Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
Hivi kati ya huyu Marehemu Lamwai na Lissu ni nani ametakata vilivyo katika Nyanja nzima ya Sheria na Uwakili nchini Kwetu?
Bwashee unajua maana ya kudumu!..TL amedumu ktk mageuzi tangu 1994 mpaka leo.
..Dr.Masumbuko alijaribu kwa miaka michache akasalimu amri kwa ccm.
Kwa heri Masumbuko. Tutakukumbuka sana sisi marafiki zako. Tangulia na RIP. Amen.View attachment 1440056
Aliwayewahi kuwa Mbunge wa Ubungo na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 05, 2020.
Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, Mwanasheria nguli na Mkufunzi Mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.
Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi (RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl Nyerere akaingilia kati baada kusimama majukwaani CCM.
Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani.
MDOGO WA MAREHEMU DKT. LAMWAI, MH. JOSEPH SELASINI AZUNGUMZIA KIFO CHA KAKA YAKE
Kupitia mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio asubuhi ya leo, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza hivi:
Dk Lamwai ni kaka yangu. Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya Mzee Roman Selasini na Mama Katarina Roman.
Na kama kiongozi wa familia ametuongoza kwa hekima na busara mpaka mwisho wa uhai wake. Kama mtoto wa kwanza, ametutengenezea misingi mizuri katika familia.
Alikuwa ni mwanasheria aliyebobea katika mwenendo wa mashitaka pamoja na ushahidi (evidence and civil procedures)
MBUNGE PEKEE WA UPINZANI
Katika maisha yake ya kisiasa alipata kuwa diwani wa Manzese mwaka 1995 na baadaye alikuwa ni mbunge wa Ubungo na alikuwa mbunge pekee wa upinzani. Nakumbuka mwaka 1995 Tume ya Uchaguzi ilipofuta uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yeye hakuafiki akaendelea na kumshinda marehemu Venance Ngula wakati huo. Alidumu kwa miaka miwili na baadaye mahakama ikatengua ubunge wake.
Kipindi kilichofuata Mh. Benjamin Mkapa alimteua kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Hiyo ilikuwa baada ya kurejea CCM kutokea NCCR-Mageuzi. Amefariki akiwa ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.
ALIKUWA HODARI, MWENYE MSIMAMO NA USHIRIKIANO
Namfahamu kama mtu hodari, mtu aliyekuwa na misimamo. Mtu ambaye alikuwa akikusudia jambo lake anapambana nalo mpaka ahakikishe limefika mwisho. Ni mtu alikuwa determined kwaakweli.
Alikuwa anashirikiana na watu kufanya jambo. Hata sisi wadogo zake alikuwa akituagiza hasubirii mrejesho, bali munakwenda wote.
Tumepata pengo kubwa katika familia. Tulipotelewa na wazazi na yeye alibaki kuwa kiongozi wetu na sasa ameondoka. Ni pengo ambalo halizibiki.
ALIPENDA KAZI YA UALIMU
Alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alianzisha kampuni yake ya Uwakili inayoitwa Lamwai Advocates. Amefanikiwa kuwasomesha watoto wake wote wanne (4) ambao ni mawakili na wanashughulika na hiyo ofisi yake.
Baada ya kutoka Chuo Kikuu alikuwa ni mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Dar es Salaam. Aliendelea na kazi hizo mbili: Kuendesha kampuni yake pamoja na hiyo ya Uhadhiri.
Kazi ya ualimu aliipenda sana. Ni kazi ya familia. Familia yetu ina wanasiasa wengi sana na walimu wengi. Kwahiyo alipenda sana kusomesha mpaka mwisho wa uhai wake.
AFYA KUDHOOFU NA UMAUTI
Afya yake ilidhoofu katika kipindi cha wiki mbili tatu zilizopita. Lakini pamoja na kudhoofu huko, alipigwa na malaria kali ambayo alikuwa anaendelea kupata dawa.
Hata Jumapili alikaa na watoto wake wakaongea sana ni vile tu hauwezi kujua Mungu amepanga nini. Jana usiku akazidiwa na katika safari ya kumpeleka hospitali, akafia njiani.
Kwa sasa mwili umehifadhiwa Hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.
=====
SOMA: BAADHI YA KESI ALIZOWAHI KUSIMAMIA
Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti - JamiiForums
Mbunge wa Longido Onesmo Nangole (CHADEMA) huenda akavuliwa ubunge kwa kufoji elimu - JamiiForums
Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini - JamiiForums
Kipindi hicho mahakama zilikuwa na uhuru kiasi na siyo kama sasa. Hawa majaji wa sasa sidhani kama wanathubutu kuwa huru kiasi hicho.Nakumbuka Mzee wetu Mkapa aliwahi mlaumu baada ya wabunge wengi wa CCM kushindwa kwenye kesi za uchaguzi ambapo Masumbuko alikuwa wakili upande wa upinzani.
Mkapa alisema" ukiona mtu ambaye kazi yake ni kuwavua wenzake ubunge hafai" akimaanisha Masumbuko Lamwai. Nakumbuka asilimia 99% ya kesi zoote alizosimamia Lamwai alishinda. R.I.P JEMBE
Pengine ni kam Mwigulu nchemba, kukariri madarasa.Kutokana na maelezo ya mbunge wa Rombo mheshimiwa Selasini ya kwamba Masumbuko Lamwai ni Tumbo moja wana share baba na mama.
Je kwanini aliitwa Masumbuko Lamwai bila kutumia Selasini nahisi ndio jina la ukoo wao?
R.I.P mwalimu Masumbuko Lamwai.
Pole kwa familia.View attachment 1440056
Aliwayewahi kuwa Mbunge wa Ubungo na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 05, 2020.
Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, Mwanasheria nguli na Mkufunzi Mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.
Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi (RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl Nyerere akaingilia kati baada kusimama majukwaani CCM.
Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani.
MDOGO WA MAREHEMU DKT. LAMWAI, MH. JOSEPH SELASINI AZUNGUMZIA KIFO CHA KAKA YAKE
Kupitia mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio asubuhi ya leo, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza hivi:
Dk Lamwai ni kaka yangu. Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya Mzee Roman Selasini na Mama Katarina Roman.
Na kama kiongozi wa familia ametuongoza kwa hekima na busara mpaka mwisho wa uhai wake. Kama mtoto wa kwanza, ametutengenezea misingi mizuri katika familia.
Alikuwa ni mwanasheria aliyebobea katika mwenendo wa mashitaka pamoja na ushahidi (evidence and civil procedures)
MBUNGE PEKEE WA UPINZANI
Katika maisha yake ya kisiasa alipata kuwa diwani wa Manzese mwaka 1995 na baadaye alikuwa ni mbunge wa Ubungo na alikuwa mbunge pekee wa upinzani. Nakumbuka mwaka 1995 Tume ya Uchaguzi ilipofuta uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yeye hakuafiki akaendelea na kumshinda marehemu Venance Ngula wakati huo. Alidumu kwa miaka miwili na baadaye mahakama ikatengua ubunge wake.
Kipindi kilichofuata Mh. Benjamin Mkapa alimteua kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Hiyo ilikuwa baada ya kurejea CCM kutokea NCCR-Mageuzi. Amefariki akiwa ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.
ALIKUWA HODARI, MWENYE MSIMAMO NA USHIRIKIANO
Namfahamu kama mtu hodari, mtu aliyekuwa na misimamo. Mtu ambaye alikuwa akikusudia jambo lake anapambana nalo mpaka ahakikishe limefika mwisho. Ni mtu alikuwa determined kwaakweli.
Alikuwa anashirikiana na watu kufanya jambo. Hata sisi wadogo zake alikuwa akituagiza hasubirii mrejesho, bali munakwenda wote.
Tumepata pengo kubwa katika familia. Tulipotelewa na wazazi na yeye alibaki kuwa kiongozi wetu na sasa ameondoka. Ni pengo ambalo halizibiki.
ALIPENDA KAZI YA UALIMU
Alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alianzisha kampuni yake ya Uwakili inayoitwa Lamwai Advocates. Amefanikiwa kuwasomesha watoto wake wote wanne (4) ambao ni mawakili na wanashughulika na hiyo ofisi yake.
Baada ya kutoka Chuo Kikuu alikuwa ni mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Dar es Salaam. Aliendelea na kazi hizo mbili: Kuendesha kampuni yake pamoja na hiyo ya Uhadhiri.
Kazi ya ualimu aliipenda sana. Ni kazi ya familia. Familia yetu ina wanasiasa wengi sana na walimu wengi. Kwahiyo alipenda sana kusomesha mpaka mwisho wa uhai wake.
AFYA KUDHOOFU NA UMAUTI
Afya yake ilidhoofu katika kipindi cha wiki mbili tatu zilizopita. Lakini pamoja na kudhoofu huko, alipigwa na malaria kali ambayo alikuwa anaendelea kupata dawa.
Hata Jumapili alikaa na watoto wake wakaongea sana ni vile tu hauwezi kujua Mungu amepanga nini. Jana usiku akazidiwa na katika safari ya kumpeleka hospitali, akafia njiani.
Kwa sasa mwili umehifadhiwa Hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.
=====
SOMA: BAADHI YA KESI ALIZOWAHI KUSIMAMIA
Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti - JamiiForums
Mbunge wa Longido Onesmo Nangole (CHADEMA) huenda akavuliwa ubunge kwa kufoji elimu - JamiiForums
Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini - JamiiForums
Bwashee unajua maana ya kudumu!
π π π π π π π π..Sawa anko!!!!!!!!Sio 2015 ilikuwa 1995
Jr[emoji769]
Take it easy mzee. Tupo wengi wenye umri mkubwa, lakini inapofika kwenye malumbano, hapo inakuwa kitu kingine.Marahaba, wala hujakosea. Nasikitika kuwa humu JF kuna vitoto vya chekechea vinanitukana. Nami kwa uchungu navirudishia kwa kinyongo kikubwa
Take it easy mzee. Tupo wengi wenye umri mkubwa, lakini inapofika kwenye malumbano, hapo inakuwa kitu kingine.
Lkn ile prominence aliyokuwa nayo enzi hizo akiwa upinzani hakuwa nayo tena. He became a spent force.Alikua mwalim wa sheria chuo cha Tumaini Dar es Salaam

Yeah jamaa alikuwa hata hatumii mic pale lecture thearter 1or 2 lakini alikuwa anasikika hadi njeRIP Lamwai
Wakati anaota Lecture kwenye Jengo la Faculty of Law (wakati huo), ilikuwa mtu unaweza kukaa pale darajani kutokea bookshop na kuchukua notes. Alikuwa ana sauti ya juu kweli kweli.
2015 si juzi tu au umejichanganyawewe kweli ni anko...kama ulipiga kura 2015...wewe ni wasiku nyingi mno..shikamooo anko!