TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

Kwamba Dkt Mwele kafariki...aiseee!!!
 
Hivi kwa nini Watanzania huwa tunafurahia vifo vya wenzetu?
Ni jambo la kawaida kwa watu kufurahia au kuua mtu ambaye anawatesa au anawapa kero iwe kijamii au kisiasa.

Majambazi, wezi, wachawi na hata wanasiasa waovu wanaotumia madaraka kutesa au kuua wengine wapo kwenye kundi hilo.

Vibaka, wezi na majambazi yanauawa Kila siku watu walifurahia. Hakuna cha ajabu hapa.

Ukitenda mema watu watasikitika ukifa, mabaya yatasababisha wafurahie kifo chako au hata kukifanikisha.
 
Hapa kwenye kifi Mwenyezi Mungu ameonyesha ufundi usiotikisika. Sisi wote tutakufa. Na hata tufanye nini, maisha yetu tulio wengi, ni ngumu kufika miaka mia na kadhaa kwa sasa.

Tuwe na kiasi. Tusifanye mambo kama vile tunaishi milele...maisha ya kutojari na kukandamiza wengine. Kudhulumu. Kuua na kadhalika
Ubinadamu wetu ulivyo, wazazi wanategemea watoto wawazike...lakini sio kila mzazi ana bahati hiyo. RIP Dr. Mwele
 
Ndugu cancer uwahi uchelewe kifo kipo pale pale... nimeuguza mgonjwa wa cancer naongea kwa uzoefu.
Kinachoongezeka ni siku tu za kuishi kwa aliyewah. Ila siku msipotegemea inakusaprize

Cancer inatibika ukiiwahi, kuna survivors wengi tu walioweza kuishinda cancer kwa matibabu...

Mambo huwa magumu pindi mtu anapochelewa kujua kama ana cancer...
 
Ndugu cancer uwahi uchelewe kifo kipo pale pale... nimeuguza mgonjwa wa cancer naongea kwa uzoefu.
Kinachoongezeka ni siku tu za kuishi kwa aliyewah. Ila siku msipotegemea inakusaprize

Pole sana kuna cancer ukigundua mapema zina zaidi ya 90< kupona mfano tezi dume mheshimiwa kikwete na mzee wangu waliwahi wakatolewa tezi dume bila hivyo ingekuwa ngumu.

Cancer ya maziwa na tumbo nayo ukifanya screening mapema inasaidia sana. Kuna tofauti sana na cancer ya stage 1 na cancer ya stage 3 au 4. Na mimi sisemi kwa hisia kuna data za kuthibitisha haya. Kosa tutakalo fanya ni kusema stage 1 and stage 3 au 4 ni sawa.
 
So sad!
I think her god needs her than we do.
RIP.
 
[emoji15][emoji15][emoji15]RIP[emoji29]
 
Mungu amlaze mahali pema peponi Dr Mwele Mengi mema kwa nchi yetu uliyatekeleza
 
Halafu enzi Ile akiwa MEWATA yeye ndio alikuwa msimamizi wa Ile kampeni ya kupima kansa ya matiti. Kweli mganga hajigangi.
 
Kifo ni safari ya kila binadamu.

Hakichagui maskini wala tajiri..utibiwe amana ama utibiwe majuu apollo kifo kikiamua kukubeba hutoki
Kila mmoja ana agano la uhakika na mauti, anytime (t) unaondoka hapa duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…