Dkt. Mwaka ajitafakari. Upendo ukiisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee

Dkt. Mwaka ajitafakari. Upendo ukiisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee

View attachment 2510019
Kuna kipindi sisi wanaume huwa tunajipalilia maanguko yetu sisi wenyewe. Haijalishi umempenda mtu kiasi gani, ikifikia wakati upendo ukaisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee.

Kupitia hili sakata la Mwaka na mke wake, Mwaka anaweza akahisi ameshinda, ila daima mwanamke sio wa kumfanya adui yako, hasa mwanamke ambae anajua undani wako.

Bila kujua Mwaka anapigwa laana na machozi ya mkewe, watoto wake na hata watu wengine wanaouguswa na haya mambo.

Sio kwa kuwa biased, ila Mwaka ana kila traits za Sadisit (mtu anaepata faraja katika maumivu ya wengine) na hili halitamalizika vyema kwake.
ALIMFUNGA MKEWE KISHIRIKINA SASA ALICHOKISHIKILIA KIKAMPAISHA KINAMTOKA LAZIMA AJIFANYE CHIZI.NI UPATAJI WA HOVYO WA KIROHO.
 
Kuna vitu vitatu muhimu sana kwenye hili sakata
1. Mwanamke ndio anataka talaka
2. Hataki kudhalilishana kwenye mitandao ya kijamii( hili nimempa big up sana)
3. Hataki kugombea mali anataka amani ya moyo aachwe alee wanae!
Kwa hizo point tatu unaweza kuona wazi tatizo liko upande gani
Mshana najua akili zako zinaona tatizo rohoni.Kuna mchawi anapambania nafsi ya mwenzake na wakirudiana hadumu.
 
Amemaanisha hivi wanawake wengi wanaonewa sana na hakuna sheria kali za kuwalinda asaidie wanawake wasionewe pia kuimarisha sheria kumlinda mwanamke
Unaongelea sheria za nchi gani dada angu? Kama ulikua ujui sheria za ndoa na mahusiano zinamlinda zaidi mwanamke. Uyo mwanamke afate utaratibu tu talaka atapata kwa mujibu wa dini yao mwanamke anaweza kutoa talaka ila atawajibika kulipa kila kitu alichopewa na mwanaume kuanzia mahari na mali zingine kama alipewa.
 
Walinunua nyumba ilala BOMA,kiwanja kina nyumba tatu,lakini inasomeka Moja waliuziwa Toka kwa familia na mwaka aliwaambia anamnunulia mkewe,mauziano yakafanyika watoto walikuwa watano iliuzwa sh 150milion ila Dr akawaomba waandike 80ml Ili waweze kushughulikia transfer Toka walipokabidhiana alimuandika Queen binti kashughulikia mpaka hati ikatoka maisha yakaendelea.
Aliyetoa pesa ya kununua nyumba ndie mwenye mali
 
Angekuwa na hekima angeomba watu wenye hekima kukutanishwa na mumewe ampigie magoti.
Hii ni sanaa kutaka huruma za watu tu.
Ampigie magoti KUMUOMBA AMUACHE??
Kama mwanamke hakutaki ACHANA NAE,WACHA KUNG'ANG'ANIA MKE ASIETAKA KUWA MKEO TENA!
 
Wanaume wa siku hizi hawaachiko kirahisi mpk zifanywe drama nyingi😂😂😂 kinachomuums dr makanjanja ni kutoa talaka akijua kuna mtu atachukua zigo😂😂,,

Hapa piga ua talaka yangu utatoa, atoe talaka wanaume wachukue zigo😂
Hajatoa na bado wahuni wanazagamua kama kawa.Yakiisha yaache yaishe!
 
Ampigie magoti KUMUOMBA AMUACHE??
Kama mwanamke hakutaki ACHANA NAE,WACHA KUNG'ANG'ANIA MKE ASIETAKA KUWA MKEO TENA!
Mkuu hivi umejiuliza chanzo cha mgogoro ni nini?
Mwanamke amezini halafu akimbilie kuomba talaka?
Mwaka ndiye aliyepaswa kuomba talaka sio huyu mnayemhurumia.
Mnadannganywa na machozi?
 
Shida ni wanawake wa sasa wanaangalia mahusiano kimasilahi sasa pale anapodai sana talaka lazima mwanaume lazima ushtuke mwenzangu ana ajenda gani huyu, nafikiri ugumu wa uyo Mwaka kutoa talaka upo kwenye mgawanyo wa mali, fikiria wanawake mlivyo wagumu kutoa hata elfu 10 tu kumsaidia mwanaume mnaona ni nyie tu ndio mna haki ya kusaidiwa na jinsia nyingine sasa mkiachana mwanaume inabidi akuachie nyumba aliyojenga kwa jasho lake bila wewe kuchangia hata tofari moja just imagine machungu yake. Uyo mwanamke kama anataka talaka atafute mwanasheria amwandalie document kwamba anataka talaka tu hana shida ya mali ili itambulike ivyo kisheria na sio maneno ya kujiliza mitandaoni tu. Wito wangu kwa wanawake ukitaka kuachana na mwanaume wako kwa amani rudisha kila alichokupa au mlipe gharama zote alizotumia kwa ajiri yako.. kama ni kiwanja, gari n.k mrudishie vitu vyake kama alikusomesha mlipe gharama zote alizotumia kukusomesha. Mapenzi yameisha kwa mwanaume ila hayajaisha kwa mali zake. Ridiculous.!
Kwani si alimzagamua hadi wakazaa jamani,, ukiachwa achika babu weee chombo bado kiko ng'aring'ari roho inauma kukiachia😜
 
Wanaume wa siku hizi hawaachiko kirahisi mpk zifanywe drama nyingi😂😂😂 kinachomuums dr makanjanja ni kutoa talaka akijua kuna mtu atachukua zigo😂😂,,

Hapa piga ua talaka yangu utatoa, atoe talaka wanaume wachukue zigo😂
Lakini kwanini sisi hatujwahi kuipenda kweli watu wangu?

Kosa la Mwaka liko wapi?

Unajua mwanaume unapokuwa na mke wako unamhudumia kwa kila hali halafu ghafla unamfumania analiwa na jitu labda limehonga mafuta ya 50k tu ni sawa?
Kwanini hamvai kiqtu cha Mwaka?
Kama Mwaka ana makosa na wameahindwa kusuluhishwa hapo sawa.
Lakini kwa ishu ya uzinzi tutetee uovu wanangu?
 
Nimegundua huyu mama ana hekima sana
... hata mimi nimeliona hilo; ni wife material. Huyu siku anapokea talaka yake siku hiyo hiyo anaolewa unless uniambie sijui kuna eda sijui vitu gani vya kumkwamisha temoprarily lakini "halali njaa" huyu! Na ndicho kinachomsumbua Mwaka.
 
Lakini kwqnini sisi hatujwahi kuipenda kweli watu wangu?

Kosa la Mwaka liko wapi?

Unajua mwanaume unapokuwa na mke wako unamhudumia kwa kila hali halafu ghafla unamfumania analiwa na jitu labda limehonga mafuta ya 50k tu ni sawa?
Kwanini hamvai kiqtu cha Mwaka?
Kama Mwaka ana makosa na wameahindwa kusuluhishwa hapo sawa.
Lakini kwa ishu ya uzinzi tutetee uovu wanangu?
Hivi kwani huyu dada alifumaniwa? Na hata km alifumaniwa bado yeye ndo anadai talaka shida iko wapi?

Kama sivyo mwaka anakosea ilitakiwa alimalizie hukohuko lisifikie hapa,, kwa picha ilivyo dokita anakosea kumtisha na kuzungusha kutoa talaka,, mwanamke akifikia hapa huwa haitakiwi kumng'ang'ania ampe talaka yake waachane, akaolewe kwingine na hiki ndicho mwaka kinamkoroga utumbo,, nimepitia kitu km hiki wanaume nawajua vizuri vichwa vyenu
 
Back
Top Bottom