PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,786
- 35,916
Na yeye amepata ajali au ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aliandika Kitabu kimoja kinaitwa Fungate ya Uhuru. Kwenye Kitabu hicho enzi zake aliponda sana tabia ya watawala wetu kujisahau kuwatumikia wananchi na badala yake wanaendelea kusherehekea uhuru kwa kuwanyonya wanyonge wakati wao wakineemeka kwa raslimali na fdha za umma huku wakiwanyima wananchi uhuru halisi wa kutoa mawazo yao na kudai utumishi toka kwa viongozi wao.
Bahati mbaya ni kwamba baada ya kuona yupo nje ya mfumo wa utawala kwa muda mrefu alivutiwa na mapaja ya kuku yanayoliwa kwenye hiyo fungate na watawala na baadaye alikuja kuungana na tabaka tawala kula fungate hadi mauti ilipomkuta
siku hizi kifo ni changamoto tu, sio amri na mapenzi ya Mungu tena?Mara ya mwisho kukutana na kufanya naye mahojiano ni January 20 katika kongamano la siku ya Kiswahili duniani lililofanyika Dodoma mama Samia Suluhu Hassan akiwa ni mgeni rasmi alikuwa mzima bukheei wa Afya. Mara ya mwisho kusikia sauti yake ni katika PB on Saturday ya Clouds FM.
Ameona amfuate Brigadier Mbena fasta. Changamoto hii bhana.
kwani huko kwenye sayansi hawafi?Namba zina soma kwa kasi sana...Sayansi HAIDANGANYI ...na matunguli hayajawahi kushinda Sayansi....
kwani kabla ya corona hakukuwa na vifo?Wakati mwingine Mungu hutumia matukio kuponya Taifa au kuonesha ukuu wake. Kifo Cha kamarada Dkt Mohhamed Seif Khatib kuna jambo tunataka kuoneshwa...
akili za ajabu sana hizi, kwani ukitangaza kama ipo ndo itaisha au watu hawatakufa tena?Sijui jamaa anataka afe nanii ili atangaze hali ya dharura
Mtunzi wa kitabu maarufu " WASAKATONGE" Inna lillah wa inna ilahy rajiunDkt. Muhammed Seif Khatibu ambaye alikuwa ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa siku nyingi Serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi amefariki dunia. Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Uzini kisiwani Zanzibar.
Nyadhifa alizowahi kushika Dkt. Khatib
- Mwenyekiti wa UVCCM kutoka 1978 hadi 1983.
- Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kutoka 1978 hadi 2002.
- Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na Habari.
- Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo
- Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Masuala ya Muungano
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.
Dkt. Mohamed Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kupata shahada ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha Dodoma
Baada ya kuongea nae kwa kina, nikawa najiuliza sijui nianze na hili jina la Daktari ambalo alilipata rasmi mnamo Novemba 25, 2011 pale alipotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.
“Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Ni bahati ilioje mimi kuipata Shahada hii ya juu kitaaluma”-Dkt Seif Khatib
=====
Assallam allaykum,
Uongozi wa Zanzibar Media Coporation Ltd unasikitika kutangaza kifo cha Mkurugenzi mtendaji wake Dr. Muhammed Seif Khatib kilichotokea hii leo asubuhi, taratibu za mazishi zitatolewa na familia yake baadae hii leo. Seif Khatib (70), amefariki dunia leo Februari 15, 2021 asubuhi mjini Unguja.
Amewahi kuhudumu serikalini kwa nafasi mbalimbali kama waziri wa muungano/habari pia amewahi kuhudumu km Mkuu wa organizesheni wa ccm Taifa wakati huo akiwa mbunge wa Jimbo la uzini, hadi umauti unamkuta alikuwa akimiliki vyombo vya habari vya zenj fm/zenj tv pamoja na gazeti la Nipe habari
Ramadhan Sendah
Meneja mkuu.
--
Dkt. Khatib amewahi kushika nyadhifa nyingi na kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (1978-82), Katibu Mkuu Umoja huo (1982 - 88) ambapo hapo kwa vijana amekuwa kiongozi kwa miaka 10.
Amekuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na awamu ya Tatu ya Mhe. Mkapa na ya nne ya Dkt. Jakaya Kikwete (1988-2010), safari hiyo akianzia toka akiwa mbunge wa viti vya Vijana na baadaye wa Jimbo la Uzini tokea mwaka 1988 hadi alipostaafu mwaka 2015.
Vile vile amekuwa Mjumbe wa NEC ya CCM tokea 1978 hadi 2017, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (1995-2017), na baadaye Katibu wake wa Oganaizesheni 2012-2017.
Licha ya kuwa mwanasiasa mwenye nyadhifa mbalimbali, Dkt. Khatib katika muda wake wa ziada alikuwa mwandishi wa makala za michezo katika gazeti la Serikali la Daily News, gazeti la chama Uhuru na katika Mzalendo akiwika na makala yake mashuhuri KIPANGA.
Na hakuishia magazetini pekee. Huyu bwana pia ni Mwandishi mashuhuri wa vitabu vikiwemo “Fungate ya Uhuru”, “Wasakatonge”, “Chanjo”, “Vifaru Weusi”, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar” na “Taarab Zanzibar”.
Nakumbuka mwaka fulani kama sikosei 2002 mwandishi mmoja nguli aitwaye Joseph Mihangwa aliwahi kuhoji kama Mohamed Seif Khatibu anaweza kughani mashairi yake.Alipopata vyeo serikalini hakuweza kamwe kuyaishi maandishi yake.
Lakini maadishi yake yataendelea kumuenzi.
Apumzike kwa amani.
Poleni Ndugu , Jamaa na Marafiki.View attachment 1702847
Hii ndio taarifa mpya kutoka Zanzibar
Huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa siku nyingi serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi .
Innalillah ya Innalillah Rajuun
Amefia Dodoma au Zanzibar? Maana kifo chake kina utata.
Ngoja niandike kiswahili cha kiarabu " kul nafsi dhaalikatul maut"Kila nafsi itaonja mauti!
Mzee larry king alikuwa na umri mkubwa still korona imepita nae, kwahiyo hata wazee korona inachukuakwa picha tu inasadifu mzee alikuwa kala chumvi hasaaa.Ni natural death. Kila la kheri pumzka kwa amani comrade. Tutakukumbuka kwa mchango wako ulioutoa ktk taifa hili la Tanzania.