#COVID19 Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia

#COVID19 Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia

Hayo machanjo ni uchafu mtupu acha kujidanganya wewe!

Bibi na babu zetu wameishi miaka kwa miaka hawakudungwa hayo machanjo uchwara lakini walikuwa imara na madhubuti.

Wewe ukiugua kidogo tu unatega makalio unataka kudungwa michanjo ya ajabu ajabu.

MAKINIKA bwana mdogo!
Hujui chochote wala lolote.Unaijua historia ya Ndui?Unaelewa kuwa Babu zetu walichanjwa chanjo ya Ndui?
 
Naibu waziri wa Afya anaefanya Kazi nchi nzima anakuwaje mdogo Kwa mbunge tena wa kijisehemu!!...tuwe tunafikiri wakati mwengine!!...Gwajima ambae amebebwa tu tena na mtu hata chama hakikumpitisha tuwetunafikiria hata kidogo
Gwajima anajua kucheza na wakati,anajua bunge halimgusi linapiga siasa za kutoeleweka vibaya kwa Bishop Gwajima,anajua CCM haitamgusa licha ya kumfokea kwenye vyombo vya habari.
Anajua Waziri wa Afya Dr Gwajima hawezi kumuwajibisha kwa kuwa ameshindwa kupanga mashambuli ya nguvu ya hoja.Pia anajua Raisi SSH hapendi majibizano,na hapendi mikiki.
 
Yaani serikali imeamua kupambana na Mungu kama pharao alivyopambana na Mungu! Ina maana hawajui historia?
Haya endeleeni ila Mungu hashindwi.
 
Unapoona mtu anatembea kifua mbele ujue nyuma yake ana nguvu kubwa
Kwenye siasa usiwaamini watu walio nyuma yako.Gwajima akishushiwa Rungu walio nyuma yake wote watapotea.Wanasiasa wa Tanzania wengi wao sio wasafi hivyo Hakuna ambaye huwa yupo tayari kushindana na mamlaka.Ukiwa mjinga utakubali kutangulizwa mbele.Mambo ya kutangulizwa mbele muulize Fred Mpendazoe,James Lembeli na Lowasa wanajua sana.Usitegemee kabisa mtu anayekutanguliza mbele,mwambie wote muende kwa pamoja sio kutangulizwa mbele
 
Chanjo imefanikiwa kupambana kwa kiwango kikubwa sana na magonjwa hatari ambayo yalitishia kumfuta binadamu katika uso wa dunia kama vile ndui,surua,ebora na kadhalika.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kuziita chanjo kuwa ni uchafu.
Siyo J&J watu wamekufa pamoja kupigwa chanjo. Hata hapa nchi kuna wadosi wamevuta pamoja na kumkimbilia chanjo. Ni Mungu tu atunusuru.
 
Huyo Mollel ni bwana mdogo sana kwa Gwajima na hawezi kumfanya kitu

Mollel katupiga sound
Kweli Gwajima kawaokota wengi,frankly speaking sijui kawapa nini aisee...total brainwash...poleni sana, imebakia awaambie muanze kutafuna nyasi kama yule mwenziwe wa Afrika Kusini.
 
Gwajima anajua kucheza na wakati,anajua bunge halimgusi linapiga siasa za kutoeleweka vibaya kwa Bishop Gwajima,anajua CCM haitamgusa licha ya kumfokea kwenye vyombo vya habari.
Anajua Waziri wa Afya Dr Gwajima hawezi kumuwajibisha kwa kuwa ameshindwa kupanga mashambuli ya nguvu ya hoja.Pia anajua Raisi SSH hapendi majibizano,na hapendi mikiki.
Angekuwa hapendi mikiki Mbowe asingekuwa Ukonga muda huu
 
Siyo J&J watu wamekufa pamoja kupigwa chanjo. Hata hapa nchi kuna wadosi wamevuta pamoja na kumkimbilia chanjo. Ni Mungu tu atunusuru.
Unaelewa maana ya efficacy katika sayansi ya chanjo?Sasa kama efficacy ya chanjo ni asilimia 70 kwa nini baadhi ya watu wasife ambao wamepata chanjo hiyo?
 
Labda babu zenu mabeberu, lakini sio mababu ninaowajua mie.

Kula mizizi, majani, matunda, mambo safiii kabisa.

Sasa nyie kukohoa kidogo tu tayari ushakimbilia kudungwa uchafu.

Mwili haukuumbwa kwa ajili ya machanjo ya ajabu ajabu.

There is a natural mechanism installed by God in the body to fight off diseases!

Kula matunda wewe acha kuhusudu machanjo ya mabeberu hayakusaidii kitu.
Unaongea kama mtu aliechanganyikiwa.Kasome historia ya gonjwa la Ndui.
 
Back
Top Bottom