Dkt. Mpango: Mkandarasi wa Bwawa la Nyerere hana Uzoefu, pia mradi upo nyuma ya muda

Nilipitia miradi ya mabwawa mengine Kama Ethiopia na Egypt nikawa najiuliza hili letu Labda Kama limetengenezwa kiwandani ni la kufitisha tu hapo mtoni.
Time frame Ilikuwa ya uongo mkubwa
 
13 October 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango Octoba 12, 2021 atembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP / Stiegler Gorge Rufiji
Source : Millard ayo


N.B
Ni kweli kwa kutazama hata kwa macho inaonesha wazi kuwa bwawa la mradi wa JNHPP haliwezi kujazwa mwezi November 2021 kama alivyosema Dr. Medard Kalemani mbunge wa Chato ambaye alipata kuwa waziri wa Nishati ktk serikali ya Rais John Pombe Magufuli.

Na makamu wa Rais Phillip I. Mpango ametupa sababu hasa ya mradi kuwa nyuma ya wakati uliopangwa kukamilika hatua kwa hatua.
 

Mungu atusaidie kama taifa. Mh Makamu wa Rais awambie Watanzania serikali inachukua hatua gani kuzuia hizi fedha za kodi zinazolipia mkopo wa hili bwawa la Nyerere kuhakikisha haziendi tena kumlipa huyu mkandarasi asiye na uzoefu kuepuka kuendeleza madudu ya serikali ya awamu ya tano. Kiongozi anatoa kauli ambazo akimaliza tu kutamka zinageuka kuanza kumuwinda.
 
VP yupo sahihi. Mara nyingi una outsource kazi ambazo wewe mwenyewe huwezi kuzifanya kwa ufanisi au faida kwa sababu yoyote ile. Unafanya kile unachoweza au ambacho kwacho you are the best. Kwa hivyo kama Arab Contractors ame outsource kazi zote maana yake ni kuwa yeye asingeweza au hawezi kufanya kazi husika kwa ufanisi mkubwa (na faida) kwa hapa Tz kuliko hao subcontractors.....ama?
 
Lakini nawaza pia bado kuna uwezekano baada ya JPM kufariki ndo wameanza kufanya huu upuuzi ili kumfanya jiwe aonekane alikua anatudanganya ili wao ndo waonekane bora zaidi wkt kuna uwezekano sio kweli.
 
Reactions: Ame
Ndugu acha Kudanganya watu. Miradi mikubwa kama hii lazima kuwe na Consultant ambaye huwa ni Designer na Main supervisor wa Project husika. Labda
Ututhibitishie kuwa huo mradi wa Umeme Contractor ndio pia Designer wa hiyo Project..
 

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AITAKA TANESCO KUONGEZA NGUVU KATIKA UTEKELEZAJI.



13 Oct 2021

MRADI WA JNHPP / RUFIJI STIEGLER'S GORGE, MKANDARASI ALALAMIKA TANESCO KUWAPATIA 33KV BADALA YA 220 KV KUENDESHA MITAMBO YA UJENZI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameitaka wizara ya Nishati kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mradi wa kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere unakamilika kwa wakati.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere ambapo amesema ni muhimu wizara ya Nishati kupitia shirika la umeme nchini (Tanesco) kuimarisha usimamizi, kuongeza wataalam sehemu zenye upungufu pamoja na kuongeza umeme utakaoendesha vema mitambo ya mkandarasi wakati huu wa ujenzi wa mradi
Source : Fullshangwe tv
 
Why using the word Architecture? Kwamba Designer wa project yoyote ile anaitwa kwa hilo jina? Ule mradi unahusisha multiple Disciplines! Electrical, Civil, Mechanical Engineering, Environmental etc...wote ni Architecturals??
 
Siku zote lazima apatikane mtu wa kupewa lawama watalaam humuita scapegoat na serikali haiwezi kubali kuwa scapegoat tena hususani nyakati nyeti kama izi yenyewe inabidi isimame kama sterling wa muvi
 
Arab contractor imeanzishwa kabla makamu hajazaliwa.. na kabla Tanzania haijazaliwa arab contractors ipo duniani.. na imejenga Aswan dam na mabwawa kibao.. ila leo tunaambiwa hawana uzoefu

Mambo ya ajabu sana haya. Na sababu kama sijakosea kuwa na subcontractors wengi ikikuwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi, Hayati alisema mahali. Lakini ukisikiliza hotuba za Mh huyu pale JNIA, kwenye uapisho wa wateule juzi Dodoma, kuna siku nyuma kidogo alisahau jukumu la kumkaribisha Mh Rais akaongea aliyo ya ongea akasepa ili bidi akumbushwe na msimamizi wa shughuli. Hatimaye unakuta yako maswali mengi ya kujiuliza kuliko majibu. Mh Mpango wakati ni Waziri wa Fedha akishuka nondo za nguvu na kwa kutulia mpaka unakubali mnyewe. Sijui nini kinamnyemelea? Takwimu za waliochanjwa hazijatolewa muda sasa.
 
Isije ikawa Manyanga construction ndio walipewa tenda na mwendazake
 
Baba zima lina ramba sikonkiko za mtu na lenywe lilikuw linatoa pesa leo lina ropoka kma toto dgo
 
Ndugu acha Kudanganya watu. Miradi mikubwa kama hii lazima kuwe na Consultant ambaye huwa ni Designer na Main supervisor wa Project husika. Labda
Ututhibitishie kuwa huo mradi wa Umeme Contractor ndio pia Designer wa hiyo Project..
Nani aliye design huo mradi?
 
Nimekusoma vizuri tu, mara ya mwisho Leo tu himu ukidhihaki ukweli wa maumivu ya wengine ukiyaita delusions za Twitter na JF. Kama kuna anayekuamini humu mwambie nina daraja aje nimuuzie
 
Why using the word Architecture? Kwamba Designer wa project yoyote ile anaitwa kwa hilo jina? Ule mradi unahusisha multiple Disciplines! Electrical, Civil, Mechanical Engineering, Environmental etc...wote ni Architecturals??
What does an architecture do?
 
Nimekusoma vizuri tu, mara ya mwisho Leo tu himu ukidhihaki ukweli wa maumivu ya wengine ukiyaita delusions za Twitter na JF. Kama kuna anayekuamini humu mwambie nina daraja aje nimuuzie
Kama sijakuelewa vile unauza madaraja, sitaki hata kujua unapohifadhi hizo inventory zako.

Au unataka discussion za realistic energy investment, maana hiyo ndio ilikuwa sababu ya kusema kule Twitter wana mijadala delusional.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…