Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

Akichambua Ripoti ya CAG, Dr Msukuma Mbunge wa Geita vijijini amemlaumu Godwin Kunambi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza miradi inayoleta hasara.

Dkt. Msukuma amesema Ujenzi wa Hotel ya nyota 5 ni ubabaishaji mtupu.

Ujenzi wa Soko la Ndugai hauna tija na Fedha iliyowekezwa pale haitarudi.

Ujenzi wa Stendi za Mabasi ya mikoani ni ufisadi mtupu ukiondoa chache za miji mikubwa amesema Msukuma

Kuna haja gani ya Law School kuwepo wakati katika Wanafunzi 700 wanayofanya mtihani kila Mwaka wanafaulu 26 tu amehoji Dokta.

Inawezekana CAG naye huwa anapokea mlungula kwa sababu ziko Halmashauri bobezi kwa ufisadi lakini zimepewa Hati Safi, amesisitiza Daktari wa Heshima

Mwisho Dkt. Msukuma ameshauri utaratibu wa kuwapata Wakurugenzi wa Halmashauri ubadilishwe badala ya kuteuliwa wawe wanaomba kazi kwa kushindanishwa.

Chanzo: TBC
Watu wa aina hii tunao toka uhuru. Kina Msukuma. Ndio maana hakuna plan A na B kwenye mambo ya huduma zetu kwa jamii.
Ukijaribu kujenga bwawa la kuweka maji, watasema unapoteza hela za walipa kodi. Kisicho ulizwa ni hela ya kujikimu tu. Sio mambo ya maendeleo
 
Unalinganisha upanukani wa Dsm na Dodoma?
Ni miaka 5 toka Serikali ihamie huko ila upanukaji wa mji ni mdogo mno
Tusiache long term plans sababu ya wasomi waliotukuka kama kina msukuma
 
Miradi mingi ya Dodoma haitakuja zalisha kutokana na aina ya wananchi wa Dodoma

Treni ya SGR ikimamilika ndo mtaamini Dodoma itapoteza watu kila weekend maana watakuwa na uhakika wa kurudi mapema.

Haya masaa 10 njiani hukera watu, treni ikitumia masaa 4 hadi Dodoma watu watakaa Dsm
Nafikiri hiyo treni ya sgr haitakuwa na ufanisi unaoutarajia. Mfano kidogo ni atcl, licha ya kuwa na ndege mpya lakini kutokana huduma mbovu, watu wanaona bora wapande basi
 
Miradi mingi ya Dodoma haitakuja zalisha kutokana na aina ya wananchi wa Dodoma

Treni ya SGR ikimamilika ndo mtaamini Dodoma itapoteza watu kila weekend maana watakuwa na uhakika wa kurudi mapema.

Haya masaa 10 njiani hukera watu, treni ikitumia masaa 4 hadi Dodoma watu watakaa Dsm
Dodoma haihitaji stand zisizo na faida. Kumlaumu Kunambi siyo sahihii kabisa,yupo au wapo waliojivika umungu wa maamuzi ya nchi.Kunambi alikuwa anatekeleza matakwa yao.
Na si Dodoma tu,stendi nyingi zimejengwa mbali na sehemu iliyotakiwa kujengwa,na wakati mwingine ni kubwa kuliko mahitaji.
 
Hivi ukilaumu ujenzi wa stand kubwa kama ile ya Dodoma ina maana utapinga pia ujenzi wa barabra ya njia 6 kule Dar, maana hesabu ya ujenzi wake inapigia miaka takribani 10 au 20 mbele, AU hata ile aiport terminal 3 kule Dar mbona bado sehemu kubwa tu haijaweza kutumika,ni kwa sababu ya hesabu za mbali,ni kweli tunalaumu sasa hivi lakini manufaa yake tutayaona baadaye sana.
Ujue nn viongoz WetU awa wanafki sana Amin kwamba ni Bora ukaetengeza Kitu kikubwa baaadae kilete manufaaa kuliko kidgo baaadae mmbomoe mtengeneze Tena wanafki sana awa jamaaa
 
Yani nataman Sana izi Bara bara za mwendo Kasi zingekuwa ata three way kwend na Kurud ila ndio Ivyo viongoz wanatakiwa kutengeneza Kitu miaka 30 Mbele stand ya Dodoma ukubwa wake Sio tija Bali imeengalia idadi ya matumiz apo baaadae na Iyo hotel ni sawa maaan Dodoma ndio mji mkuuu na wagen kibao watamiminika
 
Hivi tatizo ni nini hasa?

Maana hao 26 utakuta ni wa mchongo
Tatizo ni maslahi, LST inajiendesha kwa ada inazokusanya kutoka kwa wanafunzi. Kwa hiyo inawafelisha makusudi ili wanafunzi waendelee kulipa ada na LST walipane mishahara na posho. Kwa miaka 5 inatumia bilioni 18 kutengeneza mawakili 100 na kuhakikisha wanasheria wanafunzi 3000 wanapoteza muda wao na dira za maisha.
 
Tuombe asitokee mtawala atakayetamani kurudi Dar
Ni kawaida tu kubadili headquater inaweza ukawa hata Tanga,Njombe au Mtwara kigezo Cha katikati ni kigezo kilichopitwa na wakati kwa Leo watu hawatembei sana kufuata huduma na hii ndio itaifanya Dodoma ichukue miaka na miaka kuwa Metropolitan City.
 
Tatizo ni maslahi, LST inajiendesha kwa ada inazokusanya kutoka kwa wanafunzi. Kwa hiyo inawafelisha makusudi ili wanafunzi waendelee kulipa ada na LST walipane mishahara na posho. Kwa miaka 5 inatumia bilioni 18 kutengeneza mawakili 100 na kuhakikisha wanasheria wanafunzi 3000 wanapoteza muda wao na dira za maisha.
Ile time ya Mwaki Embe imeshatoa report yake?
 
Ila mji wa kiserekali umejegwa vizuri Sana ukikamilika utakuwa moja ya vivutio maana sio Kwa majengo yale
 
Kweli hata mimi hilo limenishangaza. Yaani ujenge kastendi kadogo halafu baada ya miaka mitano ipangwe mipango ya kujenga stendi nyingine!

Ukifanya tathmini utagundua idadi ya abiria imeongezeka na route pia. Miaka saba iliyopita nilipofika Dodoma kulikuwa hakuna route ya Dom to Musoma, Dom to Tarime, Dom to Bukoba. Lakini kwa sasa idadi ya route imeongezeka sana hence idadi ya mabasi kuongezeka. Kiongozi hatakiwi kulaumu tu, anatakiwa kutoa na solution
Dodoma umekuja lini???! Bus la bunda express umelikuta? Mohmed bus ulizikuta?
 
Msukuma pamoja na uccm wake bado ametoa hoja ya msingi moja tu, kwa nini dodoma kulijengwa soko la Ndugai??? je kiasi gani kimeshakusanywa ukilinganishwa na malengo ya makusanyo yaliyokuwepo?? soko la Ndugai ni mradi wa kifisadi kama ulivyo mradi wa stendi kuu ya mabasi Nyamongoro iliyoko Mwanza.
 
Kaongea fact huyo Dr wa mchongo.
kwangu mm ijapokuwa soko liko nje kidogo nafikiri kunambi alikuwa anawaza 10 years to come.ingekuwa vigumu kujenga soko la namna hiyo kati kati ya mji pia miji huwa inapanuka kwa haraka na hapo baadaye hilo soko litakuja kuwa katikati ya mji.kwa sasa hatuwezi kuona faida yake sababu hakuna mtu atakayetoka mjini kulifuata hilo soko kwa kuwa bado kuna masoko mengi katikati ya mji.swala la hoteli kwa dodoma ni sawa kwa hadhi yake na aina ya watu wanaotembelea jiji hilo.kama kungekuwa na vivutio kama arusha,iringa,musoma ingekuwa siyo shida lkn kwa dodoma bado jiji halina attractions za kitalii.
 
Namuunga mkono kuhusu stendi za Mabasi. Mbali ya ufisadi nyingi zinaingiza hasara na usumbufu Kwa Wananchi kwenda mbali wakati stendi za zamani bado Zinakidhi mahitaji na zinafanya chini ya kiwango mfano ni Sumbawanga na Tanga.
Maendeleo sio kujenga vinavyo kidhi leo tu..umeshaambiwa by 2050 tutakuwa 150,000,000.
 
Back
Top Bottom