TANZIA Dkt. Muhammed Seif Khatib afariki dunia

TANZIA Dkt. Muhammed Seif Khatib afariki dunia

Speciality yake ilikuwa kumnanga Augustine Mrema.

Mzee wa Kiraracha alipogeuka kuwa political zero jamaa naye taratibu akapotea.
Really? Nilimsoma sana kwenye makala zake za Muungano wa Tangangika na Zanzibar
 
Mataifa yaliyoendelea vifo vya korona vimekuwa vingi kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa. Kwa nyakati hizi, na kwa nchi kama Tanzania iliyokusa uongozi thabiti wa kupambana na covid 19, si jambo la ajabu, mzee wetu huyu akawa amesombwa na ugonjwa huu.

Kwa mtu mwenye afya njema, miaka 70 ni mtu anayejimudu vizuri. Trump aligombea urais akiwa na umri gani? Papa Fransisco alipewa upapa akiwa na umri gani? Jakaya Kikwete ana umri gani? Bkhresa ana umri gani? Bilgates amebakiza miaka 5 tu kufikisha 70. Kabudi kabakiza miaka 5 kufikisha 70. Mfikirie Baba yako, mjomba wako, mama yako, kaka yako, wenye umri huo, unapenda wote wafe?

Dunia inawahitaji sana wazee, na wazee kwa maelfu Duniani biashara zao, uongozi wao, vitega uchumi vyao, ndivyo vinavyowategemeza vijana kwa mamilioni Duniani. Tunawahitaji sana wazee, wazee wana haki ya kuishi. Kuna wazee wengi wana mchango mkubwa kuliko hata vijana.

Hatuwezi kuzuia kifo lakini ni muhimu kuwalinda watu wetu kwa uwezo wetu wote kuhakikisha wanaendelea kuwa hai, wanaendelea kua na afya njema. Wazee hawa wanalipa kodi kuzidi hata vijana. Kodi hiyo inastahili kutumika kuwalinda na kuwahifadhi.

Pole sana familia ya Khatibu, pole wafanyakazi wote wa makampuni ya khatibu, pole kwa watanzania wote. Mungu wa rehema akupokee kwenye makao yake ya milele, na mema uliyowatendea wanadamu wenzako ulipokuwa duniani hii yamridhishe Muumba wetu kukutakasa ulipopungukiwa.

Kinachosumbua wengi ni uwezo mdogo wa kutafsri namba na elimu kiduchu ya demography.
 
Alikua muandishi mzuri sana wa ushairi.

Mungu ailaze roho yake pahala pema
 
Innaa milkullah yataswarrafu fiinaa kayfa yashaau
Dkt. Muhammed Seif Khatibu ambaye alikuwa ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa siku nyingi Serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi amefariki dunia. Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Uzini kisiwani Zanzibar.

Nyadhifa alizowahi kushika Dkt. Khatib
  • Mwenyekiti wa UVCCM kutoka 1978 hadi 1983.
  • Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kutoka 1978 hadi 2002.
  • Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na Habari.
  • Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo
  • Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Masuala ya Muungano

Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.



Dkt. Mohamed Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kupata shahada ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha Dodoma

Baada ya kuongea nae kwa kina, nikawa najiuliza sijui nianze na hili jina la Daktari ambalo alilipata rasmi mnamo Novemba 25, 2011 pale alipotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.

“Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Ni bahati ilioje mimi kuipata Shahada hii ya juu kitaaluma”-Dkt Seif Khatib

=====

Assallam allaykum,
Uongozi wa Zanzibar Media Coporation Ltd unasikitika kutangaza kifo cha Mkurugenzi mtendaji wake Dr. Muhammed Seif Khatib kilichotokea hii leo asubuhi, taratibu za mazishi zitatolewa na familia yake baadae hii leo. Seif Khatib (70), amefariki dunia leo Februari 15, 2021 asubuhi mjini Unguja.

Amewahi kuhudumu serikalini kwa nafasi mbalimbali kama waziri wa muungano/habari pia amewahi kuhudumu km Mkuu wa organizesheni wa ccm Taifa wakati huo akiwa mbunge wa Jimbo la uzini, hadi umauti unamkuta alikuwa akimiliki vyombo vya habari vya zenj fm/zenj tv pamoja na gazeti la Nipe habari

Ramadhan Sendah
Meneja mkuu.


--
Dkt. Khatib amewahi kushika nyadhifa nyingi na kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (1978-82), Katibu Mkuu Umoja huo (1982 - 88) ambapo hapo kwa vijana amekuwa kiongozi kwa miaka 10.

Amekuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na awamu ya Tatu ya Mhe. Mkapa na ya nne ya Dkt. Jakaya Kikwete (1988-2010), safari hiyo akianzia toka akiwa mbunge wa viti vya Vijana na baadaye wa Jimbo la Uzini tokea mwaka 1988 hadi alipostaafu mwaka 2015.

Vile vile amekuwa Mjumbe wa NEC ya CCM tokea 1978 hadi 2017, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (1995-2017), na baadaye Katibu wake wa Oganaizesheni 2012-2017.

Licha ya kuwa mwanasiasa mwenye nyadhifa mbalimbali, Dkt. Khatib katika muda wake wa ziada alikuwa mwandishi wa makala za michezo katika gazeti la Serikali la Daily News, gazeti la chama Uhuru na katika Mzalendo akiwika na makala yake mashuhuri KIPANGA.

Na hakuishia magazetini pekee. Huyu bwana pia ni Mwandishi mashuhuri wa vitabu vikiwemo “Fungate ya Uhuru”, “Wasakatonge”, “Chanjo”, “Vifaru Weusi”, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar” na “Taarab Zanzibar”.
 
Really? Nilimsoma sana kwenye makala zake za Muungano wa Tangangika na Zanzibar
Joseph Mihangwa alikuwa ahangaiki na makala za kina Mrema hao!
Makala zake huwa fikirishi sana. Gazeti la Raia Mwema la wiki hii, ameandika makala akionyesha mshangao kwa JPM kumpandisha cheo yule Jaji, eti kwa kuandika hukumu kwa Kiswahili.
Ametahadharisha kupata wataalam wasiostahili, ambao wamezawadiwa vyeo kwa style hiyo!
Aliyekuwa anahangaika na akina Mrema na Wapinzani wa CCM kwenye gazeti la Mzalendo, ni huyo Mohamed Seif Khatib, kwenye zile makala zenye jina la KIPANGA! Alikuwa wa hovyo huyoooo!!!!
 
Mara ya mwisho kukutana na kufanya naye mahojiano ni January 20 katika kongamano la siku ya Kiswahili duniani lililofanyika Dodoma mama Samia Suluhu Hassan akiwa ni mgeni rasmi alikuwa mzima bukheei wa Afya. Mara ya mwisho kusikia sauti yake ni katika PB on Saturday ya Clouds FM.

Ameona amfuate Brigadier Mbena fasta. Changamoto hii bhana.
January 20/ 1978 mpaka leo ?
 
Joseph Mihangwa alikuwa ahangaiki na makala za kina Mrema hao!
Makala zake huwa fikirishi sana. Gazeti la Raia Mwema la wiki hii, ameandika makala akionyesha mshangao kwa JPM kumpandisha cheo yule Jaji, eti kwa kuandika hukumu kwa Kiswahili.
Ametahadharisha kupata wataalam wasiostahili, ambao wamezawadiwa vyeo kwa style hiyo!
Aliyekuwa anahangaika na akina Mrema na Wapinzani wa CCM kwenye gazeti la Mzalendo, ni huyo Mohamed Seif Khatib, kwenye zile makala zenye jina la KIPANGA! Alikuwa wa hovyo huyoooo!!!!

Ni kweli mkuu.

Nimemchanganya Joseph Mihangwa wa Raia Mwema na Joseph Kulangwa aliyekuwa Mzalendo.

Nimtake radhi Joseph Mihangwa na wakuu wote kwenye huu uzi.
 
Tuko vizuri-.jpg
 
Back
Top Bottom