Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

Msukuma pamoja na uccm wake bado ametoa hoja ya msingi moja tu, kwa nini dodoma kulijengwa soko la Ndugai??? je kiasi gani kimeshakusanywa ukilinganishwa na malengo ya makusanyo yaliyokuwepo?? soko la Ndugai ni mradi wa kifisadi kama ulivyo mradi wa stendi kuu ya mabasi Nyamongoro iliyoko Mwanza.
Hii ni akili ya kitanzania kabisa.

Wewe ulitaka wanjenge mjini afu 2040 wabomoe tena?
 
Stendi ya mabasi haiko mbali kivile, na ukubwa wake ni sahihi kwa sababu unapojenga mradi kama huo lazima uangalie miaka kadhaa mbele. Stendi imetulia na haina vurugu. Kutokuwa na magari mengi kwa sasa ni kufikiria mwisho wa pua.

Hii ni pia kwa soko la Ndugai, pale lilipo inaweza kuonekana mbali lakini lipo kilometa kama 8 kutoka city centre tena pembeni ya barabara kuu Baada ya miaka 10 litaonekana lipo ndani katikati ya Jiji. Kwa mfano kuna Watu wanatoka Tegeta (kilomita zaidi ya 20) kufuata bidhaa Kariakoo kwa hiyo hakuna ajabu, au alitaka lijengwe katikati ya Mji?!!

Kuhusu hoteli, ile siyo nyota tano labda nyota mbili au tatu ikikamilika. Ikipata usimamizi zuri itaingiza faida kwa sababu ipo katikati ya Mji karibu ya maeneo mengi muhimu.

Napinga miradi isiyokuwa na tija, lakini kwa hiyo miradi ya Dodoma ipo sahihi
Watanzania wachache sana watakuelewa, wengi washazoea majengo ya tembe kila mwaka wanabomoa.

Akili za kuangalia leo tu za Msukuma ndio hizo za watanzania wengi.

Hongera kwa hili bandiko.
 
Ile time ya Mwaki Embe imeshatoa report yake?
Walipewa mwezi mmoja kutoka tarehe 13 Oktoba 2022, kwa hiyo inatarajiwa watatoa ripoti yao tarehe ifikapo tarehe 13 Novemba 2022.
 
Hivi ukilaumu ujenzi wa stand kubwa kama ile ya Dodoma ina maana utapinga pia ujenzi wa barabra ya njia 6 kule Dar, maana hesabu ya ujenzi wake inapigia miaka takribani 10 au 20 mbele, AU hata ile aiport terminal 3 kule Dar mbona bado sehemu kubwa tu haijaweza kutumika,ni kwa sababu ya hesabu za mbali,ni kweli tunalaumu sasa hivi lakini manufaa yake tutayaona baadaye sana.
Msukuma darasa la 7 mchunga mbuzi hawezi ona miaka 20 au 30 ijayo yye ameona 2025 kwenye kujaza tumbo lake tu upuuuuuz kumsikikizaa msukuma
 
Usipinge tu! Kilomita kumi toka mjini kuelekea njia ya Morogoro unaingia stendi ya Mkoa, mbele yake kuna kambi ya Jeshi Ihumwa, kuna lami. Mbele ya hapo Mji wa serikali Mtumba (pazuri sana na kuna miundombinu safi kabisa), mbele ya Mtumba kuna hospitali ya Uhuru (mpya), mbele yake kuna njia panda ya kuelekea Ikulu ya Chamwino.

Ukipita njia ya Arusha, kilomita kumi kutoka Mjini kuna Chuo cha Mipango (lami), Kambi ya Jeshi Makutupora halafu barabara safi ya lami kuelekea Arusha.

Ukipita njia ya kuelekea Iringa barabara ya lami safi kabisa.

Lakini pia kuna ring road inajengwa, hii inazunguka nje ya Mji wa Dodoma. Lami ikikamilika viwanja vitaongezeka thamani na mji kukuwa. Pia itaondoa jam mjini kwa kuwa kwa sasa malori yanapita katikati ya Mji kuelekea Mikoa mingine.
Maendeleo si ya majengo ya serikali.

Maendeleo ni wananchi wenyewe, kujenga na kufungua biashara
 
Nafikiri hiyo treni ya sgr haitakuwa na ufanisi unaoutarajia. Mfano kidogo ni atcl, licha ya kuwa na ndege mpya lakini kutokana huduma mbovu, watu wanaona bora wapande basi
Watu hupanda basi sababu ya gharama

ATCL ndege zao hujaa sana kwa sasa, ukitaka jaribu book
 
Usipinge tu! Kilomita kumi toka mjini kuelekea njia ya Morogoro unaingia stendi ya Mkoa, mbele yake kuna kambi ya Jeshi Ihumwa, kuna lami. Mbele ya hapo Mji wa serikali Mtumba (pazuri sana na kuna miundombinu safi kabisa), mbele ya Mtumba kuna hospitali ya Uhuru (mpya), mbele yake kuna njia panda ya kuelekea Ikulu ya Chamwino.

Ukipita njia ya Arusha, kilomita kumi kutoka Mjini kuna Chuo cha Mipango (lami), Kambi ya Jeshi Makutupora halafu barabara safi ya lami kuelekea Arusha.

Ukipita njia ya kuelekea Iringa barabara ya lami safi kabisa.

Lakini pia kuna ring road inajengwa, hii inazunguka nje ya Mji wa Dodoma. Lami ikikamilika viwanja vitaongezeka thamani na mji kukuwa. Pia itaondoa jam mjini kwa kuwa kwa sasa malori yanapita katikati ya Mji kuelekea Mikoa mingine.
Kweli mkuu
 
Dodoma haihitaji stand zisizo na faida. Kumlaumu Kunambi siyo sahihii kabisa,yupo au wapo waliojivika umungu wa maamuzi ya nchi.Kunambi alikuwa anatekeleza matakwa yao.
Na si Dodoma tu,stendi nyingi zimejengwa mbali na sehemu iliyotakiwa kujengwa,na wakati mwingine ni kubwa kuliko mahitaji.
Ya Mbezi tu ndiyo imejengwa sehemu ambayo wananchi walishawekeza tayari na ndo maana pale kuna changamoto na pa moto sana kupata duka, kiwanja
 
Ila ile stend ya dodoma daaah ni hasara labda itafaa miaka 100 ujayo unaingia stend unakuta mabasi 8
Ya chato ndio kiboko,basi moja tu linaitwa sabuni,linatoka chato to mwanza
 
Ila mji wa kiserekali umejegwa vizuri Sana ukikamilika utakuwa moja ya vivutio maana sio Kwa majengo yale
Maendeleo ni watu au ya watu na si vitu vya serikali.
 
kwangu mm ijapokuwa soko liko nje kidogo nafikiri kunambi alikuwa anawaza 10 years to come.ingekuwa vigumu kujenga soko la namna hiyo kati kati ya mji pia miji huwa inapanuka kwa haraka na hapo baadaye hilo soko litakuja kuwa katikati ya mji.kwa sasa hatuwezi kuona faida yake sababu hakuna mtu atakayetoka mjini kulifuata hilo soko kwa kuwa bado kuna masoko mengi katikati ya mji.swala la hoteli kwa dodoma ni sawa kwa hadhi yake na aina ya watu wanaotembelea jiji hilo.kama kungekuwa na vivutio kama arusha,iringa,musoma ingekuwa siyo shida lkn kwa dodoma bado jiji halina attractions za kitalii.
Mbona Dsm KKOO soko limejengwa kati kati kabisa?
Masoko ya Magomeni, Kisutu yote yako km 5 ndani ya KKOO
 
Msukuma pamoja na uccm wake bado ametoa hoja ya msingi moja tu, kwa nini dodoma kulijengwa soko la Ndugai??? je kiasi gani kimeshakusanywa ukilinganishwa na malengo ya makusanyo yaliyokuwepo?? soko la Ndugai ni mradi wa kifisadi kama ulivyo mradi wa stendi kuu ya mabasi Nyamongoro iliyoko Mwanza.
Kuna mradi gani Tz ambao sio wa kifisadi?
 
Msukuma again!?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Kunambi ni kati ya vijana visionary waliowahi kuiongoza Dodoma.

Tangu atoke mapato sijui yanafanyiwa nini na akina Mafuru, Dodoma imedorora hata takakataka tu zimeshindikana kukusanywa, Msukuma aseme katika hili alilenga nini na ametumwa na akina nani!?

Kati ya miradi yote mitatu wa hoteli tu ndio mradi wa jiji mingine ni ya serikali kuu, naomba kurekebishwa.
 
Akichambua Ripoti ya CAG, Dr Msukuma Mbunge wa Geita vijijini amemlaumu Godwin Kunambi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza miradi inayoleta hasara.

Dkt. Msukuma amesema Ujenzi wa Hotel ya nyota 5 ni ubabaishaji mtupu.

Ujenzi wa Soko la Ndugai hauna tija na Fedha iliyowekezwa pale haitarudi.

Ujenzi wa Stendi za Mabasi ya mikoani ni ufisadi mtupu ukiondoa chache za miji mikubwa amesema Msukuma

Kuna haja gani ya Law School kuwepo wakati katika Wanafunzi 700 wanayofanya mtihani kila Mwaka wanafaulu 26 tu amehoji Dokta.

Inawezekana CAG naye huwa anapokea mlungula kwa sababu ziko Halmashauri bobezi kwa ufisadi lakini zimepewa Hati Safi, amesisitiza Daktari wa Heshima

Mwisho Dkt. Msukuma ameshauri utaratibu wa kuwapata Wakurugenzi wa Halmashauri ubadilishwe badala ya kuteuliwa wawe wanaomba kazi kwa kushindanishwa.

Chanzo: TBC
Dr. Musukuma alitulia yuko vizuri sana.
 
Unalinganisha upanukani wa Dsm na Dodoma?

Ni miaka 5 toka Serikali ihamie huko ila upanukaji wa mji ni mdogo mno
Huifahamu Dodoma.... kama kuna miji imekuwa kwa kasi ya kimbunga ni pamoja na Dodoma and i garantee you miaka kumi ijayo Dodoma itakuwa moja ya majiji makubwa nchini. Mfano mdogo ni kodi za majengo binafsi ya biashara.... kwa sasa imeongezeka mara nne mpaka tano kuliko miaka mitano iliyopita hizo ni sehemu za indictation za ukuaji wa mji. Ujenzi unaoendelea kwa kasi wa majengo ya ghorofa katikati ya mji... naongeleo barabara ya sita mpaka ya 11. Ukuaji wa usafiri wa umma Daladala, Taxi, Bajaj na pikipiki.... Purchesing power ya wakazi.... ongezeko la hotel, kumbi na mfanowe. Kudhani hiyo miradi ni hasara ni ujinga wa kufiri mbali... hata uwanja wa ndege Msarato ni 50 years solution to come.
 
Miradi mingi ya Dodoma haitakuja zalisha kutokana na aina ya wananchi wa Dodoma

Treni ya SGR ikimamilika ndo mtaamini Dodoma itapoteza watu kila weekend maana watakuwa na uhakika wa kurudi mapema.

Haya masaa 10 njiani hukera watu, treni ikitumia masaa 4 hadi Dodoma watu watakaa Dsm
Hii inaweza kusaidia mtu kuishi Dar na kufanyia kazi Dodoma
 
Akichambua Ripoti ya CAG, Dr Msukuma Mbunge wa Geita vijijini amemlaumu Godwin Kunambi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza miradi inayoleta hasara.

Dkt. Msukuma amesema Ujenzi wa Hotel ya nyota 5 ni ubabaishaji mtupu.

Ujenzi wa Soko la Ndugai hauna tija na Fedha iliyowekezwa pale haitarudi.

Ujenzi wa Stendi za Mabasi ya mikoani ni ufisadi mtupu ukiondoa chache za miji mikubwa amesema Msukuma

Kuna haja gani ya Law School kuwepo wakati katika Wanafunzi 700 wanayofanya mtihani kila Mwaka wanafaulu 26 tu amehoji Dokta.

Inawezekana CAG naye huwa anapokea mlungula kwa sababu ziko Halmashauri bobezi kwa ufisadi lakini zimepewa Hati Safi, amesisitiza Daktari wa Heshima

Mwisho Dkt. Msukuma ameshauri utaratibu wa kuwapata Wakurugenzi wa Halmashauri ubadilishwe badala ya kuteuliwa wawe wanaomba kazi kwa kushindanishwa.

Chanzo: TBC
Sasa hapo ndio ameongea nini? Hilo la soko sawa ila hilo la Hoteli na stand kuna shida gani?
 
Hivi ukilaumu ujenzi wa stand kubwa kama ile ya Dodoma ina maana utapinga pia ujenzi wa barabra ya njia 6 kule Dar, maana hesabu ya ujenzi wake inapigia miaka takribani 10 au 20 mbele, AU hata ile aiport terminal 3 kule Dar mbona bado sehemu kubwa tu haijaweza kutumika,ni kwa sababu ya hesabu za mbali,ni kweli tunalaumu sasa hivi lakini manufaa yake tutayaona baadaye sana.
Stand sawa ila soko la Ndugai ni upuuzi tuu.
 
Back
Top Bottom