LGE2024 Dkt. Mollel: Hii sio kodi yenu, ni CCM ndio imeleta hela

LGE2024 Dkt. Mollel: Hii sio kodi yenu, ni CCM ndio imeleta hela

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ccm wanafikirisha sana...wanaishi miaka ya giza,wanaropoka pasi kujua dunia sasa ni kama kijiji...shwaini
 
Msomi yeyote anapoingia katika siasa za CCM lazima level ya usomi wake ishuke by half.
Hiyo Dkt Hana tofauti na certificate holder kwa Sasa. Hana taaluma Wala weledi tena kichwani, kilichobaki ni uchawa na praise and worship
 
Ni kati ya Mawaziri wasioenea kwenye viatu vya maeneo waliopo.
 

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Siha, Dkt. Godwin Mollel akizungumza wakati akiwa katika kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhamasisha Wananchi wa jimbo hilo kuhusu umuhimu wa kuchagua wagombea wa nafasi za uenyekiti wa mitaa kupitia chama hicho.

Hamna anaetaka hisani!
Tunataka matumizi ya kodi zetu, pesa zako kale na mkeo!
 
huyu braza anazingua sana, akicheza mwakani atapoteza jimbo la siha. bora hata AD. Mwanri arudi.
 
KAULI ya Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Jimbo la Siha,Dkt .Godwin Molllel kwamba fedha za maendeleo zinazotolewa na serikali hazitokani na Kodi za wananchi bali ni fedha za chama Cha Mapinduzi (ccm),imeonekana kuwachefua wananchi wengi.

Mollel anasikika kwenye video inayozunguka mitandaoni akiwaeleza wananchi wa Jimbo la Siha kuwa fedha za maendeleo hazitokani na Kodi zao.

Alikuwa akihutubia kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi A
za uenyekiti wa vijiji na vitongoji kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mapema jumatano wiki hii .

"Sasa ngoja niwaeleze,eti watu wanasema hii ni Kodi yenu,eti wanasema ni hela ya serikali,hakuna cha Hela ya serikali hapa"
"Ni mbunge wa Chama cha Mapinduzi ,Rais wa Chama Cha Mapinduzi,madiwani wa Chama cha mapinduzi na wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi tumeenda kutafuta Hela tukazipata tukazileta",amesikika Mollel.

Baada ya video hiyo kusambaa ,wananchi wamepaza sauti na kuitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi hayo wakidai yanaichafua serikali .

"Hivi hii kauli ilistahili kutolewa na mtu mwenye hadhi kama Naibu Waziri kwamba Kodi zinazotolewa na wananchi haziendi kufanya shughuli za maendeleo kweli au amechanganyikiwa?"amehoji Mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mwananchi huyo amesema kuwa kwa uelewa wake chama Cha Mapinduzi (ccm) na vyama vingine vya siasa vyenye wabunge hupata ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya uendshaji wa shughuli za vyama vyao na si vinginevyo.

"Mimi kwa uelewa wangu mdogo,fedha za maendeleo zinapitishwa na bunge wakati wa kikao cha bunge la bajeti na si vinginevyo"amesema Mwananchi huyo .
 
Back
Top Bottom