TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

Halafu enzi Ile akiwa MEWATA yeye ndio alikuwa msimamizi wa Ile kampeni ya kupima kansa ya matiti. Kweli mganga hajigangi.
Mimi nilikuwa naishi Houston, Texas miaka kama 10 imepita. Kuna Dr mmoja wa Pharmacy nilikuwa nacheza naye Tennis alikuwa ametokea Nigeria.

Siku mmoja akaja kucheza Tennis akafa kwa stroke uwanjani pale. Kumbe alikuwa hatumia hata dawa ambazo madaktari walimpa za pressure. Madaktari wengi wanajiamini sana na hii sio nzuri. Lakini simuongelei huyu Mama maana sina habari za uhakika huu ni mfano tu
 
Sanaa,huwa nasikia vibaya Sana kuona mtu anafariki anaacha mzazi wake Kama alivyo mzee malecela...inaumiza Sana,,Ni vile tu kazi ya Mola Haina Makosa
Mwaka juzi niliumwa sana Baba yangu alilia na kuomba sana akisema nakuombea sana upone, ili wewe uje unizike miye. Huwezi amini nilipona na yeye alitwaliwa na muumba mwaka jana.
 
Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, Imani umeilinda.

Kwa wasio mfahamu Dr. Mwele, alikuwa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti ya kiafya Tanzania (NIMRI) Kabla Ya Kuondoshwa Kazini Rais Magufuli alipotangaza Kupatikana Kwa Visa Vya Ugonjwa Wa "Zika'' Hapa Nchini Tanzania...

Mungu ampokee katika makao yake. Naomba kuuliza: kwa theory ya CHadema kuwa Mungu anawaita waovu ili dunia ibaki salama. Je Huyu Dr. Kawakosea nini mpaka maombi yao yamemfanya Mungu amwite
 
Mkuu Mwaikibaki , asante kuni tag, it's so sad!.
Dr. Mwele ananihusu sana, kwanza nimesoma nae Primary, yeye alitangulia darasa moja, mimi nikisoma Class moja na mdogo wake, Mwendwa (Jaji)...
Pasco wa Iliboru wewe na yule mtoto wa Malechela Senyagwa (rip)aliyepata ajali akiendesha benzi pale Mbuyuni kati yenu nani alikuwa amemzidi mwenzie umri?
 
We umesoma na kila mtu
Mtu utasomaje na kila mtu?, mimi sijasoma na kila mtu, ila nimetokea kuwa na kumbukumbuku nzuri kwa niliosoma nao, au darasa moja, shule moja, au chuo kimoja, tena huwezi amini nawakumbuka kwa majina, toka niliosoma nao Kindergarten!, ila imetokea wengi niliosoma nao, tangu Primary, sekondari, A lever na Chuo, they happen to be somebodies!.

Tena huyu, sio tuu nimesoma nae, hadi kwao tumecheza!.

P
 
Pasco wa Iliboru wewe na yule mtoto wa Malechela Senyagwa (rip)aliyepata ajali akiendesha benzi pale Mbuyuni kati yenu nani alikuwa amemzidi mwenzie umri?
Senyagwa ndio wa kwanza kwao, Mwele ni wa pili, Mwendwa ni wa tatu, mwendwa ndio darasa moja na mimi, Ippy ni wa mwisho. Tukiwa primary alitutangulia, Mimi nimejiunga Tambaza form 1, Senyagwa yuko form V - PCM. Nikiwa form III, Mwele akaja Tambaza PCB.
P
 
Back
Top Bottom