Dkt. Mpango: Mkandarasi wa Bwawa la Nyerere hana Uzoefu, pia mradi upo nyuma ya muda

Halafu kuna watu wanalaumu humu why Kalemani kaondolewa, mara oh ni mzalendo, mara oh umeme enzi zake ulikuwa haukatiki (ulikuwa unakatika sana tu ila hakuna aliyedhubutu kulisema hilo, ilikuwa ukisema unashughulikiwa), kuwa MLUGALUGA haina maana wewe ni MZALENDO, and KUWA MTOTO WA MJINI, EXPOSED, WITH MANY CONNECTIONS haina maana wewe ni MPIGAJI!
 
Kuweka sub contractor ni moja ya njia za kutekeleza miradi mikubwa kimataifa wala si kosa.
Mradi wa Mwenge/Moroko mkandarasi Mjapani NIPPO Construction, sub contractor MAC , mkandarasi mzalendo.
Na Tanroads huwa inaafiki kama mpango huo.
 
Nakubali, nchi ina viongozi wa hovyo sana.
 
Nakubali, nchi ina viongozi wa hovyo sana.
Power is the ability to make someone do something otherwise he wouldn’t do.

Ndio njaa aliyoenyesha Dr Mpango kwa maelezo yake ya jumla jumla kwa akili za kawaida tu mradi kama huo una ‘project structure’ yake kujua nani ana majukumu gani, OBS kujua usimamizi wake, RAM kusaidia flow of information mpaka kwa raisi mwenyewe.

Sasa kusikiliza kiongozi anaporoka mpaka wewe raia ndio unaona aibu; hata sijui hilo swala unaliweka wapi.

Njaa ndio silaha inayotumiwa sana nchi yetu kuwanyamazisha viongozi wenye kuhoji hasa wabunge.

Mfano Ndugai anapenda kuwapiga mikwara sana wabunge kama alivyomtisha Jerry Slaa. Ya kuwa kanuni karibu zote zinamtaja yeye kama muamuzi bungeni na yupo kwenye kamati kuu ya CCM kwenye mchujo wa wabunge.

Maana yake wabunge wasiende njee ya mitazamo yake na wasihoji asiyoyapenda what an idiot.

Binafsi kama vile naanza kukubali yaishe; hii vita ni kati ya wazalendo na mafisadi ndani ya vyombo vyetu vya usalama.

Bila ya backup ya upande ni kujiweka in the middle of firing squads.

Nonetheless aina maana ntaacha kusemea maslahi yangu what CCM does and opposition struggle is not my problem (let’s face as yet hakuna mbadala wa CCM pamoja na mapungufu yao).

Good Morning 👋
 
Ndo tumeshapigwa hiyo, na saa hizi bei za material zimeshapaa na usafirishaji umekuwa mgumu.......ilikuwaje msimpe mchina moja kwa moja ambaye anao utaalamu?
 
Tunawaachia watoto wa TZurithi gani? kila miradi haina ukweli mtoto toka anaanza kusoma mpaka anamaliza anasikia miradi hewa matamko yanayo kinzani kati ya viongozi nae akiingia humo anakuwa kafisadi mpaka akikomaa anakuwa li papa kabilaaa.
 
Mpango ameropoka tuu ... sub contractor ndio njia rahisi ya kuharakisha kumaliza mradi....hatutegemei mkandarasi mkuu kufanya kazi zote.... mimi nafikiri Mpango si mtu sahihi kuongelea huu mradi inaonekana hajui lolote kabisa kuhusu miradi.... yani anafikiri mtu akipewa mradi basi afanye kila kitu... sasa mradi si utachukua miaka kumi kuisha?

Mimi nafikiri Mpango ametujulisha mpango wa kusitisha huu mradi ambao ulikuwa unapingwa muda sana......... yani haingii akilini eti Arab Contractor hawana uzoefu......
Mpango wa kusitisha huu mradi na kubinafsisha Tanesco umepamba moto.
 
Na hilo ndio leongo Lao kuuu halafu hyu si alikuwa waziri wa fedha mbona mdomo wake ni mchafu kma dampo katumwa huyu si bule na wanataka kuhararisha dhambi yao
 
Unauhakika kati ya hao wawili Kalemani ndio amekudanganya?
Hicho nacho ni cha kuuliza. Wewe kama unamwamini Kalemani, subiri mwezi ujao bwawa lianze kujazwa maji.

Watendaji wengi, pamoja na mawaziri na Rais mwenyewe, wakati wa awamu ya 5, walizoea kuoongea uwongo. Katika mambo makubwa, hakuna hata moja ambalo lilikuwa la kweli. It was a good government fir the fools:

1) Dhahabu tunaibiwa nyingi sana, tunadai kodi ya dola billion 190 - uwongo

2) Makinikia kwenye makonteina, 90% ni dhahabu - uwongo

3) SGR itaanza kufanya kazi mwezi wa November 2020 - uwongo

4) Trump amepongeza utendaji kazi wa Rais Magufuli - uwongo

5) Serikali ina pesa za kutosha, tunajenga miradi yote kwa pesa zetu - uwongo

6) Uchaguzi wa 2020 utakuwa huru na wa haki - uwongo

7) Wanavyuo wote watapewa mikopo - uwongo

8) Wafanyakazi tutawaongezea mishahara, siyo ongezeko dogo kama mlivyozoea - uwongo

9) Kuna mtu kila saa moja alikuwa anaiba shilingi milioni 7 - uwongo

10) Gas wamechukua wachina - uwongo

11) Ujenzi wa bwawa la Nyerete umefikia 70% - uwongo

12) Ndege zimeingiza faida ya shilingi bilioni 17 - uwongo

13) Watanzania tembeeni vifua mbele, uchumi wetu upo pazuri - uwongo

Waliozoea kuishi katika uwongo, hawawezi kubadilika ghafla na kuwa wakweli.
 
Kunazingine ni bangi we unamhukum kalemani kwan bado ni waziri?
Aliyekuwa waziri wa fedha kipind cha uchum wa kati ni nan?
 
Mkadarasi wakati anapewa tenda Mpango alikuwepo na alishiriki, hawa watawala wetu kwa maigizo hawajambo
 
Huko kumejaa matapeli tupu
 
Hiyo kauli kuwa mkandarasi hana uwezo wa mradi mkubwa kama huo, iliwahi kutamkwa hata wakati mwendazake akiwa hai.

Huo ndiyo ukweli ambao wanafiki wamekuwa waoga kuutamka. Hata angekuwepo marehemu, kamwe mradi huo na mingine mikubwa yote, hakuna ambao ungemalizika kwa wakati kwa sababu mbalimbali. Uliambiwa treni ya kisasa ingeanza safari kati ya Dar - Morogoro mwezi November 2020, je, ilianza? Marehemu si alikuwa bado hai?
 
Huu mradi ni bomu litalokuja kulipuka huko mbeleni.

Haya ni madhara ya mtu mmoja kuaamua kila kitu huku akipigiwa makofi na mazuzu.

Haya yangesemwa na wapinzani wangeshambuliwa vibaya sana na hata kukamatwa au kufanyiwa hujuma.
Ndiyo shida ya kuwa na katiba mbovu ambayo inampa mamlaka makubwa sn mtu mmoja
 
Alikwishaondolewa. Kalemani alikuwa na tofauti ndogo sana na mpiga sound wa cherehani 3 ni viwanda.
 
Kuna mtu alikuwa na uwezo wa kueleza ukweli, kama marehemu alikuwa hataki, wakati wa awakubya 5?

Humu JF ilikwishawahi kuletwa hiyo habari kuwa Mkandarasi alikuwa hana uwezo.

Wewe si ulikuwa unaambiwa ATCL ilikuwa inapata faida, ilikuwa inapata faida?
 
Wewe ni mpuuzi kweli. Wataalam walikwishaeleza tangu marehemu akiwa hai kuwa mkandarasi alikuwa hana uwezo wa kujenga mradi mkubwa kama huo, na alikuwa hajawahi kufanya mradi wa kiwango hicho.

Sub-cobtractors ni sahihi huwa wanatumika lakini siyo kwa kazi zote. Core activity inatakiwa kufanywa na contractor mwenyewe, na siyo sub-contractor. Usiwadanganye wajinga wa masuala haya ya miradi mikubwa.
 
Hayo maneno ya Makamu wa Rais yanaweza Leta shida ya kidiplomasia na watu wa Misri, hawatapenda kuzaraulika
Hata marehemu alikuwa anajua, aliambiwa. Lakini kwa vile alikuwa anahofia ukosoaji, aliamua kukaa kimya. Hii siyo taarifa mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…