Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Acha kupotosha wewe.. yaani waharibu wengine, lawama umtupie Lamwai? ama kwa sababu Mchaga?Kwangu mimi Lamwai simuoni kama shujaa bali namuona kama msaliti aliyepaswa kufungwa jiwe la chumvi na kutoswa baharini toka zamani sana...
Poleni wafiwa
Kwa sababu ni mchagga ndiyo asiseme anachoona ni sahihi? Acha mihemko ya kiboshoAcha kupotosha wewe.. yaani waharibu wengine, lawama umtupie Lamwai? ama kwa sababu Mchaga?
Sasa kwa akili yako kweli, Masumbuko Lamwai ndo ameifikisha Tanzania hapa? Usinge na wewe mkono hoja za kijinga.Kwa sababu ni mchagga ndiyo asiseme anachoona ni sahihi? Acha mihemko ya kibosho
Kama Kuna mmoja wao alisoma seminary za kikatoliki majina hayawezi fanana,kule unatumia jina la ubatizo na ulilopewa nyumbani,hakuna la ukooKutokana na maelezo ya mbunge wa Rombo mheshimiwa Selasini ya kwamba Masumbuko Lamwai ni Tumbo moja wana share baba na mama.
Je kwanini aliitwa Masumbuko Lamwai bila kutumia Selasini nahisi ndio jina la ukoo wao?
R.I.P mwalimu Masumbuko Lamwai.
Usimlinganishe marehemu Lamwai na Lissu kwenye ulingo wa sheria.Lissu ni mwanasheria populist wakati marehemu Lamwai alikuwa mwanasheria principled. Lissu anaweza kutoa matusi na shutuma bila kuwa na ushahidi wowote wakati Lamwai alikuwa hafanyi hivyo hata siku moja.Hivi kati ya huyu Marehemu Lamwai na Lissu ni nani ametakata vilivyo katika Nyanja nzima ya Sheria na Uwakili nchini Kwetu?
Kuweza kukusaidia tu.Sasa kwa akili yako kweli, Masumbuko Lamwai ndo ameifikisha Tanzania hapa? Usinge na wewe mkono hoja za kijinga.
Shukrani mkuu.Kama Kuna mmoja wao alisoma seminary za kikatoliki majina hayawezi fanana,kule unatumia jina la ubatizo na ulilopewa nyumbani,hakuna la ukoo
Yaishe mkuu.. mimi Lamwai hata simjui.. wala hanihusi.. ko tusigombane kwa mtu asiyetuhusu.. Unaonaje tujadili Forex kidogo?Kwa sababu ni mchagga ndiyo asiseme anachoona ni sahihi? Acha mihemko ya kibosho
Kuweza kukusaidia tu.
Toka mwaka 2000 Masumbuko Lamwai aliachana na siasa za upinzani kisha kuhamia CCM (mwanzoni kimya kimya baadaye rasmi akahamia CCM) huko akawa mwanasheria mwandamizi wa CCM makao makuu, na mshauri wa Rais Mkapa wa masuala mbali mbali ya kisheria. Na mwisho wa siku Lamwai alizawadiwa ubunge wa viti maalum vya Rais Mkapa, na kauli za mwisho mwisho za Lamwai mwaka 2005 akiwa bungeni aliomba bunge lifikirie kubadili Katiba ili mheshimiwa Mkapa aendelee kukaa madarakani hata baada ya miaka 10 ya kikatiba kwisha 2005...
yeah ila inaonesha jinsi gani bunge letu la leo halina watu wanaoweza kujisimamia.. wengi wao ni vibaraka tu!. watu makini hakuna!!......... Kumbe wabunge enzi hizo walikula kiapo cha utii kwa Rais? Anyway, japo kanuni zilibadilishwa, leo hali ni mbaya zaidi kuliko enzi hizo maana mhimili mzima sasa ni full utii kwa ule uliojichimbia zaidi.
. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.1. Ndiye mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada ya udaktari wa Falsafa katika sheria (Criminal and Procedural Law - LLD) Chuo Kikuu Oxford, moja ya vyuo vinavyoheshimika sana duniani.
2. Ndiye mwanafunzi wa kwanza kutoka Afrika kusoma kozi ya miaka minne kwa miaka miwili chuoni hapo. PhD in Criminal &Procedural Law (Oxford) ni miaka minne (full time) na miaka 6 hadi 8 (part time). Lakini Lamwai aliomba kusoma miaka miwili na akahitimu.
3. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa Mhadhiri UDSM alishirikiana na wanaharakati wenzie kuanzisha vuguvugu la kudai mfumo wa vyama vingi.
4. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.
5. Akiwa diwani pekee wa upinzani Manispaa ya Kinondoni aligombea Umeya na kupata kura moja (ya kwake). Alipoulizwa kwanini aligombea wakati alijua hatashinda, alijibu "nisingegombea ningelazimika kumpigia mgombea wa CCM au kuharibu kura. Yote mawili ni makosa. Hivyo niliamua kugombea ili nimpe kura mgombea sahihi"
_
6. Ndiye Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi mkuu 1995.
7. Yeye na Mabere Marando wakiwa bungeni waligomea kiapo cha Utii kwa Rais, kwahoja kuwa wabunge hawapaswi kumtii Rais kwa sababu bunge ni mhimili unaojitegemea. Baada ya mabishano makali ya kisheria, Spika Msekwa alikubaliana na hoja yao. Kiapo cha wabunge kikafanyiwa marekebisho na kuondoa sehemu ya "utii kwa Rais" kisha wabunge wote wakaapa upya.
8. Mwaka 1996 aliongoza kesi maarufu ya uchaguzi iliyomvua ubunge aliyekua Mbunge wa Temeke, Ramadhani Kihiyo kutokana na kughushi taarifa za elimu yake. Mbali na kesi hiyo ameshiriki pia kusimamia kesi mbalimbali nje na ndani ya nchi. Mwaka 2006 alishiriki kuandaa muongozo wa Haki za binadamu kwa nchi za jumuiya ya madola.
9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.
10. Dr.Masumbuko Lamwai ni kaka yake Mhe.Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo). Majina yake kamili ni Dr.Emmanuel Masumbuko Roman Selasini Lamwai.!
PICHANI: Mwanasheria wa Chadema John Mallya akiwa na mwalimu wake Dr.Masumbuko Lamwai (PhD) mwaka 2012 wakati Mallya alipohitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB).!View attachment 1441225
Sent using Jamii Forums mobile app