Dkt. Mpango ni kweli ulishiriki kumtuma Sabaya kufanya mambo machafu?

Afungwe kivipi wakati hakuna ushahidi wa kutosha kumfunga!? Labda Mpango aje Mahakamani aseme hawajawai kumtuma Sabaya kufanya kazi maalumu ya kuwasaka wahujumu Uchumi!!
Aliyemtuma ni JPM (mamlaka ya uteuzi), sio Mpango. Mpango alijua tu.

Swali kubwa: alitumwa kama undercover agent (mtu asiyejulikana) au kama DC? Mbona alikuwa akijinasibu sana kwenye misheni hizo? Hakuwa professional kabisa.

Ajiandae kurukwa na kuangushiwa jumba bovu na hao “wanaojua”. Aliyemtuma ndio hivyo tena. The dead tell no tales. Ni kawaida katika nchi zetu hizi wakubwa kutafuta watu wenye viherehere na kuwapa kazi chafu halafu kuwasakizia mbwa wasipohitajika tena ili wasije wakawa-contaminate. He is expendable.

Sabaya angekuwa smart angejua ile kufutiwa kesi ya kujifanya TISS na kupewa ukuu wa wilaya halafu kuanza kutumwatumwa ovyo tayari wajanja walishamfanya kifaa cha kufanyia kazi chafu. Angeenenda kwa tahadhari sana. Halafu anajua kazi yenyewe alirithishwa na nani. Mwenzake saa hizi anajifanya kama hakuwa yeye ingawa amechafuka kupita maelezo.
 
Jambazi ameamua kuweka wazi kuwa huu ujambazi aliofanya Arusha alikua anashirikiana na Magufuli na Mpango full stop.
 
Mpango ajiuzulu haraka sana , ukiona kiongozi anajifanya Mcha Mungu huku kazungukwa na matunguli muogope sana
Kiufupi mtu yeyote anayejifanya mcha Mungu sana muogope kama ukoma,mara nyingi huwa ni watu hatari sana
 
Hiyu ana akili za kitoto sana.kesi hii sidhani kama ni ya kunyongwa.sasa anapowataja wakuu wa nchi ni dhahiri hakuwa jasusi .Kama kweli alitumwa sidhani kama alitumwa kufanya uhalifu.Amejiharibia kupita kawaida
 
Amiri jeshi mkuu Ana vyombo rasmi vya kutekeleza jukumu hilo. Kuna vilivyo juu ya meza (overt) na viliyo chini ya meza (covert) na vyote vina wateule wake.

Jiulize, alimpaje kazi hiyo DC Sabaya mtu mwenye weledi haba na kelele nyingi za kujinasibu? Kwa kifupi ni game over kwake.
 
Mleta uzi amezungumzia kuwa kama ni kweli Mpango amefanya madudu haya ajitokeze na ajisafishe ila wewe unasema kuwa kama ni kweli Mpango amefanya madudu haya ajitokeze awajibike.Huoni kuwa hizi ni sentensi mbili tofauti ambazo zimebeba jumbe mbili tofauti?(Hapa tunazungumzia upande mmoja wa Mpango kukubali tuhama pekee)
 
Uko sahihi. Mada inataka kujua kama Dr pango alijua au hata kushiriki, na kama alishiriki basi ameharivu CV yake. Kama hakushirikia ajitokese akanushe. Ili kulinda heshima yake tunayompa sisi tunaompenda
 
Wanahusishwa kwasababu wanajua, sasa ili mambi yawe safi wayatolee ufafanuzi haya.
Ni rahisi tu Wajitokeze wasema aliyofanya Sabaya wao hawakufahamu kwa namna yoyote. Hata kama hawakumtuma ila kama walifahamu kinachoendelea kikaendelea maana yake walikibariki.
 
Swadakta kabisa. Hii ndio lengo la uzi huu.
 
umekubali na umepinga nini? Ugumu wa kuelewa uko wapi? inaonekana wewe ndiye mgumu wa kuelewa
 
Sasa ametajwa vipi huko mahakamani? kumbuka ile ni kesi ya Uhalifu. Kiongozi wa umma kutajwa tu maana yake kuna association ya namna fulani. Hili ni doa.
 
Hizi operation zinahitaj watu wenye uvumilivu...sabaya mwez mmoja jela kashaanza kutaja? Akibinywa mbupu si fasta tu anatoa siri zote
 
Hakuna viongozi wa dini. Hapo kuna wafanyankazi wanaotafutia tumbo kama ilivyo kwa Mwalimu, Daktari, Polisi, Mwanajeshi, Mkulima na mjasiriamali. You should not expect anything than that.
 
Huenda wanasheria wake uchwara wameona ndio namna ya kuchomoka. Lakini pia inaonekana ameanza kutapa tapa. Anaona waliomtuma wamemtelekeza.
 
Ktk mpira sabaya akifungwa inakuwa ni mbinu ya kutafuta kumpiga miaka mbowe.. Tunaita equalisation la sivyo kuna upande utajipanga kwa maangamizi makali zaidi na bibi atajuta in the end
Asante kwa kuliona hilo. Hapo wanataka kutuaminisha kuwa mahakama na polisi wanacheza fair.

Hili la Mbowe litawatoka puani. Tujipe muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…