Mkishafika hapa haijalishi nani mkosaji the only solution ni talaka tu,
Mwaka ampe mkewe talaka mana hapa ameshasema hata hizo mali hataki tena anataka tu amani ya moyo na watoto wake!
Mimi nashangaa sana watu wanaosema huenda huyo mwanamke anajiliza tu, awe anasema ukweli au uongo the fact that ameomba apewe tu talaka na mali ataziacha zote that speaks volume about Dr. Mwaka!
Mwaka amwache huyo mama aende jamani, au mpaka tusikie mtu amecommit suicide?
Amani ya moyo ni kila kitu humu duniani!
Kuna vitu mnatakiwa kujua hukmu yake kabla hajatoa ushauri wa nini kifanyike.
Talaka ina hukmu zake na baada ya kutolewa kuna masharti lazima yatekelezwe.
Kuhusu kuachana, Uislam unaruhusu Mwanamke kujivua kwenye ndoa kama atakuwa ana sababu na atatimiza masharti ya kujivua ambayo ni pamoja na kurudisha mahari aliyopewa.
Kwahiyo Dada yetu huyu ana nafasi ya kujivua kwa kuteleleza sharti hilo, kinyume chake Mwanaume akitoa talaka anatakiwa kutimiza masharti yote ambayo ni pamoja na kumfidia mwanamke baadhi ya mambo, ikiwemo kumpatia kiazio cha maisha, uhakika wa makazi baada ya hapo.
Sasa wanawake wa siku hizi, wanadai talaka ila wanalazimsha wanaume watoe talaka ili wanaume wawajibike kwenye kuwafidia kitu ambacho ni mtego.
Muulizeni Queen, je amefata taratibu za kujivua kwenye ndoa kwakuwa yeye ndio anadai talaka? Kwanini alazimishe Dr. Mwaka ataoe talaka yeye wakati yeye hakuwa na nia ya kumuacha mkewe?
Kinachotafutwa hapa ni kumuingiza Dr. Mwaka kwenye mtego, atoe talaka ambayo hakuowahi kuiombea ili baadae sheria ifate mkondo wake wa kugawana mali, na huyu Dada atakuja kusema mimi sikutaka hivyo ila sheria ndio zinataka tugawane na hapo mtakuja kusema hapa, yaani atatumia watu baki kujifanya wamemshauri na kumlazimisha na hapo ndio mtakuja kumhurumia Dr. Mwaka.
Mwisho, ajivue kwenye ndoa hiyo mwenyewe na kanuni zinasema, akijivua mwenyewe hakuna kufidiwa chochote na hakuna mgawanyo wa mali.