Dkt. Magufuli tafadhali vumilia, mwaka huu ni zamu yako. Lowassa alivumilia ingawa aliumia

Dkt. Magufuli tafadhali vumilia, mwaka huu ni zamu yako. Lowassa alivumilia ingawa aliumia

Hzo spana za kawaida Sana na haziwez athiri kishindo cha ushindi cha mweshimiwa , anamsaidia Tu kufanya marekebisho fulan fulan Kwa miaka mingine mitano lakini to knock him out , sio kazi ya kukamilishwa na sku 44 za kampeni zilizobaki
Dingilai analala na viatu safari hii na Jana makambako Lissu kaongezea tena sukari kwenye asali.

Kampeni zikiisha lazima apelekwe nje akapime sukari, lasivyo kama atafanikiwa kushinda basi tutegemee nchi yetu kuongozwa na rais mwanamke
 
Mwaka 2015, aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CHADEMA Edward Lowassa aliteseka sana. Alisemwa vibaya, alikejeliwa, alidhihakiwa, 'alitukanwa' alidhalilishwa na kutwezwa vya kutosha na kutisha. Lowassa alikosa ushawishi katika jukwaa la kampeni. Alikosa maneno ya kuongea. Aliishia kupata kigugumizi na kutoa salamu ya CHADEMA tu. Watu walijaa kwenye mikutano yake lakini hakuwa na cha kuwaambia kilichowavutia. Ulikuwa mwaka wake!

Mwaka huu, CHADEMA wana mgombea (Tundu Lissu) anayejua kusema, kusimanga, kunanga, kujenga hoja, kukera, kutangaza sera, kushawishi na kutupa vijembe. Mwaka huu makombora yanaelekezwa kwa Dkt. Magufuli, mgombea wa CCM. Yanaelekezwa kwake kwakuwa kwa miaka yote mitano ya awamu yake, ni yeye tu ndiye aliyekuwa akitajwa kwenye kila jambo linalohusu Serikali. Sifa zote alipewa yeye. Sasa apokee na kukosolewa yeye mwenyewe.

Mwaka huu, kwa nilivyomfuatilia, Dkt. Magufuli ameishiwa cha kuzungumza. Ameishiwa hoja. Hana jipya kwenye kampeni zake. Sasa imebaki 'kukopi' na 'kupesti' kutoka kwa Lissu. Mfano, jana tu ameahidi Bima ya Afya kwa kila mtanzania. Ni ahadi na sera ya Lissu tangu mwanzo. Nani kampa Dkt. Magufuli sera hii ya kuiga? Nasema, Dkt. Magufuli aseme mambo mapya; si abaki na yale yale na kuyasema vilevile.

Aseme alichoahidi mwaka 2015; alichofanikiwa na alichoshindwa. Halafu, aseme atawezaje kutimiza kile alichoshindwa. Wakati huohuo, avumilie 'madongo' ya mpnzani wake uchaguzini Lissu na kujibu kwa kutulia. Ajibu kwa kueleweka. Ajibu kwa hoja za haja. Mwaka huu ni mwaka wake, ni zamu yake katika kukosa cha kushawishi ingawa umati wa wananchi 'hukusanywa' na 'kuandaliwa' kutoa tafsiri ya kukubalika kwake.

Abadili santuri. Hakuna kipindi redioni au runingani kinachopiga wimbo mmoja tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Shinyanga Mjini)
Mwaka 2015, aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CHADEMA Edward Lowassa aliteseka sana. Alisemwa vibaya, alikejeliwa, alidhihakiwa, 'alitukanwa' alidhalilishwa na kutwezwa vya kutosha na kutisha. Lowassa alikosa ushawishi katika jukwaa la kampeni. Alikosa maneno ya kuongea. Aliishia kupata kigugumizi na kutoa salamu ya CHADEMA tu. Watu walijaa kwenye mikutano yake lakini hakuwa na cha kuwaambia kilichowavutia. Ulikuwa mwaka wake![emoji1536][emoji1536][emoji1536][emoji617][emoji617][emoji617]
 
Nikupe pole tu kwa kuwa poyoyo maana hoja zako ni vioja vya Lissu.

Ukisoma Ilani ya CCM, Uchaguzi Mkuu 2015, ndiyo yakiyotekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Unadai kwamba Sasa imebaki 'kukopi' na 'kupesti' kutoka kwa Lissu. Mfano, jana tu ameahidi Bima ya Afya kwa kila mtanzania hujui unachosema maana Lissu ndiye anafanya 'kukopi' na 'kupesti' ya CCM kama yalivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2020 (soma ukurasa wa 131-138)
Kujenga uwanja wa ndege kijijini kwake chato na uwanja huo unatua ndege moja kwa mwaka tena ya kwake tuu wakati pesa za walipa kodi za kina mama ntilie wamachinga na wengine zikijenga uwanja ule pesa zaidi ya tirioni 1.5 zimetumika

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Aseme alichoahidi mwaka 2015; alichofanikiwa na alichoshindwa. Halafu, aseme atawezaje kutimiza kile alichoshindwa. Wakati huohuo, avumilie 'madongo' ya mpnzani wake uchaguzini Lissu na kujibu kwa kutulia. Ajibu kwa kueleweka. Ajibu kwa hoja za haja. Mwaka huu ni mwaka wake, ni zamu yake katika kukosa cha kushawishi ingawa umati wa wananchi 'hukusanywa' na 'kuandaliwa' kutoa tafsiri ya kukubalika kwake.

💯

Na bado tunae.

Jamaa angu hiyo rangi ya mwandishi unafoka au?
 
Ila mzee anapata hasira kama atakubali mdahalo anaweza shikana mashati adharani!!mh alisha tu win mapema sana,kosa ni kuwabana watu wakakosa pakupumulia avumilie tu hata akishinda abadilike,paka ukijifungia naye chumbani akakosa upenyo wa kupita atakuua
 
Uzuri ni kuwa ndiye raisi 2020 Hadi 2025 , Lissu atarudi ubelgiji kuendelea na maisha yake
Hoja zikikauka huwa mwatia huruma.

Mlideka kwa kuzoea kuzungumza na kusikika wenyewe, peke yenu tu.

Mkawa mnaringia mapampio ya waliookotwa jalalani ambao uhai wao wategemea kujipendekeza.

Matokeo yake mmedumaa kisiasa. '........... Sijui mutamugongea nani..........?' labda wale 100 wa Gamboshi.
 
Back
Top Bottom