TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

Kwangu mimi Lamwai simuoni kama shujaa bali namuona kama msaliti aliyepaswa kufungwa jiwe la chumvi na kutoswa baharini toka zamani sana...
Poleni wafiwa
Acha kupotosha wewe.. yaani waharibu wengine, lawama umtupie Lamwai? ama kwa sababu Mchaga?
 
Kwa sababu ni mchagga ndiyo asiseme anachoona ni sahihi? Acha mihemko ya kibosho
Sasa kwa akili yako kweli, Masumbuko Lamwai ndo ameifikisha Tanzania hapa? Usinge na wewe mkono hoja za kijinga.
 
Kutokana na maelezo ya mbunge wa Rombo mheshimiwa Selasini ya kwamba Masumbuko Lamwai ni Tumbo moja wana share baba na mama.

Je kwanini aliitwa Masumbuko Lamwai bila kutumia Selasini nahisi ndio jina la ukoo wao?

R.I.P mwalimu Masumbuko Lamwai.
Kama Kuna mmoja wao alisoma seminary za kikatoliki majina hayawezi fanana,kule unatumia jina la ubatizo na ulilopewa nyumbani,hakuna la ukoo
 
Hivi kati ya huyu Marehemu Lamwai na Lissu ni nani ametakata vilivyo katika Nyanja nzima ya Sheria na Uwakili nchini Kwetu?
Usimlinganishe marehemu Lamwai na Lissu kwenye ulingo wa sheria.Lissu ni mwanasheria populist wakati marehemu Lamwai alikuwa mwanasheria principled. Lissu anaweza kutoa matusi na shutuma bila kuwa na ushahidi wowote wakati Lamwai alikuwa hafanyi hivyo hata siku moja.
 
Sasa kwa akili yako kweli, Masumbuko Lamwai ndo ameifikisha Tanzania hapa? Usinge na wewe mkono hoja za kijinga.
Kuweza kukusaidia tu.
Toka mwaka 2000 Masumbuko Lamwai aliachana na siasa za upinzani kisha kuhamia CCM (mwanzoni kimya kimya baadaye rasmi akahamia CCM) huko akawa mwanasheria mwandamizi wa CCM makao makuu, na mshauri wa Rais Mkapa wa masuala mbali mbali ya kisheria.

Na mwisho wa siku Lamwai alizawadiwa ubunge wa viti maalum vya Rais Mkapa, na kauli za mwisho mwisho za Lamwai mwaka 2005 akiwa bungeni aliomba bunge lifikirie kubadili Katiba ili mheshimiwa Mkapa aendelee kukaa madarakani hata baada ya miaka 10 ya kikatiba kwisha 2005.

Yote kwa yote, sheria nyingi mbovu za kisiasa zilizoletwa bungeni kuanzia kipindi cha mwisho mwisho cha Mkapa, na kipindi cha Kikwete zilitokana na ushauri wa kisheria wa Dr. Masumbuko Lamwai.

Kwa kufupisha maneno hapa na story ndefu, fahamu tu, mchakato mzima wa kuchezea rasimu ya katiba ya Warioba uliokuwa unafanya na CCM ulikuwa unaratibiwa chini ya ushauri wa kisheria kutoka kwa Masumbuko Lamwai. Lamwai ni mtu aliyeaminiwa sana na Mkapa, na kutumiwa sana na Kikwete kisha 'kutupwa' kimtindo na Magufuli.

Ujio wa Magufuli uliua nyota ya ushawishi ya Dr. Lamwai katika CCM na serikali, hapo hapo ukainua nyota ya Profesa Kabudi ndani ya CCM na serikali yake. Miaka michache ijayo, Magufuli atakapoondoka madarakani huenda Profesa Kabudi atarudi kusugua benchi, na siku akilala chini milele, wapo watu kama wewe watakuja kinafiki kumsifia Profesa Kabudo wakati sote tunajua anachokifanya sasa kinalizika taifa la Tanzania.
 
Apumzike kwa amani. 2004 alifafanulia tofauti ya literature in english na english literature wakati akiwa na wanae wawili kichawele hostel majengo secondary, moshi

Pole sana roman kwa kuondokewa na baba yako, my prayers are with you and your family in this hard times
 
Mwaka mbaya huu! tuhifadhi majina ya watu muhimu wanaodondoka mmoja baada ya mwingine
 
Kuweza kukusaidia tu.
Toka mwaka 2000 Masumbuko Lamwai aliachana na siasa za upinzani kisha kuhamia CCM (mwanzoni kimya kimya baadaye rasmi akahamia CCM) huko akawa mwanasheria mwandamizi wa CCM makao makuu, na mshauri wa Rais Mkapa wa masuala mbali mbali ya kisheria. Na mwisho wa siku Lamwai alizawadiwa ubunge wa viti maalum vya Rais Mkapa, na kauli za mwisho mwisho za Lamwai mwaka 2005 akiwa bungeni aliomba bunge lifikirie kubadili Katiba ili mheshimiwa Mkapa aendelee kukaa madarakani hata baada ya miaka 10 ya kikatiba kwisha 2005...

..Mhh!!

..sikumfuatilia sana Dr.Lamwai baada ya kuingia ccm.

..nadhani tatizo la Dr ni kuwa alikuwa mtafuta pesa kabla hajaingia kwenye siasa.

..wapo wanaosema aliipa uzito zaidi biashara yake ya uwakili kuliko kazi za kitaaluma [ kufundisha / utafiti ] , na ndiyo maana akakomea kwenye u-senior lecturer pale faculty of law.

..sasa kwasababu alipenda mno pesa na biashara basi ccm waliweza kumhujumu na hatimaye kumlazimisha kusalimu amri.

..Kuwa mpinzani ni shida sana huku Tanganyika. Vijana wanarubuniwa kwa nafasi za kazi na vyeo mbalimbali. Watu wazima wanahujumiwa biashara zao au ajira zao na hivyo kulazimika kusalimu amri kwa ccm.
 
1. Ndiye mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada ya udaktari wa Falsafa katika sheria (Criminal and Procedural Law - LLD) Chuo Kikuu Oxford, moja ya vyuo vinavyoheshimika sana duniani.

2. Ndiye mwanafunzi wa kwanza kutoka Afrika kusoma kozi ya miaka minne kwa miaka miwili chuoni hapo. PhD in Criminal &Procedural Law (Oxford) ni miaka minne (full time) na miaka 6 hadi 8 (part time). Lakini Lamwai aliomba kusoma miaka miwili na akahitimu.

3. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa Mhadhiri UDSM alishirikiana na wanaharakati wenzie kuanzisha vuguvugu la kudai mfumo wa vyama vingi.

4. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.

5. Akiwa diwani pekee wa upinzani Manispaa ya Kinondoni aligombea Umeya na kupata kura moja (ya kwake). Alipoulizwa kwanini aligombea wakati alijua hatashinda, alijibu "nisingegombea ningelazimika kumpigia mgombea wa CCM au kuharibu kura. Yote mawili ni makosa. Hivyo niliamua kugombea ili nimpe kura mgombea sahihi"
_
6. Ndiye Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi mkuu 1995.

7. Yeye na Mabere Marando wakiwa bungeni waligomea kiapo cha Utii kwa Rais, kwahoja kuwa wabunge hawapaswi kumtii Rais kwa sababu bunge ni mhimili unaojitegemea. Baada ya mabishano makali ya kisheria, Spika Msekwa alikubaliana na hoja yao. Kiapo cha wabunge kikafanyiwa marekebisho na kuondoa sehemu ya "utii kwa Rais" kisha wabunge wote wakaapa upya.

8. Mwaka 1996 aliongoza kesi maarufu ya uchaguzi iliyomvua ubunge aliyekua Mbunge wa Temeke, Ramadhani Kihiyo kutokana na kughushi taarifa za elimu yake. Mbali na kesi hiyo ameshiriki pia kusimamia kesi mbalimbali nje na ndani ya nchi. Mwaka 2006 alishiriki kuandaa muongozo wa Haki za binadamu kwa nchi za jumuiya ya madola.

9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.

10. Dr.Masumbuko Lamwai ni kaka yake Mhe.Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo). Majina yake kamili ni Dr.Emmanuel Masumbuko Roman Selasini Lamwai.!

PICHANI: Mwanasheria wa Chadema John Mallya akiwa na mwalimu wake Dr.Masumbuko Lamwai (PhD) mwaka 2012 wakati Mallya alipohitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB).!
FB_IMG_1588740820498.jpg
 
Sent using Jamii Forums mobile app
 
...... Kumbe wabunge enzi hizo walikula kiapo cha utii kwa Rais? Anyway, japo kanuni zilibadilishwa, leo hali ni mbaya zaidi kuliko enzi hizo maana mhimili mzima sasa ni full utii kwa ule uliojichimbia zaidi.
 
yeah ila inaonesha jinsi gani bunge letu la leo halina watu wanaoweza kujisimamia.. wengi wao ni vibaraka tu!. watu makini hakuna!!...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Ndiye mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada ya udaktari wa Falsafa katika sheria (Criminal and Procedural Law - LLD) Chuo Kikuu Oxford, moja ya vyuo vinavyoheshimika sana duniani.

2. Ndiye mwanafunzi wa kwanza kutoka Afrika kusoma kozi ya miaka minne kwa miaka miwili chuoni hapo. PhD in Criminal &Procedural Law (Oxford) ni miaka minne (full time) na miaka 6 hadi 8 (part time). Lakini Lamwai aliomba kusoma miaka miwili na akahitimu.

3. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa Mhadhiri UDSM alishirikiana na wanaharakati wenzie kuanzisha vuguvugu la kudai mfumo wa vyama vingi.

4. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.

5. Akiwa diwani pekee wa upinzani Manispaa ya Kinondoni aligombea Umeya na kupata kura moja (ya kwake). Alipoulizwa kwanini aligombea wakati alijua hatashinda, alijibu "nisingegombea ningelazimika kumpigia mgombea wa CCM au kuharibu kura. Yote mawili ni makosa. Hivyo niliamua kugombea ili nimpe kura mgombea sahihi"
_
6. Ndiye Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi mkuu 1995.

7. Yeye na Mabere Marando wakiwa bungeni waligomea kiapo cha Utii kwa Rais, kwahoja kuwa wabunge hawapaswi kumtii Rais kwa sababu bunge ni mhimili unaojitegemea. Baada ya mabishano makali ya kisheria, Spika Msekwa alikubaliana na hoja yao. Kiapo cha wabunge kikafanyiwa marekebisho na kuondoa sehemu ya "utii kwa Rais" kisha wabunge wote wakaapa upya.

8. Mwaka 1996 aliongoza kesi maarufu ya uchaguzi iliyomvua ubunge aliyekua Mbunge wa Temeke, Ramadhani Kihiyo kutokana na kughushi taarifa za elimu yake. Mbali na kesi hiyo ameshiriki pia kusimamia kesi mbalimbali nje na ndani ya nchi. Mwaka 2006 alishiriki kuandaa muongozo wa Haki za binadamu kwa nchi za jumuiya ya madola.

9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.

10. Dr.Masumbuko Lamwai ni kaka yake Mhe.Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo). Majina yake kamili ni Dr.Emmanuel Masumbuko Roman Selasini Lamwai.!

PICHANI: Mwanasheria wa Chadema John Mallya akiwa na mwalimu wake Dr.Masumbuko Lamwai (PhD) mwaka 2012 wakati Mallya alipohitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB).!View attachment 1441225

Sent using Jamii Forums mobile app
. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.

Jr[emoji769]
 
Nilikuwa naishi Manzese kipindi anagombea udiwani na ingawa nilikuwa mdogo nina miaka 13 lakini nilikuwa sikosi kwenda kwenye mikutano yake ya kampeni. Alikuwa anachambua hoja mpaka mimi pamoja na kuwa mdogo kipindi hicho nilikuwa namuelewa vizuri. Akimaliza mkutano wa kampeni tulikuwa tunamsindikiza kwa kuimba "Lamwai..Diwani " mpaka Bondeni Bar(ambayo kwa sasa haipo) ambapo ndio ilikuwa kama Centre yake ya kufanya tathimini na wasaidizi wake wa kampeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom