Dkt. Magufuli tafadhali vumilia, mwaka huu ni zamu yako. Lowassa alivumilia ingawa aliumia

Dkt. Magufuli tafadhali vumilia, mwaka huu ni zamu yako. Lowassa alivumilia ingawa aliumia

Waliomshauri aongee peke yake kwa miaka mitano hawakufikiri vizuri, haya ndio madhara sasa...alishaongea akamaliza, hoja zingine angeishazijibu kitambo.

Wenzie ndio kwanza wanaanza, hana kipya anaishia kujibu mashambulizi tu!
Niliwahi kuwaambia jamaa zangu wa Lumumba several times kwamba hii ban ya vyama vya upinzani kutofanya siasa itakuja kuwa cost big time during election 2020, wakawa wanadhuhaki kwamba 2020 uchaguzi ni kitonga tuu...
 
Kujenga uwanja wa ndege kijijini kwake chato na uwanja huo unatua ndege moja kwa mwaka tena ya kwake tuu wakati pesa za walipa kodi za kina mama ntilie wamachinga na wengine zikijenga uwanja ule pesa zaidi ya tirioni 1.5 zimetumika

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Ya kuambiwa changanya na zako. Yaani usiwe kasuku. Pole sana.

Kwa taarifa yako, kama hujui, Mkoa wa Geita, ambako Chato ni Wilaya ina Hifadhi za Taifa (Kisiwa cha Rubondo na Burigi) kwa ajili ya Utalii. Watalii wa nje watakuja na ndege zao hadi KIA au JKN na kupanda ATCL hadi Chato pasipo kulazimika kutua MZA.

Isitoshe kila Mkoa kwa sasa unajengewa uwanja wa ndege wenye ubora unaohitajika.

Endelea kusikia na kuamini VIOJA badala ya HOJA
 
Mwaka 2015, aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CHADEMA Edward Lowassa aliteseka sana. Alisemwa vibaya, alikejeliwa, alidhihakiwa, 'alitukanwa' alidhalilishwa na kutwezwa vya kutosha na kutisha. Lowassa alikosa ushawishi katika jukwaa la kampeni. Alikosa maneno ya kuongea. Aliishia kupata kigugumizi na kutoa salamu ya CHADEMA tu. Watu walijaa kwenye mikutano yake lakini hakuwa na cha kuwaambia kilichowavutia. Ulikuwa mwaka wake!

Mwaka huu, CHADEMA wana mgombea (Tundu Lissu) anayejua kusema, kusimanga, kunanga, kujenga hoja, kukera, kutangaza sera, kushawishi na kutupa vijembe. Mwaka huu makombora yanaelekezwa kwa Dkt. Magufuli, mgombea wa CCM. Yanaelekezwa kwake kwakuwa kwa miaka yote mitano ya awamu yake, ni yeye tu ndiye aliyekuwa akitajwa kwenye kila jambo linalohusu Serikali. Sifa zote alipewa yeye. Sasa apokee na kukosolewa yeye mwenyewe.

Mwaka huu, kwa nilivyomfuatilia, Dkt. Magufuli ameishiwa cha kuzungumza. Ameishiwa hoja. Hana jipya kwenye kampeni zake. Sasa imebaki 'kukopi' na 'kupesti' kutoka kwa Lissu. Mfano, jana tu ameahidi Bima ya Afya kwa kila mtanzania. Ni ahadi na sera ya Lissu tangu mwanzo. Nani kampa Dkt. Magufuli sera hii ya kuiga? Nasema, Dkt. Magufuli aseme mambo mapya; si abaki na yale yale na kuyasema vilevile.

Aseme alichoahidi mwaka 2015; alichofanikiwa na alichoshindwa. Halafu, aseme atawezaje kutimiza kile alichoshindwa. Wakati huohuo, avumilie 'madongo' ya mpnzani wake uchaguzini Lissu na kujibu kwa kutulia. Ajibu kwa kueleweka. Ajibu kwa hoja za haja. Mwaka huu ni mwaka wake, ni zamu yake katika kukosa cha kushawishi ingawa umati wa wananchi 'hukusanywa' na 'kuandaliwa' kutoa tafsiri ya kukubalika kwake.

Abadili santuri. Hakuna kipindi redioni au runingani kinachopiga wimbo mmoja tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Shinyanga Mjini)
Rais magufuli hapaswi ā€œkutofokeaā€ inatakiwa arudi kwetu kwa upole na heshima atuambie

ā€ndugu wananchi, mlinipa dhamana ya kuwatumikia, katika KAZI mliyonituma nimefanya kadha wa kadha, kama mmeridhika naombeni mnipe tena ridhaaā€ sio kama anavyofanya ā€œmakasirikoā€ na ā€œkutufokeaā€!
 
Dingilai analala na viatu safari hii na Jana makambako lisu kaongezea tena sukari kwenye asali.

Kampeni zikiisha lazima apelekwe nje akapime sukari, lasivyo kama atafanikiwa kushinda basi tutegemee nchi yetu kuongozwa na rais mwanamke
Magufuli akifanikiwa kushnda , mbinyo mtakaoupata , mtaimba haleluya
 
Usiwalaumu wananchi wakuwalaumu ni NEC na vyombo vya ulinzi na usalama

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa. Balaa lote ni ZEC na NEC. Waulize NEC kwa nini walifuta matokeo ya uchaguzi 1995 kwa mkoa mzima wa DSM? Majimbo yote ya Dar yalikuwa mikononi mwa wapinzani! ZEC nao wakafanya vivyo hivyo kwa Zanzibar nzima. Wakikwambia sababu jua litasimama kama wakati wa Yoshua. Watanzania hawana shida. Wao kama wajumbe! Muulize Mo Raza alivyopata sifuri licha ya kufungua vijiwe vya Wakereketwa Pemba nzima. Kila kijiwe na tv. Ilikujajulikana kwa matokeo ya uchaguzi wa masheha, wawakilishi na wabunge Pemba, kumbe vijiwe vilijaa Wafurukutwa pyu!
 
Kwa kweli kama mitandao ndio inapiga kura sawa, lakini kihuhalisia Mgombea wenu anaishia kupiga kelele tu Hakuna anayemjali bali wajinga wachache humu mitandaoni, subiri sanduku la kura ndio utaijua Tanzania, kama ahuamini kawaulize wajumbe.
Kwa ufinyu wa akili yako Waite wajinga ila utashangaa sana mwaka huu. Hayuko 30% na hiyo mitandao ndiyo itamvusha.

Wewe mwenyewe umelipwa na Hpolepole kuja mtandaoni kupima upepo na kujibu hoja za wakosoaji ba bado ukadharau mitandao. Insane
 
Wahenga walinena Nyani hucheka kundule. Hii inakugusa wewe na wote wanaodhihaki ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato, ambacho matumizi yake ni ya kitaifa.

Kwenye kampeni za huyo mgombea anayedhihaki mgombea mwenzake anatembeza bakuri la ombaomba baada ya viongozi wenzake kutafuna ruzuku. Isitoshe huyo huyo mgombea anatoa ahadi za kutokutoza kodi, lakini kwenye kampeni anatembeza bakuri. Je, viongozi wa aina hiyo ni wa kukabidhiwa HAZINA ya Taifa? VIOJA tupu.
Kwa hiyo bora huyo omba omba ni mzuri kwani anajua hali za wenziwe walivo huko chini tofauti na yule aliye kwapua trilioni 1.5

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Uzuri ni kuwa ndiye raisi 2020 Hadi 2025 , Lissu atarudi ubelgiji kuendelea na maisha yake

Alikwenda Ubelgiji kutibiwa, maana kundi hatari la jiwe lingekatisha maisha yake kwa maelezo ya kuwa shambulio lilikuwa kubwa. Au mna mpango wa kumshambulia tena?
 
Kwa kweli kama mitandao ndio inapiga kura sawa, lakini kihuhalisia Mgombea wenu anaishia kupiga kelele tu Hakuna anayemjali bali wajinga wachache humu mitandaoni, subiri sanduku la kura ndio utaijua Tanzania, kama ahuamini kawaulize wajumbe.
Wajumba ilikua hakuna mtutu wa bunduki pale lkn huku mitaani vovote munavotaka na sisi twataka

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli kama mitandao ndio inapiga kura sawa, lakini kihuhalisia Mgombea wenu anaishia kupiga kelele tu Hakuna anayemjali bali wajinga wachache humu mitandaoni, subiri sanduku la kura ndio utaijua Tanzania, kama ahuamini kawaulize wajumbe.
Sasa huyo mpiga kelele ndio mzuri tofauti na wale mulio wakoto jalalani

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom