Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

Kuhusu soko la ndugai ,,, serikali ili miscalculate ..wangerenovate soko la majengo.likawa modern..
Kuhusu stendi Kwa geography ya dodoma stendi ingejengwa pale medeli karibu na NHC ili kuruhusu magari yanayotaka njia nne za dodoma kupark bila usumbufu..watu wengi hawaendi nane nane Kwa sababu ni usumbufu na ni gharama..mtu hawezi Toka mipango aende nane nane kupanda gari za Arusha wakati pale ni njiani ..au atoke Nala aende nane nane kupanda gari za mwanza ...
Cha kushauri serikali iwekeze zaidi maeneo ya nzuguni palipo stendi na soko na ikiwezekana wauze viwanja watu wahamie maeneo yale ...Kuna eneo kubwa liko wazi limeshikwa na serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tabu hii miradi haishirikishi jamii ile stend na soko la ndungai ingekuwa stend bora vingeongezewa thamani hitajika kwa kadri ya mazingira.

  • Ndungai kulitakiwa kuwe na ghorofa ambazo kungekuwa na wapangaji kwa juu bachelor house chumba na sebule ili wawe chanjo cha mahitaji kwa soko husika.
  • stend kulitakiwa kuwe na ghorofa ambazo kungekuwa na mahitaji yafuatayo
    • kumbi za sherehe
    • maofisi mabao hawa
    • hotel au Lodge pamoja na migahawa
  • pia zoo za wanyama wadogowadogo
  • bustani na sehemu za kuchezea watoto
nauhakika kungekuwa na tija kubwa
Lazima kuwe na pa kuanzia... then hayo yote yanafuata... mfano unajenga majengo ya kupangisha wakati huna ofisi za wafanyakazi, huna viwanda inshort huna economic trend za uhakika nani atapanga? Mimi sioni ubaya kwa miradi hiyo kuwa ndio starting point... then vichocheo vingine vinafuata.... ukiwa na infrastructure madhubuti unaanza kujenga uwezo wa pato la watu wako... unaangalia vyanzo vipya kwa kuviibua.. kwa sasa Msukuma alitakiwa afikirie nje ya box kuliko kutupa lawama za kijinga kwa mkurugenzi aliyesimamia kilichofanyika.
 
Usipinge tu! Kilomita kumi toka mjini kuelekea njia ya Morogoro unaingia stendi ya Mkoa, mbele yake kuna kambi ya Jeshi Ihumwa, kuna lami. Mbele ya hapo Mji wa serikali Mtumba (pazuri sana na kuna miundombinu safi kabisa), mbele ya Mtumba kuna hospitali ya Uhuru (mpya), mbele yake kuna njia panda ya kuelekea Ikulu ya Chamwino.

Ukipita njia ya Arusha, kilomita kumi kutoka Mjini kuna Chuo cha Mipango (lami), Kambi ya Jeshi Makutupora halafu barabara safi ya lami kuelekea Arusha.

Ukipita njia ya kuelekea Iringa barabara ya lami safi kabisa.

Lakini pia kuna ring road inajengwa, hii inazunguka nje ya Mji wa Dodoma. Lami ikikamilika viwanja vitaongezeka thamani na mji kukuwa. Pia itaondoa jam mjini kwa kuwa kwa sasa malori yanapita katikati ya Mji kuelekea Mikoa mingine.
Dodoma ni mji wa hovyo, haufai kuwa Makao Makuu ya Nchi yetu.
 
Kuna miradi ambayo ni ajabu serikali kuwa nayo. .hivi inaingiaje akilini halmashauri wajenge hotel ya nyota 3...kwanza ni Kwa namna gan walifanya investment analysis na kujua possible return..
Dodoma bado haina uwezo wa kuaccomodate nyota 3 Kwa sababu Ina kiwango kidogo Cha utalii na wageni wake wengi ni government servant ambao uwezo wao kuafford nyota 3 ni mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miradi mingi ya Dodoma haitakuja zalisha kutokana na aina ya wananchi wa Dodoma

Treni ya SGR ikimamilika ndo mtaamini Dodoma itapoteza watu kila weekend maana watakuwa na uhakika wa kurudi mapema.

Haya masaa 10 njiani hukera watu, treni ikitumia masaa 4 hadi Dodoma watu watakaa Dsm
Ndio maana spidi ya ununuzi Dodoma imeanza kupungua makampuni ya kuuza viwanja yanafuata watu hadi mahotelini kubembeleza wanunue viwanja
 
Dr Msukuma anawashinda wabunge na wanasiasa wengi sana Africa hii. Asante sana Professor Msukuma you are doing great keep up the good work, MAY ALL BLESS YOU WITH HEALTH, SANITY AND WEALTH
 
Soko au hoteli inahitaji long term plan gani? Hizo zinataka kujengwa na kuleta tija kuanzia mda huo huo
Tatizo Halmashauri zinasingizia kujenga mjini Kuna gharama kubwa ya fidia lakini wanasahau return on investment ya mjini ni ya muda mfupi kuliko kuweka mradi vichakani kwenye mitunduru eti wanatanua mjini.
 
Lazima kuwe na pa kuanzia... then hayo yote yanafuata... mfano unajenga majengo ya kupangisha wakati huna ofisi za wafanyakazi, huna viwanda inshort huna economic trend za uhakika nani atapanga? Mimi sioni ubaya kwa miradi hiyo kuwa ndio starting point... then vichocheo vingine vinafuata.... ukiwa na infrastructure madhubuti unaanza kujenga uwezo wa pato la watu wako... unaangalia vyanzo vipya kwa kuviibua.. kwa sasa Msukuma alitakiwa afikirie nje ya box kuliko kutupa lawama za kijinga kwa mkurugenzi aliyesimamia kilichofanyika.
shida ya CCM inawatu wengi wenye busara kuliko wenye akili na hawa wenye busara hawana akili tena na hawajui kama hawana akili tena hivyo(wamebaki kuwasujudia wanaotudhurumu) walitakiwa waingize na kuwapa madaraka vijana (na hapa sio watoto wa viongozi wanaowakumbatia) ambao wana vision na mission mpya ya utekelezaji
 
Mkuu unazingua mbona uko google tuu Dodoma City Hotel unaiona? Iko Mji wa Serikali na ni mali ya Jiji la Dodoma.
Acha kudanganya watu wew .. dodoma city hotel haipo mji wa serikali.ipo hapo jirani na makao makuu ya ccm . Nyerere square au paradise....kama hujafika dodoma ukae kimya usije umbuka ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom