kuongea na wasimamizi wawasaidie, wangejua wasingepoteza muda wao
Wapo wengi mkuu
Elimu haija isaidia, baada ya uchaguzi wasubiri visasi na wasilalamike,Magu ni zaidi ya dikteta
 
Ila huyu mheshimiwa Mungu amjalie tu.

Watumishi wa umma walikua wanapanda daraja kila baada ya miaka mitatu,akatengua na kupeleka mitano lkn hata hiyo mitano watumishi wengi hawajafanikiwa kupanda, aliyemwachia kiti alikua anaongeza walau 40,000/= hadi 80,000/= kwa mwaka,yeye hakufanya na kusema yeye anaona Stiglers gorge ni ya maana kuliko mishahara kupanda.

Mwenzake alisema sio kwamba hakujua kwamba kuna watumishi wenye vyeti feki ila waliona wabane mfumo wa kutoa vyeti na kukagua vyeti feki wakati wa kuajiriwa na tatizo litajimaliza maana hakuna wapya watakaoingia kwenye ajira. Yeye akawatumbua onspot,watu wamepoteza uhai,baadhi ya familia zinaishi maisha magumu sana.

Leo unataka hawa watu ndio wakupigie kura kweli? Basi bwana Mungu mwenyewe ndio anajua.
 
Huyu sie yule aliyewapiga za uso wafanyakazi siku ya Mei Mosi kwa miaka mitano mfululizo?

Sitashangaa kabla kampeni kuisha nikiskia waliochishwa kazi kwa vyeti feki watarudishwa makazini na kulipwa mishahara yao ya miezi yote waliokaa nje ya ajira.
 
Dunia nzima hakuna vyama vyenye ofisi, ni Tanzania tu. Wapi ipo office ya Republican au Democratic? Tusidanganyane hapa, CCM imetuchangisha michango wakati wa mfumo wa chama kimoja kujenga maofisi ambayo leo hii ingekuwa mali ya serikali. Ofisi za vyama zinakuwa active wakati wa chaguzi tu....Hapo ndipo wanapokodi nyumba ya ofisi na si vinginevyo.

Uchumi wa chini kati tulishafikia tangu wakati wa Kikwete ila hakutaka ku-declare kwa sababu misaada ingepungua.....Sasa huyu ili kutaka sifa akaona hilo litam-boost. By the way Tanzania bado ni nchi maskini sana, kati ya idadi yake ya watu Mil 58, Milioni 29 wanaishi kwenye umaskini wa kutupwa. Msijifariji....SAFARI BADO NI NDEFU.
Kwa hiyo kwa akli yako kitendo cha Tanzania kutangazwa kuingia uchumi wa kati wewe kumekuudhi sana? Daah ama kweli tunakiwa tukamuliwe zaidi ili akili irudi pamoja!
 
Najua kwamba wataiba kura,lkn mimi nitakwenda kupiga kura ili kujiondoa kwenye laana na kujisafisha mbele ya mwenyezi Mungu kwamba sihusiki na madhira na mateso yoyote yatakayofuata katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Mungu anitie nguvu.
Fanya kazi jitume na tumia akili usifikiri kuna mtu hapa dunianai atakuletea hela huku wewe umebweteka tu. Hata umachague Tundu hatakuletea hela kirahisi hivyo na pengine hali ndiyo inaweza kuwa mbaya zaidi labda kama atauza nchi kwa wanyonyaji ili awadanganye na vimisaada vya fedha kwenye mzunguko wa fedha nchini kama ilivyo kwa baadhi ya majirani zetu!
 
Hakuna mfanyakazi atakaa achague huyu dhalimu. Anajidanganya tu.

Si alijifanya kuwafokea! Leo maji yamemfika shingoni ndo anaanza kutapatapa. Ameshachelewa yaani.
Sasa unadhani wamchague nani..kwa sababu Lissu na Membe ngoma isomile tayari..wapinzani nadhani wanawapotezea muda wananchi..waende wakatatute kazi nyingine ya kufanya..siasa hawaziwezi
 
Back
Top Bottom