TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

Nimesikia ni cancer ingekuwa vizuri kama ni cancer waseme ili kusaidia watu kwenye hospitali mapema. Cancer ni kuiwahi[emoji120] RIP
Ndugu cancer uwahi uchelewe kifo kipo pale pale... nimeuguza mgonjwa wa cancer naongea kwa uzoefu.
Kinachoongezeka ni siku tu za kuishi kwa aliyewah. Ila siku msipotegemea inakusaprize
 
Masikini Mwele RIP.
Huyu dada alikuwa mpiganaji na haogopi.
She took chances and had the courage ya kugombea urais 2015.
Pole sana family ya mzee Malecela.

Msy the Lord receive her soul.
 
Apumzike kwa amani mzalendo Dr. Mwele Ntuli Malecela



From the archives:

4 December 2019

Keynote Address by From Dr. Mwele Malecela, Director, Department of Control of NTDs, WHO.

Beautful brain and soul. Hizo akili zingefaa kutolewa akapewa MTU jamani. Very hardworking and innovative fellow. Rest Dr. Mwele♥️♥️♥️♥️🌹🌹🌹🌷🌷🌹🌹
 
Na huyo dada alikuwa sahihi kubeza kifo cha yule dhalimu. Huyu mama inatuuma maana alikuwa na utu, na hakuwa na kiburi cha madaraka. Huyu ataenda mbinguni, wakati dhalimu yuko motoni.
Sawa,wewe utaenda mbinguni,unaongea kama vile wewe ndio Mungu eti huyu mbinguni yule motoni!TRASH!!!
 

Lazima watu wafahamu kuwa kubaki duniani ni fursa ya kutengeneza maana kama kifo ni adhabu basi hakuna atakayekwepa!

Mungu ni mwenye huruma sana lakini hutupa kipimo kile kile kipimo tunachowapimia wengine!

Ukifurahia vifo vya watu lazima kuna ambao utawaumiza lakini siku nawewe utafiwa umpendaye na utapata maumivu yale yale uliyowapa wenzio!

Hakika tuna kila sababu ya kubadilika
 
RIEP Dr. Mwele, Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Kifo Ni adhabu ambayo walipewa baba yetu Adamu na Hawa pale bustanini na ndio kinatawala mpaka leo
 
Pole kwa mzee malecela Mungu awatie nguvu
Wabaya wetu Mungu anawahesabia muda na wakati sahihi
 
Kifo Ni adhabu ambayo walipewa baba yetu Adamu na Hawa pale bustanini na ndio kinatawala mpaka leo

Lakini si adhabu unayoweza kumuombea mtu usiyempenda ukidhani wewe utaikwepa!

Kama ni adhabu kimantiki basi kila mtu adhabu hiyo kila aliyezaliwa na mwanamke ataipata!
 
Pole sana wafiwa. Tumwombe Mungu wetu wa huruma, na muweza wa yote amjalie pumziko la milele mja wake.
 
Yah right. This is sad. Pole kwa Williams aka Field Mashal ES sauti ya Umeme toka enzi za jukwaa la BCS ya Nyaurawa (RIP) before Jambo Forums.
 
Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, Imani umeilinda.

Kwa wasio mfahamu Dr. Mwele, alikuwa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti ya kiafya Tanzania (NIMRI) Kabla Ya Kuondoshwa Kazini Rais Magufuli alipotangaza Kupatikana Kwa Visa Vya Ugonjwa Wa "Zika'' Hapa Nchini Tanzania.

Miezi michache baadaye yaani Mwezi Aprili 2017, Dr Mwele Malecela aliteuliwa na Shirika la Afya duniani (WHO) Upande wa Africa Akiwa Ni Msimamizi wa Masuala ya Utawala, Sera na Ushauri wa kidiplomasia Na Mkurugenzi Wa Idara Ya Magonjwa Ya Kitropiki Katika Shirika La Afya Duniani.

Mwaka 2015 Dr Mwele Alikuwa ni Miongoni mwa Wana CCM Walioomba Ridhaa Ya Kupeperusha Bendera Ya CCM Katika Nafasi Ya Urais Kwenye Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka 2015.

Dr.Mwele atakumbukwa kwa Uhodari, Utaaluma, Uchapakazi Na Uhodari Wake. Kwa hakika alikuwa Wa kuigwa Mfano Na Kuigwa Na Kila Mtu. Naam atakumbukwa kwa Misimamo yake na kusimamia taaluma yake bila kuogopa watawala.

Pumzika Kwa Amani Dkt Mwele
 
NIMRI ametumikia miaka mingapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…