Demokrasia ya vita uhasama na chuki inapoteza maana halisi ya neno demokrasia.
Tunashuhudia kipindi cha sasa maeneo mengi yanayochagiza kutekeleza taratibu za demokrasia huku hao wanaoshiriki demokrasia waki umizana kwa vita, mapigano, mauaji, kashfa na maovu mengi yasiyo na staha.
Je hii ndio demokrasia mnayoipigia mbiu ?
Ukweli lazima ubaki kuwa ukweli, Nchi nyingi za dunia ya tatu hazitafsiri maana ya demokrasia ki utekelezaji.
Badala yake demokrasia inaimbwa kwa maneno tu huku wapinzani wa demokrasia wakichukuliana kama maadui wa kudumu. Mahusiano yao yakijikita katika hatua ya juu kabisa ya uadui wa kuchukiana, kusutana na hata kuuana.
Kitendo alichokionesha Halima Mdee kwa Mashinji ni tafsiri halisi ya mahusiano ya washindani wa demokrasia katika ukanda wetu huu.
Ni afadhali Halima ameonesha moyo wake halisi, kuliko mshindani anayekusalimia kwa bashasha na tabasamu ya makumbatino huku akishiriki kikamilifu katika kupanga njama za kukuhujumu au kukuangamiza kabisa.
Kutokana na tafsiri yetu halisi ya Dhana ya Demokrasia Halima amefanya kitendo Sahihi kabisa, hajataka kuwa mnafki kwakuwa kitendo hicho ndicho cha kiungwana kabisa katika mahusiano ya Kiadui, ni kwamba amemuonesha wazi kuwa 'Mimi sio rafiki yako'
Hongera Sana Halima kwa kuivaa ngozi ya Chui kwenye Mwili wa Kondoo. Kuliko ungevaa kinyume chake.
Sent using
Jamii Forums mobile app