Dkt. Mpango: Vijana achaneni na kupenda mashangazi

Wakuu mmesikia huko alichokisema Dkt. Mpango kuhusu Mashangazi?

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philiph Mpango, amesema zinahitajika tafiti za kina pamoja na mikakati katika kufanya mapinduzi ya kitamaduni kubadili tabia na mazoea yasiyofaa yanayojitokeza katika Jamii hivi sasa ambayo ni kikwazo kwa maendeleo.
Wazee hamtaki kung'atuka huko serikalini hadi kwenye chama mnataka vijana wawe wakabaji ? Ngoja watumie fursa ya kuruka na mishangazi ili maisha yasonge mbele.
 
Wakuu mmesikia huko alichokisema Dkt. Mpango kuhusu Mashangazi?

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philiph Mpango, amesema zinahitajika tafiti za kina pamoja na mikakati katika kufanya mapinduzi ya kitamaduni kubadili tabia na mazoea yasiyofaa yanayojitokeza katika Jamii hivi sasa ambayo ni kikwazo kwa maendeleo.

Dkt Mpango amesema hayo wakati akifungua mkutano wa kusherehekea miaka 30 ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) uliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo ametaja baadhi ya mazoea na tabia hizo ni pamoja na kutojali muda, kutokuwa na uaminifu mahali pa kazi pamoja na kutumia njia zisizofaa katika kupata kipato.

Makamu wa Rais ameitaka ESRF pamoja na Watalaam wa Fikra Tunduizi (Think Tank) kuangazia pia tabia za hivi karibuni za Vijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wanawake waliyowazidi umri (Mashangazi) kama njia rahisi ya kujikimu, kutumia muda mwingi bila kufanya kazi kwa kushinda Vijiweni, uchezaji kamari, utupaji taka ovyo, uchomaji moto ovyo wa nyasi na misitu pamoja na ubinafsi.

Pia Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuangazia tabia nyingine kama vile matumizi makubwa ya fedha katika anasa kuliko kuweka akiba ikiwemo uchangiaji zaidi katika matukio ya sherehe na tafrija kuliko kusaidia gharama za elimu na matibabu kwa familia za kipato cha chini.
Soma: Kuhusu utafiti wa tatizo la ajira, Dkt. Mpango usihadae Watanzania
Nimekasirika sana.
 
Kizazi cha Kupenda Mteremko, kupenda Kitonga, Kupenda utelezi..!

Kizazi kipo bize Kubet..! Kufanya Kazi aaah..

Vizazi vya late 90's 2000's havijapata benefits ya vilivyotangulia.

Enzi za Dr Mpango, viongozi wengi ukimaliza form 4, 6, chuo, unapata kazi ya uhakika kwa maisha. Pia walikuwa na ukoo, jamii, wazazi wawili wanawaangalia.

Namshauri Makamu wa Rais aangalie vyanzo vya vijana kukengeuka
Namsaidia ni familia kuvunjika, ukoo, jamii kutojali, mitandao ya kijamii kuruhusu maudhui mabovu, wahuni wa kila aina ndio role models. Australia hawaruhusu watoto kupewa simu janja mpaka wakifishe miaka 14.
 
Duh! Hadi makamu anajua kuna mashangazi, hii kali! Mashangazi yana hela, vijana wanaona bora wayakimbilie kuliko kung'ang'ana na vibinti vyenye njaa kali na vidangaji ni visumbufu kutwa kutaka hela na hela zenyewe hakuna. Mashangazi nayo yanawapenda vijana kwa kupeleka moto wa uhakika mwanzo hadi mwisho hadi lishangazi liseme lenyewe imetosha
Shida ya mashangazi ni kutodumu nalo kwa muda mrefu!!! Halafu likiamua linakupiga chini na huna Cha kufanya 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wakuu mmesikia huko alichokisema Dkt. Mpango kuhusu Mashangazi?

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philiph Mpango, amesema zinahitajika tafiti za kina pamoja na mikakati katika kufanya mapinduzi ya kitamaduni kubadili tabia na mazoea yasiyofaa yanayojitokeza katika Jamii hivi sasa ambayo ni kikwazo kwa maendeleo.

Dkt Mpango amesema hayo wakati akifungua mkutano wa kusherehekea miaka 30 ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) uliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo ametaja baadhi ya mazoea na tabia hizo ni pamoja na kutojali muda, kutokuwa na uaminifu mahali pa kazi pamoja na kutumia njia zisizofaa katika kupata kipato.

Makamu wa Rais ameitaka ESRF pamoja na Watalaam wa Fikra Tunduizi (Think Tank) kuangazia pia tabia za hivi karibuni za Vijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wanawake waliyowazidi umri (Mashangazi) kama njia rahisi ya kujikimu, kutumia muda mwingi bila kufanya kazi kwa kushinda Vijiweni, uchezaji kamari, utupaji taka ovyo, uchomaji moto ovyo wa nyasi na misitu pamoja na ubinafsi.

Pia Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuangazia tabia nyingine kama vile matumizi makubwa ya fedha katika anasa kuliko kuweka akiba ikiwemo uchangiaji zaidi katika matukio ya sherehe na tafrija kuliko kusaidia gharama za elimu na matibabu kwa familia za kipato cha chini.
Soma: Kuhusu utafiti wa tatizo la ajira, Dkt. Mpango usihadae Watanzania
Huyu naye akaage kimya tu, bora kipi vijana wajiegeshe kwa mashangazi au wajiegesha kwa Pdidy?
 
Back
Top Bottom