TANZIA Dkt. Muhammed Seif Khatib afariki dunia

TANZIA Dkt. Muhammed Seif Khatib afariki dunia

Ili kiumbe kife ni lazima itokee changamoto ya kupumua.

Kama kusingekuwa na changamoto za kupumua basi tusingekufa.

ndo mana hata kabla ya Corona watu walikuwa wanawekewa ventilator hospital.yaani wana matatizo ya kupumua.

Kama afya yako ina mgogoro ni wazi utaichukia corona.

Ila Mimi naona Bora niumwe corona kuliko kipindu pindu.
kwa picha tu inasadifu mzee alikuwa kala chumvi hasaaa.Ni natural deth.kilala kheri pumzka kwa amani comrade.tutakukumbuka kwa mchango wako ulioutoa ktk taifa hili la Tanzania.
 
Wakati mwingine Mungu hutumia matukio kuponya Taifa au kuonesha ukuu wake. Kifo Cha kamarada Dkt Mohhamed Seif Khatib kuna jambo tunataka kuoneshwa.

Kama kweli Tanzania hakuna Covid-19, na kutokana na Wana CCM wanavyopendana katika shida na raha, basi katika msiba na maziko ya Seif Khatib tunategemea kuoneshwa umati mtitiii wa wanaCCM wakimzika kada huyu maarufu.

Bila kuvaa barakoa, bila kujali social distance maana "Mungu wetu yupo", kwenye msiba huu lazima tuwaone
1. M/Kiti John Magufuli
2. Dk. Bashiru Ally
3. Jakaya Kikwete
4. Kinana
5. G. Mkuchika
6. Mzee Mwinyi
7. D. Msuya
8. Malecela
9. Ndugai
10. Familia ya Karume
11. Lowassa
12. Amos Makalla
13. Philip Mpango
14.........ongezea wewe.

Bila hao kumzika mwenzao aliyekitumikia chama kama Khatib, basi salaam kwa Magu kuwa huenda ni Chato tu hakuna "korona".
Nawasilisha.
 
Ni huzuni kwa waja wema......ni habari njema kwa wanasiasa wanaotumia vifo vya watu kama ngazi ya kujiinua kisiasa.......

Mungu amuhifadhi anapopastahili........
 
Unaweza kuta kuna ambao wameshakula chanjo, ndio maana hawana wasiwasi
 
Sijkuelewa. Una maanisha nini kuwataja hao wote?

Kwa Seif Khatibu kafa kwa COVID 19?

Kwa hiyo siyo rahisi "Covid 19 vulnerable Rais John Pombe Magufuli" na wazee wenzake kwenda kumzika mzee mwenzao?
 
Kama ulikuwa ni msomaji wa vitabu vya mashairi au diwani basi huyu ndiye muandishi wa diwani ya wasakatonge hakika taifa limempoteza mtu muhimu na aliyeleta mchango mkubwa katika fasihi andishi na lugha ya kiswahili mwenyezi mungu amrehemu
 
Unazungumziaje wapinzani waliouwawa kwa maagizo ya viongozi wa ccm wenye uchu wa madaraka, ili ccm iendelee kukaa madarakani kwa shuruti? Hayo pia ni mapenzi ya Mungu?
Mungu atajilipiza mwenyewe kama hayo Ni kweli!!

Lakini ukumbuke pia Mungu Hana ushirika na yeyote, analoamua yeye huwa!

Sasa usijeshangaa siku moja unaodhani ni wabaya wako ukawakuta katika Raha ya milele!
 
Back
Top Bottom