Dkt. Mwaka ajitafakari. Upendo ukiisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee

Dkt. Mwaka ajitafakari. Upendo ukiisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee

View attachment 2510019
Kuna kipindi sisi wanaume huwa tunajipalilia maanguko yetu sisi wenyewe. Haijalishi umempenda mtu kiasi gani, ikifikia wakati upendo ukaisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee.

Kupitia hili sakata la Mwaka na mke wake, Mwaka anaweza akahisi ameshinda, ila daima mwanamke sio wa kumfanya adui yako, hasa mwanamke ambae anajua undani wako.

Bila kujua Mwaka anapigwa laana na machozi ya mkewe, watoto wake na hata watu wengine wanaouguswa na haya mambo.

Sio kwa kuwa biased, ila Mwaka ana kila traits za Sadisit (mtu anaepata faraja katika maumivu ya wengine) na hili halitamalizika vyema kwake.
si huyu aliyewahi kwenda na mwaka studio wakajiona ndoa yao ni bora kuliko ndoa zote Tanzania?
 
Sasa sijui anajisikiaje huyo aliyelala nae akiona mume hataki kutoa talaka kwa mke mwenzie,, inaonekana hili lidada litamu sana, yani happ dokta anazidi kumuweka sokoni hajui tu
Dada anaonekana mtamu,Mwaka anaona akitoa talaka tu ndoa inaitika na kwa sheria ya dini mke ukimuacha akiolewa mpaka achike ndipo unaweza muoa tena.
 
Itamtafuna sana huyo Dr. Mwaka laiti angejua kuna siku itafika atakuwa hoi kitandani na mtu ambaye anaweza kuwa msaada ni huyo mwanamke basi angetulia. Hakunaga mapenzi kwenye nyakati za starehe na burudani bali utapeli mtupu.

Huyo anayemuona ana mahaba na mbora wa kila kitu ndio nyoka hasa ambaye atakuja kumpa suprise ya ajabu na dunia nzima itashangaa. Siku zote mkataa pema pabaya panamuita.
Mimi nili conclude Mwaka ndo problem baada ya huyu mama kusema hakulipa school fees mwaka mzima,
na hataki urafiki, kumekuwa uadui.
ambacho huwa kina affect watoto hasa kwenye talaka ni uadui,
so naona hekima ya baba mwenyewe ya kutelekeza watoto na kuweka uadui!!
 
Haijalishi kuwe na pande mbili au tatu kila mtu ana mapungufu yake kwenye Ndoa.Mungu alikuwa na maana yake alipo weka TARAKA
Point yako hasa ni nini mpendwa?

By the way japo umeiandika kwa herufi kubwa inapsaswa kuwa TALAKA na si TARAKA.

Sijapinga maana ya Mungu kuweka TARAKA (kama ulivyoiita) nilichosema ni kuwa kila jambo lina pande mbili, tusikae kushupaza shingo kutokujua undani hasa wa ndoa yao. Walipokuwa pamoja kama wapenzi sisi hatukuwepo.
 
Point yako hasa ni nini mpendwa?

By the way japo umeiandika kwa herufi kubwa inapsaswa kuwa TALAKA na si TARAKA.

Sijapenga maana ya Mungu kuweka TARAKA (kama ulivyoiita) nilichosema ni kuwa kila jambo lina pande mbili, tusikae kushupaza shingo kutokujua undani hasa wa ndoa yao. Walipokuwa pamoja kama wapenzi sisi hatukuwepo.
Sawa msubiri Mwaka akuelezee ndipo utoe maamuzi.
 
Kama unaamini machozi au hata maneno tu ya mwanamke ukichilia mama yako basi wewe hujawajua wanawake au hata hujawasoma kwenye vitabu.

Ukitaka ujue ukweli waite wote meza moja halafu waambie waseme matatizo makubwa yao, unaweza ukalia kwa kumuonea huruma mwanaume ambaye kwenye machozi ya mwanamke yeye alikuwa anatabasamu.

Kwenye Camera mwanamke anaweza akasema kuwa mwanaume wake hajali au anachepuka, ila hakuna mwanaume anaweza kulisema hilo hadharani. Wanaume wengi wanateseka kwa hawa wanawake ila hawana pa kusemea.

Dr. Mwaka sio mjinga, na ukifatilia utagundua hajawahi kukataa kumuacha huyu Mama ndio maana alikuwa hata haendi kwake ila kuna mtego anategewa kwa kisingizio cha machozi.
 
Back
Top Bottom