TANZIA Dkt. Muhammed Seif Khatib afariki dunia

Namkumbuka huyu dingi akiwa karibu mkuu wa umoja wa vijana Tanzania,
Mwenyekiti alikua Andrew masanje
Naibu karibu mkuu alikua,William lukuvi,ambae Sasa ni waziri wa ardhi.
Wengine ni said thabit mwambungu aliekua mkuu wa mkoa ruvuma wakati wa JK,kwa sasa ni marehemu.
Abubakar mwinyimvua Ally alikua mkuu wa idara ya uenezi na ushirikishwaji ya umoja wa vijana.
Wengine ni sukwa saidi sukwa,Yuko ccm Zanzibar.
Nadhani lukuvi atahudhuria maziko.
Vijana wa too whasap hawawezi wajua Hawa madingi.
Mwingine ni nurdin mohamedi Babu,kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Serengeti,kipindi hicho bado akiwa chalii Sana,alikua kwenye chipukizi,wakampromoti kuka kwenye vijana.
 
Vijana acheni kuwatembelea wazee wenu kwa sasa mnaweza kuwapelekea magonjwa wakashindwa kuhimili kirusi. Tuwalinde watu wazima na wenye maradhi. Vijana mnaweza kuwa na immunity kubwa wala msisikie kitu lakini ukaweka hatari wengine. Najuwa kuna watu wanavaa barakoa kwa sasa japo mikutano ya siasa hawataki kuvaa. Kitu kimoja ningemuombe mkuu shule azifunge ni hatari sana kwa kweli.
 
Pole kwa Familia na CCM wote, Wanasiasa na Watanzania waliokuwa wakimkubali.

Nimependa sana Wasifu wake hasa wa Kitaaluma ( Kielimu ) ila nilishtuka kidogo nilipoona kuwa ana Doctorate ya Dodoma University ( UDOM )

Itanichukua muda Kuiamini Elimu ya UDOM.
 
Aliandika Kitabu kimoja kinaitwa Fungate ya Uhuru. Kwenye Kitabu hicho enzi zake aliponda sana tabia ya watawala wetu kujisahau kuwatumikia wananchi na badala yake wanaendelea kusherehekea uhuru kwa kuwanyonya wanyonge wakati wao wakineemeka kwa raslimali na fdha za umma huku wakiwanyima wananchi uhuru halisi wa kutoa mawazo yao na kudai utumishi toka kwa viongozi wao.

Bahati mbaya ni kwamba baada ya kuona yupo nje ya mfumo wa utawala kwa muda mrefu alivutiwa na mapaja ya kuku yanayoliwa kwenye hiyo fungate na watawala na baadaye alikuja kuungana na tabaka tawala kula fungate hadi mauti ilipomkuta
Alishindwa na hakuthubutu kuighani kazi yake ya fungate ya uhuru hadharani. Hasa baada ya yeye kuwa mwanafungate
Aina ya wasomi wanafiki. Akamsalimie Ben
 
Kwa asilimia mia moja hukuelewa kabisa thread kabisa. Soma tena uelewe. Hakuna panapoonesha Seif kafa kwa korona.
 
kwa picha tu inasadifu mzee alikuwa kala chumvi hasaaa.Ni natural death. Kila la kheri pumzka kwa amani comrade. Tutakukumbuka kwa mchango wako ulioutoa ktk taifa hili la Tanzania.
Mataifa yaliyoendelea vifo vya korona vimekuwa vingi kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa. Kwa nyakati hizi, na kwa nchi kama Tanzania iliyokusa uongozi thabiti wa kupambana na covid 19, si jambo la ajabu, mzee wetu huyu akawa amesombwa na ugonjwa huu.

Kwa mtu mwenye afya njema, miaka 70 ni mtu anayejimudu vizuri. Trump aligombea urais akiwa na umri gani? Papa Fransisco alipewa upapa akiwa na umri gani? Jakaya Kikwete ana umri gani? Bkhresa ana umri gani? Bilgates amebakiza miaka 5 tu kufikisha 70. Kabudi kabakiza miaka 5 kufikisha 70. Mfikirie Baba yako, mjomba wako, mama yako, kaka yako, wenye umri huo, unapenda wote wafe?

Dunia inawahitaji sana wazee, na wazee kwa maelfu Duniani biashara zao, uongozi wao, vitega uchumi vyao, ndivyo vinavyowategemeza vijana kwa mamilioni Duniani. Tunawahitaji sana wazee, wazee wana haki ya kuishi. Kuna wazee wengi wana mchango mkubwa kuliko hata vijana.

Hatuwezi kuzuia kifo lakini ni muhimu kuwalinda watu wetu kwa uwezo wetu wote kuhakikisha wanaendelea kuwa hai, wanaendelea kua na afya njema. Wazee hawa wanalipa kodi kuzidi hata vijana. Kodi hiyo inastahili kutumika kuwalinda na kuwahifadhi.

Pole sana familia ya Khatibu, pole wafanyakazi wote wa makampuni ya khatibu, pole kwa watanzania wote. Mungu wa rehema akupokee kwenye makao yake ya milele, na mema uliyowatendea wanadamu wenzako ulipokuwa duniani hii yamridhishe Muumba wetu kukutakasa ulipopungukiwa.
 
Mkuu, Mungu ndiye Mwenye ratiba ya maisha ya wote Wenye miili, Ni Bora ujifunze kuwa na upendo tu Maana haikusaidii kumchukia mtu na kumwombea kifo wakati mtoa amri ya Nani aanze ni huyohuyo anayefahamu kwamba wewe utaondoka lini,

Na wakati mwingine ratiba ya wewe kuondoka inaweza kuwa iko Mbele ya unayemuombea afe halafu yeye akakaa miaka mingi Kwa kuku double maisha yako

Unachotamani kifanyike mpangaji wake Hana ushirika na Ujinga huo
Vipi Mungu alikuwa na ushirika na ule UJINGA wenu wa kutaka kumuuwa Lisu kwa risasi mpaka mkamtia kilema cha maisha?
 
Mkuu, Mungu ndiye Mwenye ratiba ya maisha ya wote Wenye miili, Ni Bora ujifunze kuwa na upendo tu Maana haikusaidii kumchukia mtu na kumwombea kifo wakati mtoa amri ya Nani aanze ni huyohuyo anayefahamu kwamba wewe utaondoka lini,

Na wakati mwingine ratiba ya wewe kuondoka inaweza kuwa iko Mbele ya unayemuombea afe halafu yeye akakaa miaka mingi Kwa kuku double maisha yako

Unachotamani kifanyike mpangaji wake Hana ushirika na Ujinga huo
Vipi Mungu alikuwa na ushirika na ule UJINGA wenu wa kutaka kumuuwa Lisu mpaka mkamtia kilema cha maisha
 
Mataifa yaliyoendelea vifo vya korona vimekuwa vingi kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa. Kwa nyakati hizi, na kwa nchi kama Tanzania iliyokusa uongozi thabiti wa kupambana na covid 19, si jambo la ajabu, mzee wetu huyu akawa amesombwa na ugonjwa huu.

Kwa mtu mwenye afya njema, miaka 70 ni mtu anayejimudu vizuri. Trump aligombea urais akiwa na umri gani? Papa Fransisco alipewa upapa akiwa na umri gani? Jakaya Kikwete ana umri gani? Bkhresa ana umri gani? Bilgates amebakiza miaka 5 tu kufikisha 70. Kabudi kabakiza miaka 5 kufikisha 70. Mfikirie Baba yako, mjomba wako, mama yako, kaka yako, wenye umri huo, unapenda wote wafe?

Dunia inawahitaji sana wazee, na wazee kwa maelfu Duniani biashara zao, uongozi wao, vitega uchumi vyao, ndivyo vinavyowategemeza vijana kwa mamilioni Duniani. Tunawahitaji sana wazee, wazee wana haki ya kuishi. Kuna wazee wengi wana mchango mkubwa kuliko hata vijana.

Hatuwezi kuzuia kifo lakini ni muhimu kuwalinda watu wetu kwa uwezo wetu wote kuhakikisha wanaendelea kuwa hai, wanaendelea kua na afya njema. Wazee hawa wanalipa kodi kuzidi hata vijana. Kodi hiyo inastahili kutumika kuwalinda na kuwahifadhi.

Pole sana familia ya Khatibu, pole wafanyakazi wote wa makampuni ya khatibu, pole kwa watanzania wote. Mungu wa rehema akupokee kwenye makao yake ya milele, na mema uliyowatendea wanadamu wenzako ulipokuwa duniani hii yamridhishe Muumba wetu kukutakasa ulipopungukiwa.
kubashiri kubashiri whatever happens.
 
Vijana acheni kuwatembelea wazee wenu kwa sasa mnaweza kuwapelekea magonjwa wakashindwa kuhimili kirusi. Tuwalinde watu wazima na wenye maradhi. Vijana mnaweza kuwa na immunity kubwa wala msisikie kitu lakini ukaweka hatari wengine. Najuwa kuna watu wanavaa barakoa kwa sasa japo mikutano ya siasa hawataki kuvaa. Kitu kimoja ningemuombe mkuu shule azifunge ni hatari sana kwa kweli.
Kuna mwanafunzi alikufa kwa Corona huko bagamoyo aliuziwa tarehe 2.2.2021. Mwanafunzi yule wa kidato cha kwanza wa shule ya Mtipwili akijulikana kama Dosa mwinyimkuu serikali na mamlaka zilikataa kabisa asitangazwe wala kuweka Tarantino kwa shule husika.
Afu anakuja mtu anasema nchi inakiongozi mpenda watu???? Labda kuropoka
 
Nakumbuka mwaka fulani kama sikosei 2002 mwandishi mmoja nguli aitwaye Joseph Mihangwa aliwahi kuhoji kama Mohamed Seif Khatibu anaweza kughani mashairi yake.

Ndiyo.

Na hitimisho lilikuwa asingeweza.

Ila nadhani hilo halitahafifisha utamu wa mashairi yake wala ukweli wa mada za kimapinduzi zilizomo ndani yake.

Uzuri wa kitabu ni kuwa kikishaandikwa kinageuka kuwa nafsi huru ambayo yaweza kuwa tofauti kabisa na mtunzi.
 
Hapa mnaongelea nini jamani?
 
Back
Top Bottom